Watanzania wenye vipato vya chini wanao somesha English Mediums wanateseka hadi nawaonea huruma

Watanzania wenye vipato vya chini wanao somesha English Mediums wanateseka hadi nawaonea huruma

Labda kama wakimaliza wanaenda kujiajiri. Kazi ipo kwenye interview kampuni za wageni zenye mishahara minono!

Makampuni ya kigeni Mengi yanahitaji mtu anayeongea kingereza kizuri na kukiandika.
EM chache zinauwezo wa wa kumfanya mtoto awe mahiri wa kuzungumza na kuandika kingereza ila nyingi hazina uwezo huo.

Ukitaka ushahidi utapewa.
 
Siku hizi kuna kama kaugonjwa fulani kwa wazazi wa kileo,utasikia mzazi akisema mi mwanangu awezi kuteseka kama mimi,kamwe sitampeleka kayumba!,,mara sitaki atembee umbali fulani,,ooh nitafanya kila namna asiende kayumba nk nk,, watoto wanalelewa kimayai sana na wazazi wa sampli hii,ndo hao wanaingia gharama kubwa wasizoweza kuzimudu.
Kayumba kuna mambo mengi mno.
Watoto wanalawitiana kama balaa. EM kuna usalama mkubwa.
 
Kayumba mtoto hapelekwi hata dar es salaam zoo.

Baadhi ya EM wanaweza kufikia uwezo wa kwenda ufaransa.

Baadhi wanaishia kwenda serengeti

Baadhi wanaishia dar es salaam zoo.

Baadhi huishia daraja la Kigamboni
 
Miaka yote wanaoongoza kiwilaya,kimkoa,kitaifa somo la kiswahili ni English Medium unakuta wana A ya kingereza na A ya kiswahili

Kiswahili wakiweza vizuri na kingereza pia

Anayebisha awe anaangalia matokeo ya Necta yakitoka nani wanaongoza ufaulu wa kiswahiki.kwenye shule zilizoko eneo lako ni za serikali au za English medium? Asijipe pressure Apitie tu hata matokeo tu ya mwaka jana tu uone shule za eneo lako liwe la kata shule zipi wamefaulu sana somo la kiswahili?
Cha ajabu hata za vipaji zinapiywa na EM sasa sielewi hivi ni vipawa gani
 
Kayumba kuna mambo mengi mno.
Watoto wanalawitiana kama balaa. EM kuna usalama mkubwa.
Sasa ndo mateso hayo!!,na hata hivyo uko EM yapo pia,hizo ni tabia ziko kotekote tu, mhimu kuwepo usimamizi madhubuti toka kwa wazazi na walimu.
 
Nashukuru Mungu nilijitoa kwenye utumwa wa kujitakia na Sasa naishi kwa Amani kabisa watoto niliwatoa EM nimewaleta Kayumba sina Tena stress na mambo yanaenda vizuri na watoto wanafanya vizuri darasani. Twisheni ya nguvu. Aliyekuwa la 4 mwaka jana kapata A zote Masha'Allah.

Shoga zangu tuliokuwa tunasomesha wote EM karibu wote wamewarudisha Kayumba wanao wamebaki wachache ambao eti wanaogopa kuchekwa wataonekana wameshindwa maisha ila mateso Yao Sio ya dunia hii, mikopo kama yote, wananuka madeni na ndani hawana asset, hawana viwanja watoto wanalala chini ilimradi wasome EM..

Sasa najiuliza mateso yote hayo ya Nini wakati hata Kayumba wanaweza soma vizuri tu na Chuo wakafika kama.wanavyo fika wengine.

Poleni Sana watanzania wenzangu ambao bado mpo kwenye utumwa huo. Mungu awaongoze Sana mshituke mapema.

Sisemi kusomesha mtoto EM ni Vibaya ila Uwe na uwezo mkubwa Sana WA kifedha na assets za kutosha.
Hongera kwa kujitambuwa, maana katika hili wanawake ndio tatizo wanashinikiza wanaume watoto wakasome shule ghali kisa kingereza kumbe mtoto anaweza kusoma English course akajuwa kingereza vizuri tu.
 
