Watato wakiniona huwa wanacheka sana na kunizoea hata niwe mkali

Hawajakuvunjia miwani mkuu?

Mimi ni opposite. Watoto hawaivani na mimi kabisa na napenda iendelee hivyo.

Kutupa miwani vimetupa sana sema havijawahi vunja,
Kukojolewa, kucheuliwa, kupakwa mate na kuachiwa mzigo mkubwa (Ndani ya diaper) ndiyo sana yanii!
 
Dah we jamaa umenifurahisha. Et sura ya kidemu huna labda likatuni! Ila sishangai sana mm nikibeba watoto wadogo hata kama awe ametoka kulala anarudi yena kulala.

Kweli mkuu,
Unakuta katoto kana miezi mitatu kanakuangalia kweli usoni utadhani kanakujua, halafu kanatabasamu.
Huwa wananikata maini sana hawa watoto daaah.....!
 
Leo asubuhi nimekaa sehemu fulani hivi.
Kuna katoto fulani hivi kapo na mama yake,
Ghafla mama yake akataka kutoa mlangoni, kale kajamaa kakanifukuza eti "Sogea mama yangu ashuke"
Yaani kananisukuma hadi watu wamecheka, nimekaangalia tu hako kanatembea yani urefu sawa na jogoo halafu unanipiga mimi mkwara......
 
Yaani wewe mazingira unayokuwepo vitoto havikosekani....au mzee wa singo mamaz?
 
Yaani wewe mazingira unayokuwepo vitoto havikosekani....au mzee wa singo mamaz?

Hahahaha!
Hapana Mazeee haya maisha ya kuruka-ruka sinaga, (Just too old for that)
Nikiwa nyumbani mimi nina utaratibu wa kuwapeleka na kuwachukua watoto wangu shule karibia kila siku,
Siku za michezo na maeonyesho huwa naenda kama mzazi, hivyo kuonana na vitoto vidogo ni kawaida sana.
 
Hayo mambo hayana umri....technic yako inaweza kufanya kazi.🙂
 
Aaah come on RRONDO ,
Women are the least of my worries for now,
BTW JF is the last street on Earth that i would try hook up with someone.
Literary, the last street on Earth................
Who said you are trying to hook someone up?
 
hahaha
kuna dogo muuza maziwa mtaani yeye watoto hadi wa shule ya msingi wakimuona wanakimbia huku wanalia vibaya sana utadhani wameona nyoka au mzimu. sura ya yule dogo ndio kama haijakaa sawa kwa maono ya wale watoto.

utakuwa na sura ya pekee yenye mvuto kwa watoto.
 
Ungeeleza aina ya malezi yako utotoni yalikuaje na wewe ni mtu wa aina gani moyoni? Ingependeza zaidi
 
Unakuwa mdogo wake MIKE MOUSE alafu hujui..![emoji125][emoji125][emoji232][emoji213][emoji193]
 
Inawezekana ni mpole na mchangamfu kutoka moyoni ni mtu wa kuweza beba tatizo ata la jirani yako. Mtu asiyekwazika na kuchukia kirahisi rahisi, mtu mwenye huruma sana, mwenye kujali, mwenye uvumilivu wa moyo, mtu mwenye kutamani kumfanya mwingine afurahi.
Hayo yote yakiwa moyoni kweli basi mtoto mdogo anaweza kuyaona hayo kupitia sura yako na macho yako. Na hayo hayaji kibahati mbaya mara nyingi inategemea aina fulani ya maisha from utotoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…