Watoto kuwahi shule alfajiri: je, ni mafanikio ya kielimu AU tishio kwa afya?

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
WATOTO KUWAHI SHULE ALFAJIRI: JE, NI MAFANIKIO YA KIELIMU AU TISHIO KWA AFYA?

Na Dickson Kapungu Kutoka Songwe.

Watoto kuwahi shule alfajiri imekuwa sehemu ya maisha ya kila siku kwa wanafunzi, Wengine huamka mapema sana ili kujiandaa, kutembea umbali mrefu na kutumia usafiri wa umma kuwahi masomo.

Wazazi na walimu wanaona kuwahi shule kuwa sehemu ya kujenga nidhamu, uwajibikaji na matumizi mazuri ya muda, lakini suala hili linaibua mjadala kuhusu iwapo ratiba hizo zinaendana na mahitaji ya mtoto kiafya.

Baadhi ya wanafunzi mkoani Songwe wanadai kuna wakati wanashindwa kuzingatia masomo darasani kwasababu ya uchovu unaotokana na usingizi wanao katisha kwa kuamka saa kumi na moja alfaji huku wakichelewa kulala kutokana na kukaa muda mrefu shuleni.

Marry Ayubu Kinyamagoha ni mwanafunzi wa Darasa la sita katika Shule ya msingi Tunduma anaeleza kuwa ratiba inamlazimisha kulala saa nne usiku kutokana na kuchelewa kurudi shule ambapo anatoka saa 12 jioni na akifika nyumbani husaidia wazazi kuandaa chakula cha jioni had saa 4 na kulazimika kuamka saa 11 ambapo hulala kwa masaa 7 hadi 8.

LABAN ZAKARIA mwanafunzi wa Shule ya msingo Tunduma anaeleza kuwa kuamka mapema baada ya kulala usiku kunaweza kumfanya ahisi usingizi wakati wa masomo na hivyo kushindwa kufuatilia vizuri kile kinachofundishwa huku akieleza changamoto za kukimbizwa na Mbwa ambao wanakuwa bado hawajafungiwa nyakati za asubuhi.

Kwa mujibu wa Centers for Disease Control and Prevention (CDC), watoto wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanahitaji takribani saa 9 hadi 12 za usingizi kwa siku, huku vijana wenye miaka 13 hadi 18 wakihitaji saa 8 hadi 10.

Utafiti wa mwaka 2026 uliochapishwa katika jarida la Sleep Medicine umeonyesha kuwa shule katika maeneo mbalimbali huanza masomo mapema, hali ambayo imehusishwa na changamoto ya wanafunzi, hasa vijana, kutopata usingizi wa kutosha. Utafiti huo unaongeza mjadala kuhusu umuhimu wa kuangalia muda wa kuanza shule sambamba na mahitaji ya usingizi ya watoto na vijana, badala ya kuangalia kuwahi shule kama suala la nidhamu pekee.

Akizungumza kwa niaba ya Mganga mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma Mkoani Songwe Dokta Abdulazack Haji ametaja madhara ya mtoto au mwanafunzi kukosa usingizi wa kutosha.

"Madhara ya mtoto au mwanafunzi ambaye amepata muda mfupi wa kupumzika mara nyingi tunayagawanya katika makundi matatu
ambayo ni Cognitive efect linalolenga mtoto kujitambua ambalo mtoto anakosa umakini( Short attention span), pili ni hisia ya utabia (Uwezo wa kukumbuka unapungua) kundi la tatu ni afya ya Mwili (uwezo wa mtoto kutatua changamotombalimbali unapungua) mood swings mtoto kukasirika bila sababu ,Usingizi wa kutosha una umuhimu katika ukuaji wa mtoto, afya ya akili, kumbukumbu na uwezo wa kuzingatia.

