Watawala wamebariki hizi faini za kionevu zinazofanywa na TRA mabarabarani?

Hujawahi safiri njia ya Dar Dodoma, sir tunaowahi kazi Jumatatu Dodoma tunawachangia sana za "kiwi" yangeyange wa barabarani utadhani ni sheria!

Mazafantazao!
 
Huyu dereva inawezekana alikamatwa Mikumi au nanenane pale morogoro. Ni wasumbufu sana pale, hata kama unazo documents zote.
 
Gari zote za biashara zinatakiwa kuwa na mashine ya kutoa risiti mkuu. Kila muamala unaofanyika kati ya mwenye gari na mwenye mzigo, ni lazima uwe na risiti yake.
Duh mbona kama sijaelewa hapa. Kwani wasafirishaji nao wanatakiwa kuwa na mashine ya efd? Vipi kwa wenye uber na kirikuu?
 
Sijaelewa..hapo ulitaka tra wapindishe sheria ili kodi ya serikali ipotee au unalalamika nini?
Wafanya biashara ya transport hasa malori kuna kitu wanaita chombeza, ni mizigo midogo isiyokua na athari yoyote kwenye uendeshaji ambayo mara nyingi wanaachiwa dereva na utingo kama bonasi zao. Sasa kitu hakimuumizi mwenye gari ila TRA wanaumia...
 
TIN yangu inasoma kinondoni maana ndio location yangu ya biashara. Mzigo nautoa iringa kuja dsm, wakawa wanakamata mizigo morogoro kuwa hawana imani kama mizigo yote naitolea risiti, ingawa kwenye system wanaiona mashine yangu.
Nikaamua kuibeba mashine niwe natoa risiti mwanzo wa safari ili wakifika morogoro kusiwe na usumbufu ila bado nikaambiwa kwanini TIN isome kinondoni na risiti itoke iringa?
Wakaandika fine nami nikagoma kulipa.
Kwa scenario hiyo hapo juu unadhani kosa langu ni lipi? (Kama lipo).
Unapata usumbufu upi wakati documents zote unazo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Itakuwa wanarecover pesa za uchaguzi!!!!
Lazima pesa ikusanywe miradi mikubwa itekelezwe "hakuna namna".
 
Mimi Binafsi siwezi kuwa na maneno mengi zaidi ya kusema "MITANO TEEENA"[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Nilikuuliza vile nikidhani wewe ni msafirishaji mkuu!

Kwa jinsi nilivyokuelewa, TRA wa dar ndiyo walitakiwa kuhakikisha unatoa risiti kwa wateja wako na siyo wa hapo morogoro maana mzigo haujafika sokoni.

Ulitakiwa uwakomalie kuwa risiti utatoa dar baada ya mzigo kununuliwa bahati mbaya ukakubali kuyumbishwa ukaenda kutolea risiti iringa..

Hata ukiwauzia mzigo iringa, wateja wako ndiyo wanaotakiwa kuulizwa ziko wapi risiti walizopewa baada ya kufanya manunuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mkuu, walizuia gari pale nanenane kwa siku 4 nikahofia mzigo kuharibika. Ila nahisi kuna force kutoka kwa wakubwa ya kulazimishwa kwa namna yoyote ile, makusanyo yaongezeke.
Maana mie walianza kunilazimisha kuwa nifungue ofisi (branch) Iringa, nikawagomea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…