Watendaji wa Mange Kimambi App wapandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mkurugenzi wa Mtandao wa Kijamii wa U turn Collection, Allen Mhina (31) na wenzake wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashtaka matatu yakiwemo ya kuchapisha maudhui yanayokiuka haki na uhuru wa mtu mwingine na kumfedhesha mtu kwa njia ya mtandao (cyber Bullying).

Mbali na Mhina, ambaye ni mkazi wa Temeke, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya jinai namba 57/2022 ni Mtandao wa U turn Collection na Mange Kimambi App.

Mhina na wenzake wamesomewa mashtaka yao, Ijumaa ya wiki iliyopita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na mawakili wa Serikali Waandamizi, Slyvia Mitanto akishirikiana na Mwanaamina Kombakono.

Wakiwasomea hati ya mashtaka, katika shtaka la kwanza, ambalo ni kuchapisha maudhui yanayokiuka haki na uhuru wa mtu mwingine, linalowakabili washtakiwa wote, wakili Mitanto na Kombakono wamedai kuwa, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Machi 9, 2022 katika maeneo tofauti ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Siku hiyo ya tukio, washtakiwa wanadaiwa walichapisha video ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Kitengo cha wagonjwa Mahututi (ICU) maudhui ambayo yanadhuru haki ya faragha ya mgonjwa.

Shitaka la pili, ni kufanya kazi ya uandishi wa habari bila ya kuwa na kibali kutoka bodi ya ithibati ya wanahabari, shtaka linalomkabili Mhina na U turn Collection.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo, kati ya Septemba 22, 2021 na Machi 14, 2022 Kinondoni eneo la Manyanya, ambapo siku hizo washtakiwa hao wanadaiwa walifanya kazi ya uandishi wa habari bila ya kuwa na kibali kutoka bodi ya ithibati ya wanahabari.

Shtaka la tatu ni kumfedhesha mtu kwa njia ya mtandao (cyber Bullying), shtaka linalomkabili Mhina peke yake, analodaiwa kulitenda Machi 9, 2022 katika maeneo tofauti ndani ya nje ya nchi ya Tanzania.

Mshtakiwa Allen kupitia mfumo wa kompyuta unaojulikana kama Mange Kimambi APP unaosimamiwa na U turn Colection anadaiwa kuchapisha video ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha wagonjwa Mahututi (ICU) kwa nia ya kusababisha dhiki ya kihisia (emotional distress)

Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yake, alikana kutenda makosa hayo.

Upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea hoja za awali( PH) mshtakiwa.

Hakimu Kabate alitoa masharti ya dhamana ambayo mshtakiwa huyo alitakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini dhamana ya Sh100,000.

Hakimu Kabate aliahirisha kesi hiyo hadi April 27, 2022 itakapoitwa kwa ajili ya PH. Hata hivyo mshtakiwa yupo nje kwa dhamana.

Source: Mwananchi
 
Fungia iyo takataka
 
Zigo lake hilo yeye Mhina ndie mkurugenzi wa hiyo U turn sio Mange Kimambi analo hilo zigo huyo Mhina
 
Serikali ingeweka nguvu kuboresha hali ya maisha ya watanzania inayozidi kuwa ngumu kila kukicha
 
Nadhani hii biashara ya app imemshinda arudi kuuza kyu maa tu kwa wazungu
 
Wapare Mshana Jr walivyo wachawi na wepesi kuhonga hiyo kesi itapeperushwa tu
Mange analelewa na Samia. Walikuwa wanamtumia kuvujisha siri wakati wa Mwendazake na sasa wanalipa fadhila kwa kumwachia afanye anavyotaka. Unadhani ungekuwa uongozi thabiti angeweza kupokea malipo kwa kutumia financial organs za Bongo?
 
Hii Wazungu wanaita "beating in the bush": TCRA wangeipiga block hiyo Mange Kimambi App kwenye Google Playstore na kwenye Apple App Store.
 
Wamlipe Profesa hapo ndo adabu itarudi kwa wanao weka Mambo ya watu hadharani
 
Mange analelewa na Samia. Walikuwa wanamtumia kuvujisha siri wakati wa Mwendazake na sasa wanalipa fadhila kwa kumwachia afanye anavyotaka. Unadhani ungekuwa uongozi thabiti angeweza kupokea malipo kwa kutumia financial organs za Bongo?
Muunge na yule madame aliyeenda Mbinguni hapo majuzi
 
Imagine mwanaume mzima unajitambulisha kwa watu eti wewe ni mfanyakazi wa Mange kimambi😃 hii haina tofauti na jamaa mmoja pale Buguruni ana bonge la mwili,bonge la baunsa halafu eti anauza sambusa tena za viazi
 
Back
Top Bottom