Mtoto akishaelewa kiingereza na kuwa na ufahamu mkubwa,inakuwa rahisi kwenda skondari yeyote.Wazazi wengi wamegundua shida ni kiingereza,huna haja ya kumpeleka tena sekondari za kulipia ghali.
Ujinga huu, kwani serikali haina shule za English medium?

Si unalipia gharama nafuu tu? Mfano kwa Dar Olympio ni English medium ni ya serikali na zipo nyingine sikumbuki majina na baadhi ya mikoa zipo pia.
 
Kayumba mtoto hapelekwi hata dar es salaam zoo.

Baadhi ya EM wanaweza kufikia uwezo wa kwenda ufaransa.

Baadhi wanaishia kwenda serengeti

Baadhi wanaishia dar es salaam zoo.

Baadhi huishia daraja la Kigamboni
Mtoto wangu Anagradute form six mwaka huu, nje ya ada kuna mchango wa graduation mchanganuo wake unafika laki nane, kama siyo wizi na utapeli ni nini?

Epukeni hizi EM kama kipato ni cha kuungaunga hawa hawana huruma, halafu wengi wanaosonesha watoto hizo shule ni majizi tu ya pesa za umma wao wanatowa pesa yoyote.
 
Mtoto wangu Anagradute form six mwaka huu, nje ya ada kuna mchango wa graduation mchanganuo wake unafika laki nane, kama siyo wizi na utapeli ni nini?

Epukeni hizi EM kama kipato ni cha kuungaunga hawa hawana huruma, halafu wengi wanaosonesha watoto hizo shule ni majizi tu ya pesa za umma wao wanatowa pesa yoyote.
Nchi hii watu wanaishi wa hisia
 
Somesha EM kwa kutimiza majukumu yako na kulingana na kipato chako ila sio kwa malengo ya mtoto wako aje kuajiliwa hapo badae , kwani ukifanya kwa malengo ya kuajiliwa badae utakuja kupata stress na disappointed

Nimesoma kayumba na Nina maisha mazuri tu na wanangu pia watasoma kayumba huku nikiwaandalia maisha mengine baada ya kumaliza shule

Nina mfano hai, Kuna jamaa tumesoma nae huko mbeya mbalizi shule za kayumba pale mbalizi two miaka hiyo jamaa kwao wanauwezo wa kusomeshwa shule nzuri lkn tukaenda nae shule za kata pamoja , badae sisi wengine tukafaulu advance lkn yy alipata ufaulu wa kawaida baba yake alikuwa na uwezo lkn akampereka kijana akasomee diploma ya businesses administration, sisi tukaenda advance kwa sifa na hatimae chuo, lkn yule jamaa alipomaliza chuo diploma yake ya business administration alikuja kufunguliwa biashara na baba yake na anazisimamia vizur , sisi wengine tuliofaulu advance na wale wengine waliosoma English Medium ni watu wa kawaida na wengi hawana ajira

SoMo nililojifunza kwa yule mzee alianza kuwahusisha vijana wake kumiliki Mali na kuziendeleza na kuwaandalia zingine wakiwa bado wanasoma kayumba maana jioni walikuwa wanaenda kumsaidia kazi mzazi, na mzazi hakuwa na matarajio ya vijana wake waje waajiliwe.


Sasa ww somesha EM usiwe na matarajio ya kijana wako kuajiliwa hapo utakuwa umewini.
 
Mtoto wangu Anagradute form six mwaka huu, nje ya ada kuna mchango wa graduation mchanganuo wake unafika laki nane, kama siyo wizi na utapeli ni nini?

Epukeni hizi EM kama kipato ni cha kuungaunga hawa hawana huruma, halafu wengi wanaosonesha watoto hizo shule ni majizi tu ya pesa za umma wao wanatowa pesa yoyote.
Haki ya nani ni kweli wale jamaa huruma hawana,ni mabepari wa kufa mtu.Kama una kipato cha kuunga kama ulivyosema,ni bora usionje matatizo ya ubepari.
 
