Soma statement yangu vizuri. Ulichoandika ndio nimesema kuwa ndio wakati wa kupokea msaada.
Wewe kwa umri wako mtu anakupa msaada wa nini! Mimi mtu kunipa msaada ni kushusha utu wangu labda kama kuna ukame au janga lingine. Zawadi naweza kupokea lakini na mimi nirudishe zawadi.
Nimekumbuka when growing up kuna jirani walikuwa wanaleta zawadi na kikapu baada ya kupokea tulikuwa hairuhusiwi kurudisha kikapu kikiwa tupu. Unafikiri ni kwa sababu gani? Likewise kwetu tulikuwa tukipeleka kitu kwa mtu lazima akirudishe na kitu.
Labda kama ni sadaka tumepeleka kwa Mzee asiyejiweza, lakini hata yeye alikuwa anatafuta chochote cha kukupa.
Sasa hiki kizazi cha leo mnapenda tu kupokea, ni tatizo. Ndio maana hatubarikiwi. Wewe unafikiri kwa nini Amerika anakupa msaada? Jiulize kabla hujapokea. Kuna baraka zinapatikana kwa kutoa na yule anayepokea anapoteza. Sorry I didn't mean to be religious