Watanzania wenye vipato vya chini wanao somesha English Mediums wanateseka hadi nawaonea huruma

Watanzania wenye vipato vya chini wanao somesha English Mediums wanateseka hadi nawaonea huruma

Fateema

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2024
Posts
234
Reaction score
495
Nashukuru Mungu nilijitoa kwenye utumwa wa kujitakia na Sasa naishi kwa Amani kabisa watoto niliwatoa EM nimewaleta Kayumba sina Tena stress na mambo yanaenda vizuri na watoto wanafanya vizuri darasani. Twisheni ya nguvu. Aliyekuwa la 4 mwaka jana kapata A zote Masha'Allah.

Shoga zangu tuliokuwa tunasomesha wote EM karibu wote wamewarudisha Kayumba wanao wamebaki wachache ambao eti wanaogopa kuchekwa wataonekana wameshindwa maisha ila mateso Yao Sio ya dunia hii, mikopo kama yote, wananuka madeni na ndani hawana asset, hawana viwanja watoto wanalala chini ilimradi wasome EM..

Sasa najiuliza mateso yote hayo ya Nini wakati hata Kayumba wanaweza soma vizuri tu na Chuo wakafika kama.wanavyo fika wengine.

Poleni Sana watanzania wenzangu ambao bado mpo kwenye utumwa huo. Mungu awaongoze Sana mshituke mapema.

Sisemi kusomesha mtoto EM ni Vibaya ila Uwe na uwezo mkubwa Sana WA kifedha na assets za kutosha.
 
Tuishi kwa mujibu wa vipato vyetu..
Tusijitutumue ili mradi tuonekane, sio kwenye elimu tu, hata kwenye jambo lolote lile, ishi kwa uwezo wako, kisha ndio maamuzi yako.

Mengine yatakuwa maamuzi ya mtu binafsi, naweza kuwa na kipato ambacho kinamruhusu mwanangu kusoma English medium ila kama binafsi sipendelei asome huko nikimpeleka kayumba, sio kesi, shida ni hapo ambapo mtu unaforce, kipato chako ni kidogo ila unataka mtoto akasome english medium.

Binafsi mimi si muumini wa mtoto wangu kusoma english medium, haijalishi kipato kinaruhusu ama lah.
 
Kweli kabisa mkuu
 
Nashukuru Mungu nilijitoa kwenye utumwa WA kujitakia na Sasa naishi kwa Amani kabisa watoto niliwatoa EM nimewaleta Kayumba sina Tena stress na mambo yanaenda vizuri na watoto wanafanya vizuri darasani. Twisheni ya nguvu . Aliekuwa la 4 mwaka jana kapata A zote Masha'Allah.

Shoga zangu tuliokuwa tunasomesha wote EM karibu wote wamewarudisha Kayumba wanao wamebaki wachache ambao eti wanaogopa kuchekwa wataonekana wameshindwa maisha ila mateso Yao Sio ya dunia hii, mikopo kama yote, wananuka madeni na ndani hawana asset hawana viwanja watoto wanalala chini ilimradi wasome EM..

Sasa najiuliza mateso yote hayo ya Nini wakati hata Kayumba wanaweza soma vizuri tu na Chuo wakafika kama.wanavyo fika wengine.

Poleni Sana watanzania wenzangu ambao bado mpo kwenye utumwa huo. Mungu awaongoze Sana mshituke mapema.

Sisemi kusomesha mtoto EM ni Vibaya ila Uwe na uwezo mkubwa Sana WA kifedha na assets za kutosha .
Unamanisha sie waalimu wa shule za ummah kufjndisha watoto wetu English medium ni lack of financial literacy? Kwasababu take home yetu ni 800k kodi ya nyumba 200k chakula 300k I.e 10k@ per day usafiri 50k kwa mwezi dstv/ Azam king"muzi 35k bills za maji na Luku 20k, soft drink kazini 30k hiyo inao baki ndo tunapaleka kwenye basi ya njano, huo ni kua na financial mis management.
 
Mtoto akishaelewa kiingereza na kuwa na ufahamu mkubwa,inakuwa rahisi kwenda skondari yeyote.Wazazi wengi wamegundua shida ni kiingereza,huna haja ya kumpeleka tena sekondari za kulipia ghali.
Kiingereza anaweza jifunza hata akiwa kayumba. Jiulize hawa ma daktari wetu na ma engineer je walisoma english medium ?
 
Watakuja hapa na maneno ya ooooh mtoto apate exposure ,awe na marafiki wanaoweza kumsaidia hata akimaliza shule .

Ila anasahau kuwa huyo mtoto sio kuku kwamba utaendelea kumlea pale pale mtaani unaweza kuwa unampeleka mikoa tiafauti na zenye watu wa hadhi na bado akajenga uhusiano na watu mbalimbali .

Ni utumwa ,aisee ni utumwa Ila Mimi nafurahia waendelee kuzichanga alafu vitoto vikimaliza shule hawana hata Mia ya kuwapa Kama mtaji .

Nakala moja naituma kwa baba mdogo LIKUD
 
Kama huu mwezi Januari mpaka Febuari wanachanganyokiwa kabisa.
Hivi ni nani kawaroga hawa wajinga?
Unaingiaje kwenye vita na Taifa ambalo limekuzidi nguvu?
Someni Biblia mpate hekima
Upo sahihi kabisa mkuu yani wanajitesa na kuwatesa watoto wao ili kuprove Kwa watu kwamba wao matajiri..

Huyu shoga yangu shule imefunguliwa mtoto wake yupo nyumbani haendi shule Kwa sababu ada hana wenzake wanaenda shule ya Kayumba nzuri tu Tena ina geti wanafurahia ila yeye yupo nyumbani amekaa tu Sasa hivi anamkomalia mama Ake ampeleke kwenye shule hiyo ya wenzake
 
Nashukuru Mungu nilijitoa kwenye utumwa WA kujitakia na Sasa naishi kwa Amani kabisa watoto niliwatoa EM nimewaleta Kayumba sina Tena stress na mambo yanaenda vizuri na watoto wanafanya vizuri darasani. Twisheni ya nguvu . Aliekuwa la 4 mwaka jana kapata A zote Masha'Allah.

Shoga zangu tuliokuwa tunasomesha wote EM karibu wote wamewarudisha Kayumba wanao wamebaki wachache ambao eti wanaogopa kuchekwa wataonekana wameshindwa maisha ila mateso Yao Sio ya dunia hii, mikopo kama yote, wananuka madeni na ndani hawana asset hawana viwanja watoto wanalala chini ilimradi wasome EM..

Sasa najiuliza mateso yote hayo ya Nini wakati hata Kayumba wanaweza soma vizuri tu na Chuo wakafika kama.wanavyo fika wengine.

Poleni Sana watanzania wenzangu ambao bado mpo kwenye utumwa huo. Mungu awaongoze Sana mshituke mapema.

Sisemi kusomesha mtoto EM ni Vibaya ila Uwe na uwezo mkubwa Sana WA kifedha na assets za kutosha .
Usiishi kuliko uwezo wako. Ukiona unafanya vitu kwa kujitesa sana jua unaishi above your means.
Kuna mtu nilimwambia kuwa ukiona unaishi nyumba ambayo kodi yake ya miezi sita ni zaidi ya mapato yako ya mwezi, basi unaishi kwenye nyumba ambayo haiendani na wewe.
 
Back
Top Bottom