Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Dkt. Bryson Mcharo, Daktari bingwa wa mifupa kwa watoto- MOI
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na ubongo Muhimbili (MOI) imehitimisha kambi maalum ya upasuaji wa kurekebisha kibiongo ambapo watoto 13 wamefanyiwa upasuaji huo kwa mafanikio makubwa.
Kaimu Mkurugenziu Mtendaji wa MOI, Dkt. Laurent Lemeri Mchome amesema Februari 28, 2025 kuwa kukamilika kwa kambi hiyo kunafungua milango kwa watoto wenye ulemavu wa kibiongo kupata matibabu ya kibingwa na viungo vyao kurejea katika hali yau kawaida.
“Mafanikio ya kambi hii ni matokeo ya juhudi za Serikali ya awamu ya Sita ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wau Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha taasisi ya MOI kuwa na vifaa tiba vya kisasa ambavyo vinarahisisha kufanya upasuaji wa kibingwa na kibobezi wa Mifupa, mgongo , ubongo na mishipa ya fahamu pamoja na kusomesha wataalam” amesema Dkt. Lemeri.
Mratibu wa kambi hiyo Dkt. Bryson Mcharo amesema kuwa watoto 13 wamefanyiwa upasuaji huo wa kurekebisha kibiongo katika kambi hiyo maalumu kwa ushirikiano wa vyuo vikuu vya Ramallah cha nchini Palestine na Toledo- Ohio chau nchini Marekani.
"Mpaka sasa hivi tumefanyia upasuajiu watoto 13 tangu Jumatatu (Februari 24, 2025), watoto waliokuwa na umri chini ya miaka 10 walikuwa wanne, kuna mmoja alifanyiwa upasuaji wa kitaalam zaidi, wanawakewa vyuma vya ndani lakiniU vinaruhusu kuongezeka urefu wako" amesema Dkt. Mcharo
Kwa upande wake, Mkufunzi wa kambi hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Ramallah cha nchini Palestine na Chuo Kikuu cha Toledo- Ohio_ Marekani, Prof. Alaaeldin Azmi Ahmad amesema kuwa wataendelea kushirikiana na MOI ili kuwajengea uwezo wataalam hao na kuifanya taasisi hiyo kuwa Kituo cha umahiri cha mafunzo ya upasuaji wa kurekebisha kibiongo barani Afrika.