Hivyo, mtoto anayelazimika kuamka mapema sana anapaswa pia kupata muda wa kutosha wa kulala usiku ili kutimiza mahitaji hayo " Alisema Abdulazack

Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Tunduma Bi Tutindaga Mwakibete anasema Dalili za uchovu kwa wanafunzi zinaweza kuonekana hata ndani ya darasa.
Mtoto anayelala muda mfupi anaweza kufika shuleni akiwa amechoka, mwenye usingizi na kushindwa kuzingatia somo kwa muda mrefu. Hali hii inaweza kuathiri ushiriki wake darasani, uwezo wa kukumbuka anachofundishwa na utendaji wake wa kielimu huku akisema kuwa katika Shule yake tatizo hilo linaonekana nyakati za Masomo ya mchana kutokana na njaa huku akishauri wazazi kuchangia chakula Mashuleni ili kupungiza uchovu kwa wanafunzi.

Kwa upande wa wazazi, kuwahi shule kunaonekana kuwa jambo la msingi katika kumjenga mtoto kuwa na nidhamu na kuheshimu muda. Hata hivyo, baadhi ya wazazi wanakiri kuwa changamoto hujitokeza kwani mtoto hulazimika kuamka mapema zaidi.

Wazazi pia wanakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha watoto wanalala mapema wakati mwingine kutokana na kazi za shule, matumizi ya simu, televisheni, michezo ya video au majukumu ya kifamilia.
Walimu nao wana nafasi muhimu katika mjadala huu kwa sababu ndio wanaoshuhudia moja kwa moja hali ya mwanafunzi anapofika darasani.
[08/09/2026 12:47] Haramba: Baadhi ya walimu wanaweza kubaini wanafunzi wanaofika shuleni wakiwa na dalili za uchovu au usingizi, hali inayoweza kupunguza umakini wao.

Kwa mtazamo wa walimu, kuwahi shule kunaweza kuwa na manufaa ikiwa mwanafunzi amepata muda wa kutosha wa kupumzika, lakini ratiba ya mapema kupita kiasi inaweza kuwa changamoto endapo mtoto analazimika kupunguza muda wake wa usingizi.

Tatizo linaweza kuwa kubwa zaidi kwa watoto wanaoishi katika familia ambazo ratiba zao za maisha huwalazimisha watoto kulala usiku. Baadhi ya watoto husaidia kazi za nyumbani, kufanya shughuli za kiuchumi za familia au kumalizia kazi za shule kabla ya kwenda kulala.

Endapo mtoto anapaswa kuamka alfajiri ili kuwahi shule, muda wa kulala unaweza kupungua zaidi. Hivyo, wataalamu wanashauri suala la usingizi wa mtoto liangaliwe kwa kushirikisha familia, shule na mazingira anamoishi mtoto.

Kwa wazazi, hatua muhimu ni kuweka utaratibu unaomsaidia mtoto kupata usingizi wa kutosha. Hii inaweza kujumuisha kupanga muda wa kufanya kazi za shule, kupunguza matumizi ya simu na vifaa vya kielektroniki kabla ya kulala, kuhakikisha mtoto ana mazingira tulivu ya kulala na kumsaidia kuwa na muda maalumu wa kwenda kitandani.

Kwa upande wa shule, mjadala huu unahitaji kuangalia zaidi ya mahudhurio na kuchelewa, Ratiba za masomo zinapaswa kuzingatia pia afya na uwezo wa mwanafunzi kujifunza. Hii haimaanishi kwamba kuwahi shule hakuhitajiki, bali inahitaji kuwepo kwa uwiano kati ya nidhamu ya muda, muda wa safari, ratiba ya nyumbani na mahitaji ya usingizi ya mtoto.

Ushirikiano kati ya walimu, wazazi, wataalamu wa afya na watungasera unaweza kusaidia kutambua changamoto zinazowakabili wanafunzi katika mazingira tofauti.

Hata hivyo, swali muhimu si tu “Mtoto anawahi shule?”, bali pia “Mtoto anayewahi shule amepata usingizi wa kutosha wa kumwezesha kujifunza?” Jibu la swali hili linahitaji wazazi, walimu, wataalamu wa afya na watunga sera kuangalia kwa pamoja ratiba zinazolinda afya huku zikiboresha mazingira ya kujifunza.
 
Tuache kutetea ujinga kwahiyo waende saa nne asubuhi??

