comte
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 9,019
- 6,825
Paskal, hawa watu wako wengi na wameweza. Hawa wa Helio Tower si tu kwmba wanaendesha bali pia walianzisha. Kongole kwao. Shida yetu kwa ujumla ni kukutaa kujifunza hata kwa vitu ambayo tunajua siyo sisi tuliovianzisha.Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la NIPASHE la Jumapili ya leo.
View attachment 3110071
Huu ni muendelezo wa sisi Watanzania kujitathmini uwezo wetu wa uongozi kwenye corporate level, jee Watanzania tuna uwezo wa kuongoza makampuni makubwa profitability, kama ATCL, SGR, TAZARA etc na yaka oparate kwa faida.
Kampuni ya Helios Towers Tanzania ni Kampuni ya kimataifa ya Uingereza, iko kwenye nchi 8 barani Afrika na Oman Arabuni. CEO wa Helios Towers ni Mtanzania, Gwakisa Stadi ambaye pia ni Boss wa Helios Towers Kanda ya Afrika Mashariki. Kati ya hizo nchi 8 za Afrika ambazo Helios Towers wapo, Ma CEO 3 ni Watanzania na habari njema zaidi ni hata CEO wa kwanza aliyeanzisha Helios Towers Oman, ni Mtanzania!.
Huu ni uthibitisho kuwa Watanzania tunaweza!. Kama Watanzania wameweza kwenye Helios Towers, huko kuingine kote Watanzania tunashindwa nini?.
Paskali
Miaka 1990s kwa mfano hatukuwa na ujuzi na weledi katika uchorongaji kwenye madini mpaka zilipokuka kampuni za uchorongaji kutoka nje. Leo zipo kampuni za watanzania za uchorogaji, zilizoajiri watanzania na zinafanya kazi maeneo mengi hapa Afrika.
Kweye sekta ya madini pia tunayo kampuni ya huduma za chakula ya AKO inahudumia migodi- ni ya mtanzania, imeajiri watanzania na inashindana na makampuni ya nje