kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Polisi nchini China na Afrika Kusini wamekamata maelfu ya dozi bandia za chanjo ya Covid-19 na kuwakamata wahusika, Polisi wa kimataifa, Interpol wameeleza.
Polisi wamewakamata watu 80 kwenye kiwanda nchini China kwa madai ya kutengeneza chanjo bandia , ambapo dozi 3,000 zilibainika tayari zikiwa zimetengenezwa katika kiwanda hicho.
Raia watatu wa China na mmoja wa Zambia walikamatwa katika ghala huko Gauteng, Afrika Kusini, ambapo chupa zilizokuwa na dozi 2,400 ziligundulika. BBC
Nadhani tusikimbilie kuchanjwa, wacha tuone kwanza sinema itavyokuwa