Watanzania wenye vipato vya chini wanao somesha English Mediums wanateseka hadi nawaonea huruma

Nashukuru Mungu nilijitoa kwenye utumwa wa kujitakia na Sasa naishi kwa Amani kabisa watoto niliwatoa EM nimewaleta Kayumba sina Tena stress na mambo yanaenda vizuri na watoto wanafanya vizuri darasani. Twisheni ya nguvu. Aliyekuwa la 4 mwaka jana kapata A zote Masha'Allah.

Shoga zangu tuliokuwa tunasomesha wote EM karibu wote wamewarudisha Kayumba wanao wamebaki wachache ambao eti wanaogopa kuchekwa wataonekana wameshindwa maisha ila mateso Yao Sio ya dunia hii, mikopo kama yote, wananuka madeni na ndani hawana asset, hawana viwanja watoto wanalala chini ilimradi wasome EM..

Sasa najiuliza mateso yote hayo ya Nini wakati hata Kayumba wanaweza soma vizuri tu na Chuo wakafika kama.wanavyo fika wengine.

Poleni Sana watanzania wenzangu ambao bado mpo kwenye utumwa huo. Mungu awaongoze Sana mshituke mapema.

Sisemi kusomesha mtoto EM ni Vibaya ila Uwe na uwezo mkubwa Sana WA kifedha na assets za kutosha.
Hongera yako kwa kuliona hilo na kutua huo mzigo. Kuna rafiki yangu mmoja amekuwa kama kachanganyikiwa, amejilazimisha kubeba mzigo unaozidi uzito wake, na hii ni sababu ya msukumo wa mke wake. Na jamaa anapenda sana gambe wakati mfukoni ni zero, masela wake wameamua kumtenga yaani yeye anapenda kununuliwa tu.
 
Government schools are better than english medium schools. Hii ndio topic ya kujadiliwa, lakini kwa upande wangu wakuu, kusomesha mtoto kayumba au EM ni kipato na utashi wa mzazi mwenyewe, manake kwanza hizi kayumba mwanafunzi ukiona amefaulu ujue alikuwa anapambana kweli kweli,huko EM ni ufaulishwaji tu,haiwezekani mtoto nilisoma nae,nilikuwa nampiga vibaya mno darasani eti kahamia EM eti amekuwa na uwezo ananipiga. mimi nimesomea kayumba nimemaliza O LEVEL 2019 na nimefaulu vema tu cjaona tofauti iliyopo kati ya EM na KAYUMBA. S3003/0014 2019 kode hiyo hapo mnaweza kuthibitisha matokeo yangu
 
Nyie wndeleeni kujifariji akayumba hamna kitu, ni kuanda watoto wa kufanya odd jobs kama bodo boda nk.

Ungesema international school Sawa lakini hawa EM ambao Mtaala wao ni uleule wa St. Kayumba. Waalimu ni walewale waliotokea St. Kayumba, wazazi kwa asilimia Fulani ni hawhawa huku mtaani ambao wenyewe kingereza kinawapiga chenga.
Sifikirii kama mawazo yako yatakuwa Sahihi.

Mimi kuna watu wamesoma hizo shule za English Medium lakini kuanzia matokeo ya kidato cha pili, cha nne, cha sita na Chuo niliwakimbiza.
Kingereza changu sio Fluently lakini ukiniletea hao waliosoma EM nawaburuza.

Niletee paper la kingereza Mimi niliyesoma Kayumba, na umtafute aliyesoma EM tufanye uone Nani atatoboa.

Huku mtaani, tunaendelea na maisha Mengine. Ambayo yapo Nje kabisa ya Elimu ya shuleni na sio ajabu tumeajiri waliosoma EM.(Ingawaje hii Sio hoja).

Alichosema makaveli10 ndio Hoja.

Suala la kufanya Kazi na akili za mtaani inategemea na mtoto mwenyewe yupoje
Kwa sababu wapo ambao wameishia Darasa la Saba lakini wanaupeo na uwezo Mkubwa mtaani kuliko Sisi tuliosoma
 
Kwa hali ya Sasa ilivyo haiepukiki kumtafutia mtoto elimu Bora ili aje ajisaidie siku za usoni huko.

Serikali haionyeshi u serious wowote kuboresha mfumo wa elimu kwenye public schools ili angalau kuwapunguzia wananchi mzigo, baadala yake wanaendekeza siasa wakati uhalisia wa hizi shule za serikali Kila mtu anauona.

Sasa huko EM wanafundishwa Mtaala upi?

Unajua watu kuna mambo hamyaelewi kuhusu suala la Elimu. Mtoto afundishwe juu ya mti, kwenye ghorofa, au popote pale kama Mtaala ni uleule. Inatarajiwa wote watapata lilelile.