Mm nikiamka nikifungua tuu mkulima wangu wote wapo nje kumi na mbili unusu nawapakiza kwenye Phoenix yangu na mama yao tyr kuwapeleka shuleni.....

mbamizwa ndege cc secretarybird
Binti wa maarifa ShesRise_1
BICHWA KOMWE katumeni wa kike
min -me
Seran mamnyong'ode
Dr am 4 real PhD
Umenikumbusha mwaka 2014 hadi 2017 nilivyokuwa namwamsha mwanangu wa sekondari kila asubuhi, yaani akiamka nawasha redio yangu, nampigia ule wimbo wa Maroon Commandos uitwao 'Uvivu Mbaya', namshukuru mungu kijana kila akiusikia ule wimbo hamasa ya kusoma kwa bidii ilikuwa inaongezeka.

"...hata wewe mwanangu amka kumekucha,
kwani hizi ndizo saa za kwenda shule,
hata wewe karani amka kumekucha,
kwani hizi ndizo saa za kwenda kazi, Uvivu ndiyo adui kwa ujenzi wa Taifa,
jeupeshe na Uvivu tujenge Taifa..." 🎵🎶

Cc makaveli10,
Dr am 4 real PhD.
 
Aisome
Eli Cohen 😁 jasusi langu

Wimbo ni mtamu sana kaka ndege wewe uliamua kutumia POSITIVE MOTIVATION

Unajua nini NEGATIVE MOTIVATION ni BAKORA/ FIMBO
 
Huwa sipendelei kuwacharaza vijana wangu bakora kaka. Bakora natumia ikibidi sana maana maandiko matakatifu yanasema usimnyime sana mtoto bakora.
 
Umenikumbusha mwaka 2014 hadi 2017 nilivyokuwa namwamsha mwanangu wa sekondari kila asubuhi, yaani akiamka nawasha redio yangu, nampigia ule wimbo wa Maroon Commandos uitwao 'Uvivu Mbaya', namshukuru mungu kijana kila akiusikia ule wimbo hamasa ya kusoma kwa bidii ilikuwa inaongezeka.

"...hata wewe mwanangu amka kumekucha,
kwani hizi ndizo saa za kwenda shule,
hata wewe karani amka kumekucha,
kwani hizi ndizo saa za kwenda kazi, Uvivu ndiyo adui kwa ujenzi wa Taifa,
jeupeshe na Uvivu tujenge Taifa..." 🎵🎶

Cc makaveli10,
Dr am 4 real PhD.
Mwanangu eeeh

Jiepushe na uvivu tujenge taifa,

Mwanangu amka kumekucha... Tujenge taifa
Nakumbuka kipindi hicho nikiwa pale kwetu old moshi mahoma
 
WATOTO KUWAHI SHULE ALFAJIRI: JE, NI MAFANIKIO YA KIELIMU AU TISHIO KWA AFYA?

Na Dickson Kapungu Kutoka Songwe.

Watoto kuwahi shule alfajiri imekuwa sehemu ya maisha ya kila siku kwa wanafunzi, Wengine huamka mapema sana ili kujiandaa, kutembea umbali mrefu na kutumia usafiri wa umma kuwahi masomo.

Wazazi na walimu wanaona kuwahi shule kuwa sehemu ya kujenga nidhamu, uwajibikaji na matumizi mazuri ya muda, lakini suala hili linaibua mjadala kuhusu iwapo ratiba hizo zinaendana na mahitaji ya mtoto kiafya.

Baadhi ya wanafunzi mkoani Songwe wanadai kuna wakati wanashindwa kuzingatia masomo darasani kwasababu ya uchovu unaotokana na usingizi wanao katisha kwa kuamka saa kumi na moja alfaji huku wakichelewa kulala kutokana na kukaa muda mrefu shuleni.

Marry Ayubu Kinyamagoha ni mwanafunzi wa Darasa la sita katika Shule ya msingi Tunduma anaeleza kuwa ratiba inamlazimisha kulala saa nne usiku kutokana na kuchelewa kurudi shule ambapo anatoka saa 12 jioni na akifika nyumbani husaidia wazazi kuandaa chakula cha jioni had saa 4 na kulazimika kuamka saa 11 ambapo hulala kwa masaa 7 hadi 8.

