Watanzania wenye vipato vya chini wanao somesha English Mediums wanateseka hadi nawaonea huruma

Labda kama wakimaliza wanaenda kujiajiri. Kazi ipo kwenye interview kampuni za wageni zenye mishahara minono!

Makampuni ya kigeni Mengi yanahitaji mtu anayeongea kingereza kizuri na kukiandika.
EM chache zinauwezo wa wa kumfanya mtoto awe mahiri wa kuzungumza na kuandika kingereza ila nyingi hazina uwezo huo.

Ukitaka ushahidi utapewa.
 
Kayumba kuna mambo mengi mno.
Watoto wanalawitiana kama balaa. EM kuna usalama mkubwa.
 
Kayumba mtoto hapelekwi hata dar es salaam zoo.

Baadhi ya EM wanaweza kufikia uwezo wa kwenda ufaransa.

Baadhi wanaishia kwenda serengeti

Baadhi wanaishia dar es salaam zoo.

Baadhi huishia daraja la Kigamboni
 
Cha ajabu hata za vipaji zinapiywa na EM sasa sielewi hivi ni vipawa gani
 
Kayumba kuna mambo mengi mno.
Watoto wanalawitiana kama balaa. EM kuna usalama mkubwa.
Sasa ndo mateso hayo!!,na hata hivyo uko EM yapo pia,hizo ni tabia ziko kotekote tu, mhimu kuwepo usimamizi madhubuti toka kwa wazazi na walimu.
 
Hongera kwa kujitambuwa, maana katika hili wanawake ndio tatizo wanashinikiza wanaume watoto wakasome shule ghali kisa kingereza kumbe mtoto anaweza kusoma English course akajuwa kingereza vizuri tu.
 
Mtoto akishaelewa kiingereza na kuwa na ufahamu mkubwa,inakuwa rahisi kwenda skondari yeyote.Wazazi wengi wamegundua shida ni kiingereza,huna haja ya kumpeleka tena sekondari za kulipia ghali.
Ujinga huu, kwani serikali haina shule za English medium?

Si unalipia gharama nafuu tu? Mfano kwa Dar Olympio ni English medium ni ya serikali na zipo nyingine sikumbuki majina na baadhi ya mikoa zipo pia.
 
Kayumba mtoto hapelekwi hata dar es salaam zoo.

Baadhi ya EM wanaweza kufikia uwezo wa kwenda ufaransa.

Baadhi wanaishia kwenda serengeti

Baadhi wanaishia dar es salaam zoo.

Baadhi huishia daraja la Kigamboni
Mtoto wangu Anagradute form six mwaka huu, nje ya ada kuna mchango wa graduation mchanganuo wake unafika laki nane, kama siyo wizi na utapeli ni nini?

Epukeni hizi EM kama kipato ni cha kuungaunga hawa hawana huruma, halafu wengi wanaosonesha watoto hizo shule ni majizi tu ya pesa za umma wao wanatowa pesa yoyote.
 
Nchi hii watu wanaishi wa hisia
 
Somesha EM kwa kutimiza majukumu yako na kulingana na kipato chako ila sio kwa malengo ya mtoto wako aje kuajiliwa hapo badae , kwani ukifanya kwa malengo ya kuajiliwa badae utakuja kupata stress na disappointed

Nimesoma kayumba na Nina maisha mazuri tu na wanangu pia watasoma kayumba huku nikiwaandalia maisha mengine baada ya kumaliza shule

Nina mfano hai, Kuna jamaa tumesoma nae huko mbeya mbalizi shule za kayumba pale mbalizi two miaka hiyo jamaa kwao wanauwezo wa kusomeshwa shule nzuri lkn tukaenda nae shule za kata pamoja , badae sisi wengine tukafaulu advance lkn yy alipata ufaulu wa kawaida baba yake alikuwa na uwezo lkn akampereka kijana akasomee diploma ya businesses administration, sisi tukaenda advance kwa sifa na hatimae chuo, lkn yule jamaa alipomaliza chuo diploma yake ya business administration alikuja kufunguliwa biashara na baba yake na anazisimamia vizur , sisi wengine tuliofaulu advance na wale wengine waliosoma English Medium ni watu wa kawaida na wengi hawana ajira

SoMo nililojifunza kwa yule mzee alianza kuwahusisha vijana wake kumiliki Mali na kuziendeleza na kuwaandalia zingine wakiwa bado wanasoma kayumba maana jioni walikuwa wanaenda kumsaidia kazi mzazi, na mzazi hakuwa na matarajio ya vijana wake waje waajiliwe.


Sasa ww somesha EM usiwe na matarajio ya kijana wako kuajiliwa hapo utakuwa umewini.
 
Haki ya nani ni kweli wale jamaa huruma hawana,ni mabepari wa kufa mtu.Kama una kipato cha kuunga kama ulivyosema,ni bora usionje matatizo ya ubepari.
 
Hongera kwa kujitambuwa, maana katika hili wanawake ndio tatizo wanashinikiza wanaume watoto wakasome shule ghali kisa kingereza kumbe mtoto anaweza kusoma English course akajuwa kingereza vizuri tu.
Asante
 
Wewe ndio mmoja wa wale ambao nilisema hawataelewa. Uwe na tabia ya kurudia ulichosoma ili uelewe!! umefilisika uelewa πŸ˜› πŸ˜› πŸ˜›
 
Worse enough hizo shule za EM zinafundisha uzezeta yaani maisha laini as if huyo mtoto Kila hatua ambayo atakamilisha anakuta Kuna sehemu ameandaliwa.

So hata akija maliza Chuo anatakiwa apitilize kwenye kazi,swali hizo kazi ziko wapi? Maana hawezi skills zingine za maisha ya kawaida,hawajui kufagia,wanapikiwa,wakila wanalala,wanatafuniwa shuleni,wanaenda na kurudi Kwa magari nk so unakuta anakuwa kama kuku wa Kisasa anavyofugwa.

Hata Mimi nimehamisha sio Kwa sababu Sina hela ya kulipa Bali Kwa vile naona atakuwa mfugo na hayo maisha ya nyoronyoro Sina.
 
Anatakiwa kushinda hii psychological torture Ili baadae awe mtu wa maana na asibabaishwe na chochote hapa Duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…