Kwenye Elimu kuna mambo yafuatayo:
1. Sera ya Elimu ya nchi
2. Malengo ya Elimu katika nchi
3. Malengo ya Elimu kwa kila Kozi au Somo
4. Mtaala
5. Muhtasari wa kila Masomo.

Kama Lengo ni kumpeleka mtoto EM ajue kingereza Walau cha kung'atia half cake Sawa. Ila kama unafikiri atapewa Elimu tofauti na Ile ya Kayumba basi unapoteza pesa yako.
 
Ungesema international school Sawa lakini hawa EM ambao Mtaala wao ni uleule wa St. Kayumba. Waalimu ni walewale waliotokea St. Kayumba, wazazi kwa asilimia Fulani ni hawhawa huku mtaani ambao wenyewe kingereza kinawapiga chenga.
Sifikirii kama mawazo yako yatakuwa Sahihi.

Mimi kuna watu wamesoma hizo shule za English Medium lakini kuanzia matokeo ya kidato cha pili, cha nne, cha sita na Chuo niliwakimbiza.
Kingereza changu sio Fluently lakini ukiniletea hao waliosoma EM nawaburuza.

Niletee paper la kingereza Mimi niliyesoma Kayumba, na umtafute aliyesoma EM tufanye uone Nani atatoboa.

Huku mtaani, tunaendelea na maisha Mengine. Ambayo yapo Nje kabisa ya Elimu ya shuleni na sio ajabu tumeajiri waliosoma EM.(Ingawaje hii Sio hoja).

Alichosema makaveli10 ndio Hoja.

Suala la kufanya Kazi na akili za mtaani inategemea na mtoto mwenyewe yupoje
Kwa sababu wapo ambao wameishia Darasa la Saba lakini wanaupeo na uwezo Mkubwa mtaani kuliko Sisi tuliosoma
Mkuu tunapo enda shule, sio kwamba unafata content tu ya yale tunao fundishwa, hapana kuna vitu vingi tunavipata kutokana na mazingira tunao somea hususani mind set confidence connections future friends nk, sidhani kama ukiwa umesoma na mtoto wa mama tolie au bodaboda au au saidia fundi utapata mind set sawa sawa na ukisoma na mtoto wa dakitari waziri, Engineer nk....life is all about what you are after school......
 
Hongera yako kwa kuliona hilo na kutua huo mzigo. Kuna rafiki yangu mmoja amekuwa kama kachanganyikiwa, amejilazimisha kubeba mzigo unaozidi uzito wake, na hii ni sababu ya msukumo wa mke wake. Na jamaa anapenda sana gambe wakati mfukoni ni zero, masela wake wameamua kumtenga yaani yeye anapenda kununuliwa tu.
Duh inasikitisha Sana so kashindwa kusomesha? Au kaishiwa hela yote anapeleka English Medium?
 
Pesa ina nguvu, labda hao ambao wanao struggle kulipia ada watoto wao kitu ambacho pia ni kawaida katika maisha. Wewee ambae unasifia kayumba ndio nguvu ya pesa yako imeishia hapo na haimanishi kuwa hizo kayumba ni bora kuliko EM. Ajabu ninaloliona hapa ni kutaka kuufanya uwezo wako mdogo wa kipato kufanya shule hizo za K kuonekana ni bora. Siku uwezo wako wa kipesa ukibadirika utawaza tofauti. Kama watoto wenu wako vizuri katika shule za K basi elewa kuwa Kama wangekuwa EM basi wangekuwa vizuri zaidi kuliko walivyo sasa.
 
Kwamba hakuna mtoto alisoma English medium na ni bodaboda, yupo mtoto wa faza wangu mdogo.

Hicho kitu unachozungumzia ni kipana sana.
Na hakuna sehemu nimelazimisha mtoto asome kayumba hayo ni maamuzi yangu binafsi, jibu langu la kwanza kabisa nilisema, tuishi kwa vipato vyetu, tusijiumize kufanya jambo lolote lile, elimu, shughuli ama chochote kile.
Kama kipato kinaruhusu mpeleke mtoto huko EM.

ila nikasema binafsi yangu haijalishi kipato, mie mwenyewe nimeamua wanangu wasome kayumba.
Mbona WaPo wengi Sana wengine WaPo mtaani wanadanga.Mfumo wa elimu ya Tanzania unaotolewa na NECTA ni ule ule
 
Mkuu tunapo enda shule, sio kwamba unafata content tu ya yale tunao fundishwa, hapana kuna vitu vingi tunavipata kutokana na mazingira tunao somea hususani mind set confidence connections future friends nk, sidhani kama ukiwa umesoma na mtoto wa mama tolie au bodaboda au au saidia fundi utapata mind set sawa sawa na ukisoma na mtoto wa dakitari waziri, Engineer nk....life is all about what you are after school......

😂😂
Labda hujamuelewa Mtoa Mada vizuri kama ungemuelewa Wala usingetaja hao madaktari, sijui injinia and the likes.