Hongera kwa kujitambuwa, maana katika hili wanawake ndio tatizo wanashinikiza wanaume watoto wakasome shule ghali kisa kingereza kumbe mtoto anaweza kusoma English course akajuwa kingereza vizuri tu.
Asante
 
Hoja ya kitoto kabisa kwahiyo mtoto kila anachotamani unampa😁😁😁nyie ndo mnatengeneza watoto wasio na uwezo mzuri wa kufikiri na wenye kufake maisha maana hata wazazi walifake maisha.


Muandae mtoto aweze kujitambua mapema acheni porojo na hoja mufilisi kama hizi.
Wewe ndio mmoja wa wale ambao nilisema hawataelewa. Uwe na tabia ya kurudia ulichosoma ili uelewe!! umefilisika uelewa 😛 😛 😛
 
Utotoni nilisoma kayumba, maendeleo yangu school yalikuwa mazuri, mtaani watoto wa huko nilikuwa nawakimbiza kwa kuwafanyia maswali yao, kuna binti wa olympio, jamaa yangu yupo dycc(yemen) pale ye la 7 mie la 6 lakini pepa zao namsaidia fresh tu, ila pepa zetu hagusi, labda sababu nilikuwa najua hisabati kama kipaji lakini siamini hivyo naona wao walikuwa wakifundishwa kawaida mnoo tofauti na sisi.

Lakini kayumba naona nilijifunza mengi kuanzia maisha, kuna watu wanakuja viatu vimetoboka, shati halieleweki, tisheti imechoka, nikajifunza maisha kwa namna nyingine, kuna jamaa yetu alikuwa anakaa na mama wa kambo, huyu mapumziko tulikuwa tunamchangia hrla ili nae aenjoy.
Ubabe na vitu vingine, nilijifunza vingi ambavyo naamini kule st. Nini nini nisingeyaona.

Ila tu kama mtoto kichwa mbovu jitahidi kumsimamia, tuition ya kutosha, vitabu(material) yote awe nayo hapo itasaidia, tofauti na hivyo atateseka maana kayumba darasa kuwa na wanafunzi 70 mpaka 100+ ni kawaida tu.
Hivyo itakupasa umkomalie mtoto.
Worse enough hizo shule za EM zinafundisha uzezeta yaani maisha laini as if huyo mtoto Kila hatua ambayo atakamilisha anakuta Kuna sehemu ameandaliwa.

So hata akija maliza Chuo anatakiwa apitilize kwenye kazi,swali hizo kazi ziko wapi? Maana hawezi skills zingine za maisha ya kawaida,hawajui kufagia,wanapikiwa,wakila wanalala,wanatafuniwa shuleni,wanaenda na kurudi Kwa magari nk so unakuta anakuwa kama kuku wa Kisasa anavyofugwa.

Hata Mimi nimehamisha sio Kwa sababu Sina hela ya kulipa Bali Kwa vile naona atakuwa mfugo na hayo maisha ya nyoronyoro Sina.
 
Unajua mtoto anauma eeeee. Just imagine katoto kako kananyanyasika mtaani hadi kanakonda kakiona vigari vya njano vinawabeba wenzake waende shule.. hata kama wewe una ka Vitz kako unampeleka hapo kayumba, lakini yeye bado atatamani school bus... mbaya zaidi vitoto vya hizo miedium vinacheza kwa kiinglish muda woteee.. ... katoto kako kanakodoa macho tu... hakana raha mtaani, hakana raha nyumbani, kanatamani kangezaliwa kwa jirani. Hapo ndipo utakuta Mzazi anaamua kujitosa... kama mbwai na iwe mbwai wote watasoma huko huko kwenye kingereza cha kucheza na wenzao. Labda muishauri serikali ya government yenu ibadilishe mitaala, iweke na skulibasi. KUNA WALIONIELEWA
Anatakiwa kushinda hii psychological torture Ili baadae awe mtu wa maana na asibabaishwe na chochote hapa Duniani.
 
Back
Top Bottom