Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu dereva inawezekana alikamatwa Mikumi au nanenane pale morogoro. Ni wasumbufu sana pale, hata kama unazo documents zote.Nadhani mleta uzi ingekuwa vizuri pia kujua ni eneo lipi dereva huyu lilipomkutia ili wahusika pengine waone kama hao maofisa waliokuwepo hapo walifanya kazi kwa mujibu wa sheria au la ili sheria ifate mkondo wake. Mimi ndiyo maana sasa hivi hata biskuti nadai risiti yangu sitaki shida na mtu
Duh mbona kama sijaelewa hapa. Kwani wasafirishaji nao wanatakiwa kuwa na mashine ya efd? Vipi kwa wenye uber na kirikuu?
Wafanya biashara ya transport hasa malori kuna kitu wanaita chombeza, ni mizigo midogo isiyokua na athari yoyote kwenye uendeshaji ambayo mara nyingi wanaachiwa dereva na utingo kama bonasi zao. Sasa kitu hakimuumizi mwenye gari ila TRA wanaumia...Sijaelewa..hapo ulitaka tra wapindishe sheria ili kodi ya serikali ipotee au unalalamika nini?
Unapata usumbufu upi wakati documents zote unazo?Huyu dereva inawezekana alikamatwa Mikumi au nanenane pale morogoro. Ni wasumbufu sana pale, hata kama unazo documents zote.
Itakuwa wanarecover pesa za uchaguzi!!!!Dah mkuu Hawa tra Wanachofanya sasaivi mungu ndo anajua wako brbrn wanakamata ad bajaj wamekua kama trafk
Jana nimechkua boda boda town naingia mtaani Ile dogo wa boda boda anakunja t kuingia street road jamaa Hawa hapa wakaivamia kbsa kwa kuidandia Kama tuko vitani kwa vurugu na vitisho alaf wako wawili wakaiweka pemben,kwa vurugu na vitisho kama tuko Somalia vitani
Aise nilistuka sana namuliza dogo Hawa nan aisee maana nilifkiri majambazi maana inatisha kwa kweli akaniambia WENYE NCHI YAO Hawa wanatuvamia t skuiz wanakagua Hadi Nguo z ndan .na jamaa ananshusha kbsa tafuta usafiri mwngne.
tunapoelekea Kama nchi sio kuzuri kwa kweli tunawafanya hata vijana wadog wataftaji wa Mia Mia tatu wachukie nchi yao.
Ikifika mahali kijana mdogo anakuambia HAWA WENYE NCHI YAO means tunapoelekea sio pazuri.
Serikali ijitathmini sana tunapoelekea iko wapi TZ ya wanyonge iliyohubiriwa kwenye kampeni
Nilikuuliza vile nikidhani wewe ni msafirishaji mkuu!TIN yangu inasoma kinondoni maana ndio location yangu ya biashara. Mzigo nautoa iringa kuja dsm, wakawa wanakamata mizigo morogoro kuwa hawana imani kama mizigo yote naitolea risiti, ingawa kwenye system wanaiona mashine yangu.
Nikaamua kuibeba mashine niwe natoa risiti mwanzo wa safari ili wakifika morogoro kusiwe na usumbufu ila bado nikaambiwa kwanini TIN isome kinondoni na risiti itoke iringa?
Wakaandika fine nami nikagoma kulipa.
Kwa scenario hiyo hapo juu unadhani kosa langu ni lipi? (Kama lipo).
Nilikuuliza vile nikidhani wewe ni msafirishaji mkuu!
Kwa jinsi nilivyokuelewa, TRA wa dar ndiyo walitakiwa kuhakikisha unatoa risiti kwa wateja wako na siyo wa hapo morogoro maana mzigo haujafika sokoni.
Ulitakiwa uwakomalie kuwa risiti utatoa dar baada ya mzigo kununuliwa bahati mbaya ukakubali kuyumbishwa ukaenda kutolea risiti iringa..
Hata ukiwauzia mzigo iringa, wateja wako ndiyo wanaotakiwa kuulizwa ziko wapi risiti walizopewa baada ya kufanya manunuzi
Sent using Jamii Forums mobile app