Watendaji wa Serikali wenye mamlaka zioneeni huruma kodi za watanzania

mangiTz

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2019
Posts
1,820
Reaction score
3,062
Salaam wana JF

Weekend imeendaje kwenu

Moja ya vitu vinasikitisha katika mamlaka na baadhi ya watendaji wasio waaminifu ni kufuja mali za umma na wizi uliokithiri

Hii huenda imeshuhudiwa na wengi zaidi na vingine vikionekana tu viashiria lakini hakuna jibu la moja kwa moja kubwa kuna wizi. Ndio ni katika halmashauri zetu upigaji umekuwa ni mwingi na umeshazoeleka ni kitu cha kawaida kwa baadhi ya watumishi wasio waaminifu.

Hii hali ni mbaya na inawapa moyo ama ujasiri wa walipa kodi kuona haina haja ya kulipa kodi bali uhalali ni kuikwepa kodi kwasababu, mfano mdogo achana na wanaojiweza chukua mfano mama anayeuza matunda akizunguka huku na kule kutafuta riziki jioni anamtumia mwanae yuko shule inabidi alipe tozo, ile tozo inaumiza kwa mtu asiye na kipato cha kueleweka ,halafu kesho anasikia wangu wameiba 100M na wakasimamishwa kazi au kuhamishwa. Huyu siku nyingine atalipa kwa hiari?

Hii inafanya watu wanaolipa wanalipa kodi tu kwa vile hamna namna ya kukwepa mfano tozo n.k zile ambazo zimeunganishwa na huduma/bidhaa moja kwa moja.

Hii haikubaliki watendaji baadhi wakajimilikisha kusiko stahili. Hii kuna siku watu wataingia barabarani ni vile tu Tanzania hatujazoea mambo ya fujo.

Angali ujenzi wa jengo la serikali kama hili na bado linajengwa sio gofu wala sio la siku nyingi ni jipya imagine cement iliyoweka na mchanga uliotumika.

Your browser is not able to display this video.
 
Ni sawa mtu unapewa m 20 ujenge darasa
 
Yaan nikiona yale magari ya waheshimiwa ya mamilioni ya pesa, nazidi kuwaonea huruma watanzania wenzangu
 
Hii ndio picha halisi ya Utendaji wetu watu weusi;
Hapo kuna
1.utangazaji tenda, na wazabuni wakashindanishwa na mmoja bora zaidi kuliko wote akashinda hiyo tenda.
2.Kazi ikaanza, na kuna kamati ya ujenzi inafutailia na kukagua, kuna injinia wa mkoa, Wilaya, wote wapo na wanakagua kazi.
3. Kuna mjenzi/mkandarasi ana team ya watendaji wako saiti na wanafanya kazi kwa weledi kabisa, kazi nzuri ndio hiyo.

SHERIA ZA UTUMISHI WA UMMA, ZINATAKIWA ZIBADIRIKE.
WATU WAPEWE AJIRA KUTEGEMEANA NA UTENDAJI WAO.
 
Asee nikisoma procedures hizi zote ulizoandika nabaki kusema acha nipambanie familia yangu , lakini nawaza si ni nchi yangu🤔
 
Tuunge mkono Band Wagon ya kataa Uhuru. Tumepata Uhuru mwaka 1961 leo mwaka 2024 eti tunakwenda kujifunza kwa wale tuliopata nao Uhuru mwaka 1961! Yaani kila siku unakwenda kujifunza kwa wale uliokuwa nao darasa moja! Huu ni utapeli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…