Watoto watano wamepoteza maisha kwa tukio la moto lililotokea katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Igambilo, kilichopo Kata ya Misha, Manispaa ya Tabora, usiku wa kuamkia siku ya Jumanne.
Watoto hao walikuwa ndani ya bweni lao la kulala wakati moto ulipozuka na kuliteketeza kabisa, huku ikiripotiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni hitilafu ya umeme
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mohamed Jihad, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi wa awali umeonesha kuwa moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme iliyotokea kwenye nyaya za umeme ndani ya bweni hilo.
Baadhi ya watoto walionusurika katika tukio hilo wamesimulia namna walivyoshituka kutoka usingizini baada ya kuona taa ikiwaka na kuzima ghafla, kisha cheche za moto zikaanza kurukia kwenye magodoro. Wanasema walijaribu kuzima moto huo kwa juhudi zao, lakini haukuweza kudhibitika mapema, na hivyo kusababisha madhara hayo makubwa
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paulo Chacha, ametoa pole kwa familia na wale wote walioguswa na tukio hilo, akibainisha kuwa serikali ya mkoa tayari imeanza kuchukua hatua za dharura kusaidia kituo hicho
Serikali ya mkoa pia imesema itahakikisha uchunguzi kamili unafanyika na hatua za usalama zinaboreshwa katika vituo vya malezi ya watoto ili kuzuia matukio kama haya kujirudia
Chanzo: Jambo TV