The logic is simple! Nguvu ya madaraka ipo kwa hao watekaji. Ni lazima wakumbatiwe maana ndiyo wanamsaidia kujenga empire yake. Raia wengi hawapo nae, kilichobaki ni kutumia nguvu. Kinachofanyika ni kujaza hofu. Kunyamazishwa ili yoyote atakaye doubt anakuwa targeted. Tupo gizani.
Nakubaliana na wewe.
Lakini nguvu ya madaraka anayo Rais, ambaye ndiye anayapitishia madaraka hayo kwa hao watekaji; kwa maana halisi ni kuwa watekaji wana ruhusa ya mwenye madaraka, na si kinyume chake.
Nakubaliana nawe pia kwamba njia pekee iliyo baki kwa Samia kuendelea kuwa kwenye madaraka ni kuwatumia hawa; kwa kutia hofu watu, na kwa vyombo vingine vya dola pamoja na wateule wake mbalimbali, kama waliopo kwenye tume ya uchaguzi, mahakamani, na kwingineko.
Hana tena yale matumaini ya kutumia hadaa kama zile 4Rs na wasanii kumvusha hata kwa kutumia kura za bandia.
Hizi mbinu zilianza kitambo, na ile sheria ya Usalama kupitishwa na kusainiwa haraka. Hapakuwa nahapajawahi kuwepo na maelezo kwa nini sheria hiyo ililazimu kuwepo wakati huu. Hiyo sheria matokeo yake ndiyo haya ya watu kutekwa na kupotezwa hovyo hovyo.
Uchaguzi wa srikali za mitaa, nao ukafanywa uwe wa kuandaa kwa jukumu lile lile la kumrudisha madarakani kwa nguvu Samia hapo 2025. Ndiyo sababu Wizara ya Tamisemi ikaamua ndiyo isimamie uchaguzi huo.
Kwa hiyo haya yote yame pangwa toka mwanzo, kama mkakati wa kumweka madarakani Samia kwa mabavu
Sasa swali ni, je, waTanzania baada ya kufahamu haya wapo tayari kuruhusu kiongozi anaye wekwa madarakani kwa nguvu?
Lakini, pengine kabla hata ya kujibu hilo swali la wananchi; ni muhimu kuwauliza CCM wenyewe: je, CCM wapo tayari kuvuruga amani ya nchi hii? Huko ndani ya CCM hawawezi kulimaliza hili swala kabla ya kulifikisha kwa wananchi wenyewe? Je, CCM ipo tayari kubeba huu mzigo Samia anao kitwisha chama hicho?