Napenda kuwaasa watawala wetu kuwa, kuanzia sasa waanze kusoma alama za nyakati. Mwaka 2025 tunarajia kufanya uchaguzi Mkuu. Viongozi wetu waongoke, wasirudie tena yaliyopita katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019, uchaguzi Mkuu 2020 na uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.
Kinachoendelea Msumbiji ni watu kufika nukta ya mwisho ya uvumilivu. Hatua hiyo ikifika, huwa hakuna mtu tena anayeogopa risasi, mabomu au silaha nyingine yoyote ile. Wakati huo, kufa au kutokufa huwa vina thamani sawa.
Mwenye masikio na asikie.