Hebu muwe mnasoma na kufuatilia taarifa jamani...Nina uvivu kidogo wa ku-google wizara zipi zinahusika kwenye hili sakata la mchele. Bashe Waziri wa Kilimo ameliongela lakini anasema ishu ni ya NGO (NGO ziko chini ya wizara gani vile?) zinazohusisha mashule (wizara ya Elimu). Swali langu ni jepesi tu: Watakaopewa huo mchele wenye rutuba ni Watoto wote mpaka Wazenji au ni kwa watoto wa Bara tu?
Hivyo vyakula wapelekewe Palestina!Tanzania tuna aridhi inayolimika zaidi ya hekta 44,000,000 na hekta 29,000,000 zinazofaa kilimo cha uwagiliaji.
Pia tunapata mvua ya zaidi ya milimita 3,000 ambazo zikitumiwa vizuri tunaweza kulima kwa mwaka mzima.
Hapa chini ni chakula misaada ambacho tumepokea kutoka marekani.
Chini ya mpango wa 'Pamoja Tuwalishe', Wizara ya Kilimo ya Marekani, kwa ushirikiano na Jumuiya za Kimataifa, imetoa msaada wa kwanza wa mchele ulioongezwa virutubisho, maharage na mafuta ya alizeti kutoka kwa wakulima wa Marekani moja kwa moja hadi shuleni katika eneo la Dodoma nchini Tanzania.
Zaidi ya kutoa milo yenye lishe, wanafunzi katika shule zaidi ya 300 zinazoshiriki, pia wataanzisha bustani za shule, na kujifunza mbinu za kuvuna maji ya mvua.
Ikiwa ni mfano kamili unaoweza kuigwa, programu hii inaakisi ahadi na dhamira ya dhati ya Marekani ya kukuza afya, elimu, na fursa kwa watoto kote ulimwenguni.
My Point: Chakula hiki cha msaada kimewekewa virutubisho na wanaenda kula watoto wetu katika shule zaidi ya 300, nafadhaika sana.
Yapo All over Germany mpaka najiuliza viongozi wetu wanafanya nini ?Unasema hapo ulipo kuna matangazo ya uhaba wa njaa huku afrika?.
Wewe kila unachoandikiwa unakiamini? Pole yakoSoma hii makala... View attachment 2937571
Kuna mashirika ulaya wanatumia hiyo njia kujinufaisha sababu baadhi ya wazungu hawajui afrika na wanaambiwa huko ni eneo la jangwa wanaishi watu weusi ambao hata kulima hawajui.Yapo All over Germany mpaka najiuliza viongozi wetu wanafanya nini ?
Yaani hizo picha zipo nyingi nitazipiga siku nikiwa free na nitazipost huku na wanapewa hela kibao.Kuna mashirika ulaya wanatumia hiyo njia kujinufaisha sababu baadhi ya wazungu hawajui afrika na wanaambiwa huko ni eneo la jangwa wanaishi watu weusi ambao hata kulima hawajui.
Na wanaonyeshwa picha za maeneo hatarishi ambayo kamwe hayapo.