GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Daniel Arap Moi "alijiapiza" kuwa KANU ingetawala Kenya miaka mia moja! Iko wapi kwa sasa? Haikufikisha hata miaka hamsini. Iliondolewa madarakani na waliowahi kuwa wana KANU waandamizi.
Adolf Hitler alikuwa na nia ya kuwaangamiza Wayahudi wote. Japo aliwaua wengi lakini lengo lake halikutimia. Badala yake, alikufa akawaacha Wayahudi wakiendelea "kustawi"
Kanali Ghadafi aliwapatia raia wake karibia kila kitu isipokuwa "uhuru". Kosa hilo lilimgharimu maisha na kuiharibu nchi yake "nzuri"
Rais wa Syria alijitahidi kuwanyamazisha raia wake waliotaka mabdaliko, lakini baada ya miaka mingi ya mtifuano nchini kwake, kaishia kuikimbia nchi yake. Angesoma alama za nyakati asingepatwa na hayo madhila!
Iliyokuwa nchi kubwa barani Afrika, Sudan, iliishia kugawanyika na kuwa nchi mbili, Sudan na
Sudan Kusini, kutokana na ubaguzi wa kiitikadi. Na kwa kuwa "dhambi" ya ubaguzi ni mbaya sana, amani haikudumu nchini Sudan hata baada ya Sudan Kusini kujitenga. Inafahamika kilichofuatia mpaka kumfurusha madarakani Rais Omar El Bashir.
Kama watawala wangejifunza kuwapatia wenye nchi wanachokihitaji hata kabla hawajakiulizia, wangeweza kutawala kwa utulivu na kujistaafia zao kwa amani!
Mungu ibariki Tanganyika!
Mchana Mwema!