Watanzania wenye vipato vya chini wanao somesha English Mediums wanateseka hadi nawaonea huruma

Watanzania wenye vipato vya chini wanao somesha English Mediums wanateseka hadi nawaonea huruma

Waziri wa elimu kakiri mwenyewe kuwa shule za secondary za serikali kufeli sana kunatokana na msingi mbaya wa kiingereza kwenye shule za msingi

Mbakize hukohuko.kayumba atakiona cga mtema kuni kwenye mitihani ya sekondari
Acha kupotosha
 
😂😂
Labda hujamuelewa Mtoa Mada vizuri kama ungemuelewa Wala usingetaja hao madaktari, sijui injinia and the likes.

Siku hizi hao bodaboda, Mama Ntilie, Machinga, Housegirl ndio wanapeleka watoto huko EM
Ada za EM nyingi zipo Kati ya 1.3M to 3M ndio Maana mtoa Mada kasema watu(yaani hao low class) wanachukua Mikopo ili watoto wao wasome shule za EM kwa mtazamo kuwa ndio shule nzuri.

So kama unafikiri shule anayosomea Mwanao wapo watoto wa madaktari, waalimu, Wanasheria au injinia utakuwa unakosea pakubwa Sana. Elewa huko EM siku hizi kumejaa watoto wa walalahoi kibao.

Labda ungesema International School ambazo Ada zake sio rafiki kwa Tabaka la chini hata wafanye nini.

Lakini hizo EM ambazo Ada ni 2M wengi wa watu wanajitutumua. Na wanasomesha huko.

So suala la connection Hilo achana nalo.
Wamekalia connection connection me nahisi hawajawahi kusomesha English Mediums. Labda wana confuse Ems na International school.
 
Hizo sio bure nazo zina gharama. Hizi za bure ya mchango elfu 6 hazina english zaidi ya kukaririshwa kujibu somo lake
Sahihi chukua mtoto wa darasa la saba kayumba waongee kiingereza na mtoto wa English medium darasa la pili

Kitoto cha English Medium kitamtoa knock out huyo darasa la saba wa kayumba
Vinaongea kingereza kilichonyooka na vinajiamini.
 
Pesa ina nguvu, labda hao ambao wanao struggle kulipia ada watoto wao kitu ambacho pia ni kawaida katika maisha. Wewee ambae unasifia kayumba ndio nguvu ya pesa yako imeishia hapo na haimanishi kuwa hizo kayumba ni bora kuliko EM. Ajabu ninaloliona hapa ni kutaka kuufanya uwezo wako mdogo wa kipato kufanya shule hizo za K kuonekana ni bora. Siku uwezo wako wa kipesa ukibadirika utawaza tofauti. Kama watoto wenu wako vizuri katika shule za K basi elewa kuwa Kama wangekuwa EM basi wangekuwa vizuri zaidi kuliko walivyo sasa.
Hujaelewa Mada wewe mtoa Mada wala hamaanishi unacho sema wewe
 
Kuna tofauti kubwa ya tuition na shule. Shule mnatumia muda mwingi na maongezi yanakua marefu,tuition muda mchache,mtoto kachoka hivyo umakini unapungua.

Mamilioni ni mbwembwe tu za wazazi. Ndo maana unaona mtu anasomesha shule za mamilioni bado anamtafutia mwanae connection za kazi mfano mzuri mwigulu,mwanae yupo feza international ila bado anamhangaikia vinafasi uvccm ya watoto
Sawa lakini Sio sawa na kutoa mamilioni mkuu.

As a matter of fact mbona tuition zipo nyingi tu za English na watoto wanaelewa
 
Nashukuru Mungu nilijitoa kwenye utumwa wa kujitakia na Sasa naishi kwa Amani kabisa watoto niliwatoa EM nimewaleta Kayumba sina Tena stress na mambo yanaenda vizuri na watoto wanafanya vizuri darasani. Twisheni ya nguvu. Aliyekuwa la 4 mwaka jana kapata A zote Masha'Allah.

Shoga zangu tuliokuwa tunasomesha wote EM karibu wote wamewarudisha Kayumba wanao wamebaki wachache ambao eti wanaogopa kuchekwa wataonekana wameshindwa maisha ila mateso Yao Sio ya dunia hii, mikopo kama yote, wananuka madeni na ndani hawana asset, hawana viwanja watoto wanalala chini ilimradi wasome EM..

Sasa najiuliza mateso yote hayo ya Nini wakati hata Kayumba wanaweza soma vizuri tu na Chuo wakafika kama.wanavyo fika wengine.

Poleni Sana watanzania wenzangu ambao bado mpo kwenye utumwa huo. Mungu awaongoze Sana mshituke mapema.

Sisemi kusomesha mtoto EM ni Vibaya ila Uwe na uwezo mkubwa Sana WA kifedha na assets za kutosha.
Ungewaambia ukweli kuliko kuleta uzi wa kuwasimanga huku
 
Sasa huko EM wanafundishwa Mtaala upi?

Unajua watu kuna mambo hamyaelewi kuhusu suala la Elimu. Mtoto afundishwe juu ya mti, kwenye ghorofa, au popote pale kama Mtaala ni uleule. Inatarajiwa wote watapata lilelile.

Kwenye Elimu kuna mambo yafuatayo:
1. Sera ya Elimu ya nchi
2. Malengo ya Elimu katika nchi
3. Malengo ya Elimu kwa kila Kozi au Somo
4. Mtaala
5. Muhtasari wa kila Masomo.

Kama Lengo ni kumpeleka mtoto EM ajue kingereza Walau cha kung'atia half cake Sawa. Ila kama unafikiri atapewa Elimu tofauti na Ile ya Kayumba basi unapoteza pesa yako.
100%=Fact.

Joannah
 
Sasa huko EM wanafundishwa Mtaala upi?

Unajua watu kuna mambo hamyaelewi kuhusu suala la Elimu. Mtoto afundishwe juu ya mti, kwenye ghorofa, au popote pale kama Mtaala ni uleule. Inatarajiwa wote watapata lilelile.

Kwenye Elimu kuna mambo yafuatayo:
1. Sera ya Elimu ya nchi
2. Malengo ya Elimu katika nchi
3. Malengo ya Elimu kwa kila Kozi au Somo
4. Mtaala
5. Muhtasari wa kila Masomo.

Kama Lengo ni kumpeleka mtoto EM ajue kingereza Walau cha kung'atia half cake Sawa. Ila kama unafikiri atapewa Elimu tofauti na Ile ya Kayumba basi unapoteza pesa yako.
100%=Fact.

Joannah
 
Umeona ee ndo utamu wa English medium upo hapo. Na vinakua na exposure fulani hivi amazing.

Watoto wa medium sura zimechangamka kuliko wa kwetu vidumu na mfagio stress kibao
Sahihi chukua mtoto wa darasa la saba kayumba waongee kiingereza na mtoto wa English medium darasa la pili

Kitoto cha English Medium kitamtoa knock out huyo darasa la saba wa kayumba
Vinaongea kingereza kilichonyooka na vinajiamini.
 
Back
Top Bottom