Watendaji wa serikali wakamatwa kwa wizi wa dawa

Watendaji wa serikali wakamatwa kwa wizi wa dawa

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Watu 12 wakiwamo Watendaji wa Serikali za Mtaa, wamekamatwa wakidaiwa kuiba chupa 434 za dawa za kuua wadudu wa pamba, zilizotolewa na Serikali kwa wakulima wa zao hilo katika Kata ya Nyakabindi, Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.


Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Wilaya ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Bariadi, Lupakisa Ndurea ameeleza kuwa dawa zilitakiwa ziwe 1580 lakini baada ya uchunguzi wakakuta dawa 197 hazipo.

“Wameiba dawa, tumewakamata na ninataka niwaambie watarudisha dawa zetu na tutawafikisha mahakamani.

“Chupa hizo zilizoibiwa hizo ni sehemu ya chupa 300,000 zilizotolewa na Bodi ya Pamba (TCB) kwa wakulima wilayani Bariadi,” alisema Lupakisa Ndurea.

Mmoja wa washtakiwa amesema alipigiwa simu na Mtendaji wa Mtaa ambaye ndiye aliyempa mchongo wa kuziiba dawa hizo.


Source: EastAfricaRadio
 
Kazi iendelee

Watendaji wameupiga mwingi
 
Si wanadanganyana upigaji umerudi sasa piga yakukute
 
Back
Top Bottom