makaveli10
JF-Expert Member
- Mar 27, 2013
- 31,583
- 92,670
Utotoni nilisoma kayumba, maendeleo yangu school yalikuwa mazuri, mtaani watoto wa huko nilikuwa nawakimbiza kwa kuwafanyia maswali yao, kuna binti wa olympio, jamaa yangu yupo dycc(yemen) pale ye la 7 mie la 6 lakini pepa zao namsaidia fresh tu, ila pepa zetu hagusi, labda sababu nilikuwa najua hisabati kama kipaji lakini siamini hivyo naona wao walikuwa wakifundishwa kawaida mnoo tofauti na sisi.Kwanini mkuu?
Lakini kayumba naona nilijifunza mengi kuanzia maisha, kuna watu wanakuja viatu vimetoboka, shati halieleweki, tisheti imechoka, nikajifunza maisha kwa namna nyingine, kuna jamaa yetu alikuwa anakaa na mama wa kambo, huyu mapumziko tulikuwa tunamchangia hrla ili nae aenjoy.
Ubabe na vitu vingine, nilijifunza vingi ambavyo naamini kule st. Nini nini nisingeyaona.
Ila tu kama mtoto kichwa mbovu jitahidi kumsimamia, tuition ya kutosha, vitabu(material) yote awe nayo hapo itasaidia, tofauti na hivyo atateseka maana kayumba darasa kuwa na wanafunzi 70 mpaka 100+ ni kawaida tu.
Hivyo itakupasa umkomalie mtoto.