Watawala, siku wateule wenu wakigeuziwa kibao kwenye kuchapana viboko hadharani, tutaomba mkae kimya kama mlivyochagua kukaa kimya sasa

Watawala, siku wateule wenu wakigeuziwa kibao kwenye kuchapana viboko hadharani, tutaomba mkae kimya kama mlivyochagua kukaa kimya sasa

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Hivi sasa tunaona baadhi ya viongozi wa kuteuliwa, wanachapa watu viboko hadharani huku vitendo hivyo vikirekodiwa na picha kusambazwa mitandaoni.

Binafsi naamini vitendo hivi vinajenga chuki na kuamsha hasira za wananchi na naaamini pia wako baadhi ya watu kwa sasa wameanza kupania ku-react vibaya endapo watakuja kufanyiwa udhalilishaji huu.

Hatujui watu wanapanga nini katika mioyo yao ila kuna wanaoweza ku-react wakati kitendo hicho kinaendelea na kuna wanaoweza kuja kulipiza baadae-kila mtu na akili yake.

Hivyo, ikitokea kiongozi kageuziwa kibao na kudhalilishwa mbele ya camera au siku yoyote baada ya tukio, tunaomba watawala na vyombo vya dola mkae kimya kama mlivyochagua kukaa kimya wakati wananchi wanadhalilishwa.

Endeleeni ila iko siku mtakutana na watu wanaoweza kufanya maamuzi magumu na ya kijasiri yanayoweza kumaliza kabisa hii tabia kwa kumtoa mfano mmoja wa weteule anaendekeza hii tabia ya kudhalilisha watu hadharani.
 
Nani awageuzie kibao wakati wao wanamiliki Bunduki? Acha tu wawageuze watanzania wote watoto wa chekechea kwa kuwachapa bakora hadharani. Tumekwishaaaa
 
We ngoja ipo siku utakuja kusikia mkuu wa wilaya katolewa jino
Nani awageuzie kibao wakati wao wanamiliki Bunduki? Acha tu wawageuze watanzania wote watoto wa chekechea kwa kuwachapa bakora hadharani. Tumekwishaaaa
 
Uongozi wa matumizi ya mabavu badala ya uongozi wa kutumia akili.
 
Magufuli is evil, ogopa sana mtu anajionyesha ni mcha Mungu, Yesu alitufundisha unyenyekevu na siyo ukatili dhidi binadamu wengine, atalipa siku moja kwa uonevu huu dhidi ya Watanzania.

Mahakama pekee ndiyo yenye haki ya kuhukumu kwenye ya Mungu na siyo viboko, ...
 
Ajabu ni kuwa tunategemea hao wanaochapa watu viboko kisha kurekodi ndiyo watuletee maendelo!
 
Magufuli is evil, ogopa sana mtu anajionyesha ni mcha Mungu, Yesu alitufundisha unyenyekevu na siyo ukatili dhidi binadamu wengine, atalipa siku moja kwa uonevu huu dhidi ya Watanzania.

Mahakama pekee ndiyo yenye haki ya kuhukumu kwenye ya Mungu na siyo viboko, ...
Ibambasi mwenzako kajitambua ipo siku na wewe utajifunza tu.
 
Magufuli is evil, ogopa sana mtu anajionyesha ni mcha Mungu, Yesu alitufundisha unyenyekevu na siyo ukatili dhidi binadamu wengine, atalipa siku moja kwa uonevu huu dhidi ya Watanzania.

Mahakama pekee ndiyo yenye haki ya kuhukumu kwenye ya Mungu na siyo viboko, ...
Kuna wajinga wanaamini madaraja,SGR, Stieglers, ndege na vitu vingine vya aina hiyo ni justification ya huu udhalilishaji.
 
Watu watekwe wapigwe risasi wauwawe Asiongee kitu sembuse viboko. Alivyo sema I wish I could be IGP watu hawakumuelewa. Alimaanisha IGP awapige kipigo Cha mbwa KOKO.
 
Back
Top Bottom