Watawala wamebariki hizi faini za kionevu zinazofanywa na TRA mabarabarani?

Dah mkuu Hawa tra Wanachofanya sasaivi mungu ndo anajua wako brbrn wanakamata ad bajaj wamekua kama trafk

Jana nimechkua boda boda town naingia mtaani Ile dogo wa boda boda anakunja t kuingia street road jamaa Hawa hapa wakaivamia kbsa kwa kuidandia Kama tuko vitani kwa vurugu na vitisho alaf wako wawili wakaiweka pemben,kwa vurugu na vitisho kama tuko Somalia vitani

Aise nilistuka sana namuliza dogo Hawa nan aisee maana nilifkiri majambazi maana inatisha kwa kweli akaniambia WENYE NCHI YAO Hawa wanatuvamia t skuiz wanakagua Hadi Nguo z ndan .na jamaa ananshusha kbsa tafuta usafiri mwngne.
tunapoelekea Kama nchi sio kuzuri kwa kweli tunawafanya hata vijana wadog wataftaji wa Mia Mia tatu wachukie nchi yao.
Ikifika mahali kijana mdogo anakuambia HAWA WENYE NCHI YAO means tunapoelekea sio pazuri.
Serikali ijitathmini sana tunapoelekea iko wapi TZ ya wanyonge iliyohubiriwa kwenye kampeni
 
Sijaelewa..hapo ulitaka tra wapindishe sheria ili kodi ya serikali ipotee au unalalamika nini?
Mapenzi yako yasipelekee ukosefu wa akili,naamini wewe si chizi ila mapenzi kwa utawala huu ndio yanaibadili akili yako.Na wengi tunajua ukimuona mtu kiherehere wa utawala huu utajua ni ama ananufaika na utawala huu ama kula kulala kwa shemeji,ila ukiwa muhangaikaji utawala huu vikwazo ni vingi sana kwa watafutaji.

Mifano ya watu kama nyinyi ni mingi tukianza na mwenezi wa chama bwana taratibu tangu umeambiwa tumboni pana jaa ameshageuka kasuku.

Chukua mfano rahisi wa sababu za vitambulisho vya wajasiriamali wadogo na sababu za watawala kuvianzisha,huyu dereva kama kweli alipaswa kuadhibiwa basi ilitakiwa walau hata awekwe kwenye kundi hilo kwakuwa huyu ni mlala hoi,kilichofanyika ni sawa na kumpiga faini chinga 3000,0000/= kwakua hana kitambulisho cha mjasiriliamali jambo ambalo sio sawa .Nasisitiza hapa palihitaji hekima sio sifa za kijinga.

Kuwa mtimilifu kwenye sheria usifikiri ni jambo rahisi na ndio maana nasema sio wewe tu,kama sheria zingekuwa zinafuatwa hata Magufuli asingekuwepo uraiani leo.Na ili ujue kufuata Sheria ni ngumu,maraisi wamejitengenezea vifungu kwenye katiba vya Kinga yakutoshitakiwa mahakamani,jaribu kutafakari hayo na sio unabwabwaja tu.
 
Hili swala lilianza muda mrefu tu. Madereva walichekelea wakijua litawaumiza matajiri tu!

Yaani wakasahau kabisa hata hivyo vimizigo wanavyobeba ni hisani tu kwa sababu gari yenyewe ubavuni imeandikwa "UNAUTHORISED CARGO IS STRICTLY PROHIBITED".

Labda nikuulize kitu mtoa mada,

-TRA watajuaje kama huo mzigo uliobeba ni wako na siyo wa mwenye gari?

-unachohitaji kifanyike ni kipi hasa, mwenye gari adaiwe risiti ya kielektroniki wakati huo huo dereva akibeba mzigo usio na risiti busara itumike?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu mtoa mada haujamuelewa kodi inayozungumziwa hapo sio kodi ya mazao ni kodi anayopaswa kulipa mwenye gari pale anapofanya biashara ya usafirishaji,maana yake mwenye nikwamba mzigo alitakiwa kuna na risiti inayonyesha kiasi alicholipa kwa kusafirishiwa parachich zake
 
Duh mbona kama sijaelewa hapa. Kwani wasafirishaji nao wanatakiwa kuwa na mashine ya efd? Vipi kwa wenye uber na kirikuu?
 
Huyo si kwamba ana mapenzi ya kweli kwa huu utawala bali amepata ulaji ndo unaomtia upofu.
 
Kwenye hiyo nukuu ya mzee wetu JK walijibuje mkuu???
 
Ni kweli, busara itumike, sheria ikiangaliwa strictly kila wakati, hata jiwe lingekua ndani muda huu
 
Sio kodi ya mazao, hujaelewa; ni risiti anayotoa mwenye gari kwa huduma ya usafirishaji anayoitoa, na huikabidhi kwa mteja huduma inapokamilika, yaani mzigo kufika
 
Sijaelewa..hapo ulitaka tra wapindishe sheria ili kodi ya serikali ipotee au unalalamika nini?
Kwahiyo, mi sielewi, ina maana huko kichwani kwako hakuna ubongo kabisa au neno busara ni gumu sana?
 
Kutoza kodi kindakindaki kunahitaji uchumi uwe umeshaendelea.

Kodi ni kama kumkamua ng'ombe maziwa.

Ili umkamue na upate maziwa vizuri bila kumuua ng'ombe, unahitaji kumlisha kwanza.

Ama sivyo utakamua maziwa mpaka upate damu na ng'ombe afe.

Tanzania kuna msisitizo wa kutoza kodi, wakati uchumi wenyewe dhooful-hal.

Tunaua uchumi. Kuanzia kwa makampuni makubwa, wafanyabiashara wa kati, mpaka wafanyabiashara wadogo.
 
Duh mbona kama sijaelewa hapa. Kwani wasafirishaji nao wanatakiwa kuwa na mashine ya efd? Vipi kwa wenye uber na kirikuu?
Ndio, wasafirishaji wa mizigo mikoani wanapaswa kuwa na EFD, vimzigo vya ndani ya mji wanalipia tu mapato annually, Uber wanakatwa kodi kupitia Tin ya kampuni ya uber ambayo wana ofisi hapa nchini
 
Mmeyataka wenyewe, chaguo lenu wenyewe...... Wacha muisome nambaaaa weee
 
SHIDA NI WATOTO WA MASIKINI AMBAO WANATAFUTA SIFA. HUKO JUU LAKINI NAWATANZANIA HAWASIKII KABSA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…