Siku hizi hao bodaboda, Mama Ntilie, Machinga, Housegirl ndio wanapeleka watoto huko EM
Ada za EM nyingi zipo Kati ya 1.3M to 3M ndio Maana mtoa Mada kasema watu(yaani hao low class) wanachukua Mikopo ili watoto wao wasome shule za EM kwa mtazamo kuwa ndio shule nzuri.

So kama unafikiri shule anayosomea Mwanao wapo watoto wa madaktari, waalimu, Wanasheria au injinia utakuwa unakosea pakubwa Sana. Elewa huko EM siku hizi kumejaa watoto wa walalahoi kibao.

Labda ungesema International School ambazo Ada zake sio rafiki kwa Tabaka la chini hata wafanye nini.

Lakini hizo EM ambazo Ada ni 2M wengi wa watu wanajitutumua. Na wanasomesha huko.

So suala la connection Hilo achana nalo.
 
Government schools are better than english medium schools. Hii ndio topic ya kujadiliwa, lakini kwa upande wangu wakuu, kusomesha mtoto kayumba au EM ni kipato na utashi wa mzazi mwenyewe, manake kwanza hizi kayumba mwanafunzi ukiona amefaulu ujue alikuwa anapambana kweli kweli,huko EM ni ufaulishwaji tu,haiwezekani mtoto nilisoma nae,nilikuwa nampiga vibaya mno darasani eti kahamia EM eti amekuwa na uwezo ananipiga. mimi nimesomea kayumba nimemaliza O LEVEL 2019 na nimefaulu vema tu cjaona tofauti iliyopo kati ya EM na KAYUMBA. S3003/0014 2019 kode hiyo hapo mnaweza kuthibitisha matokeo yangu
Safi Sana mkuu .

Hakuna haja ya kupoteza hela Ems wakati uwezo wako mdogo wakati mtoto anaweza kusoma Kayumba ukamsimamia na akafaulu vizuri tu Hadi chuo
 
Cc LIKUD
Screenshot_20250107-172433_1.jpg
 
😂😂
Labda hujamuelewa Mtoa Mada vizuri kama ungemuelewa Wala usingetaja hao madaktari, sijui injinia and the likes.

Siku hizi hao bodaboda, Mama Ntilie, Machinga, Housegirl ndio wanapeleka watoto huko EM
Ada za EM nyingi zipo Kati ya 1.3M to 3M ndio Maana mtoa Mada kasema watu(yaani hao low class) wanachukua Mikopo ili watoto wao wasome shule za EM kwa mtazamo kuwa ndio shule nzuri.

So kama unafikiri shule anayosomea Mwanao wapo watoto wa madaktari, waalimu, Wanasheria au injinia utakuwa unakosea pakubwa Sana. Elewa huko EM siku hizi kumejaa watoto wa walalahoi kibao.

Labda ungesema International School ambazo Ada zake sio rafiki kwa Tabaka la chini hata wafanye nini.

Lakini hizo EM ambazo Ada ni 2M wengi wa watu wanajitutumua. Na wanasomesha huko.

So suala la connection Hilo achana nalo.
Sahihi kabisa mkuu
 
Umasikini kwenye familia kuondoka huhitaji mwingine ateseke kutoa wengine kimaisha wapate elimu bora

Hongera kwa kila mzazi ansyeteseka ssna kusomesha wanae shule nzuri

Mungu awabariki sana kuwapa elimu bora watoto wenu sio bora elimu

Mleta maana wewe kula bata usiteseke wala kusumbuka kusomesha shule nzuri ils ujue fainali ya maisha uzeeni.Utazeeka ukiwa hoi kama hukuwekeza vizuri kwa elimu ya watoto utakuwa hohehahe sana
 
Sio Kweli mkuu hiyo ni dhana potofu Sana kwani Kayumba hawafundishwi English?
Waziri wa elimu kakiri mwenyewe kuwa shule za secondary za serikali kufeli sana kunatokana na msingi mbaya wa kiingereza kwenye shule za msingi

Mbakize hukohuko.kayumba atakiona cga mtema kuni kwenye mitihani ya sekondari
 
Umaskiji kwenye familia kuondoka huhitaji mwingine ateseke kutoa wengine kimaisha wapate elimu bora

Hongera kwa kila mzazi ansyeteseka ssna kusomesha wanae shule nzuri

Mungu awabariki sana kuwapa elimu bora watoto wenu sio bora elimu

Mleta maana wewe kula bata usiteseke wala kusumbuka kusomesha shule nzuri ils ujue fainali ya maisha uzeeni.Utazeeka ukiwa hoi kama hukuwekeza vizuri kwa elimu ya watoto utakuwa hohehahe sana
Elimu hii hii ya mtaala wa NECTA?

Tell me ur kidding please
 
Back
Top Bottom