LABAN ZAKARIA mwanafunzi wa Shule ya msingo Tunduma anaeleza kuwa kuamka mapema baada ya kulala usiku kunaweza kumfanya ahisi usingizi wakati wa masomo na hivyo kushindwa kufuatilia vizuri kile kinachofundishwa huku akieleza changamoto za kukimbizwa na Mbwa ambao wanakuwa bado hawajafungiwa nyakati za asubuhi.

Kwa mujibu wa Centers for Disease Control and Prevention (CDC), watoto wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanahitaji takribani saa 9 hadi 12 za usingizi kwa siku, huku vijana wenye miaka 13 hadi 18 wakihitaji saa 8 hadi 10.

Utafiti wa mwaka 2026 uliochapishwa katika jarida la Sleep Medicine umeonyesha kuwa shule katika maeneo mbalimbali huanza masomo mapema, hali ambayo imehusishwa na changamoto ya wanafunzi, hasa vijana, kutopata usingizi wa kutosha. Utafiti huo unaongeza mjadala kuhusu umuhimu wa kuangalia muda wa kuanza shule sambamba na mahitaji ya usingizi ya watoto na vijana, badala ya kuangalia kuwahi shule kama suala la nidhamu pekee.

Akizungumza kwa niaba ya Mganga mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma Mkoani Songwe Dokta Abdulazack Haji ametaja madhara ya mtoto au mwanafunzi kukosa usingizi wa kutosha.

"Madhara ya mtoto au mwanafunzi ambaye amepata muda mfupi wa kupumzika mara nyingi tunayagawanya katika makundi matatu
ambayo ni Cognitive efect linalolenga mtoto kujitambua ambalo mtoto anakosa umakini( Short attention span), pili ni hisia ya utabia (Uwezo wa kukumbuka unapungua) kundi la tatu ni afya ya Mwili (uwezo wa mtoto kutatua changamotombalimbali unapungua) mood swings mtoto kukasirika bila sababu ,Usingizi wa kutosha una umuhimu katika ukuaji wa mtoto, afya ya akili, kumbukumbu na uwezo wa kuzingatia.

Hivyo, mtoto anayelazimika kuamka mapema sana anapaswa pia kupata muda wa kutosha wa kulala usiku ili kutimiza mahitaji hayo " Alisema Abdulazack

Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Tunduma Bi Tutindaga Mwakibete anasema Dalili za uchovu kwa wanafunzi zinaweza kuonekana hata ndani ya darasa.
Mtoto anayelala muda mfupi anaweza kufika shuleni akiwa amechoka, mwenye usingizi na kushindwa kuzingatia somo kwa muda mrefu. Hali hii inaweza kuathiri ushiriki wake darasani, uwezo wa kukumbuka anachofundishwa na utendaji wake wa kielimu huku akisema kuwa katika Shule yake tatizo hilo linaonekana nyakati za Masomo ya mchana kutokana na njaa huku akishauri wazazi kuchangia chakula Mashuleni ili kupungiza uchovu kwa wanafunzi.

Kwa upande wa wazazi, kuwahi shule kunaonekana kuwa jambo la msingi katika kumjenga mtoto kuwa na nidhamu na kuheshimu muda. Hata hivyo, baadhi ya wazazi wanakiri kuwa changamoto hujitokeza kwani mtoto hulazimika kuamka mapema zaidi.

Wazazi pia wanakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha watoto wanalala mapema wakati mwingine kutokana na kazi za shule, matumizi ya simu, televisheni, michezo ya video au majukumu ya kifamilia.
Walimu nao wana nafasi muhimu katika mjadala huu kwa sababu ndio wanaoshuhudia moja kwa moja hali ya mwanafunzi anapofika darasani.
[08/09/2026 12:47] Haramba: Baadhi ya walimu wanaweza kubaini wanafunzi wanaofika shuleni wakiwa na dalili za uchovu au usingizi, hali inayoweza kupunguza umakini wao.

Kwa mtazamo wa walimu, kuwahi shule kunaweza kuwa na manufaa ikiwa mwanafunzi amepata muda wa kutosha wa kupumzika, lakini ratiba ya mapema kupita kiasi inaweza kuwa changamoto endapo mtoto analazimika kupunguza muda wake wa usingizi.

Tatizo linaweza kuwa kubwa zaidi kwa watoto wanaoishi katika familia ambazo ratiba zao za maisha huwalazimisha watoto kulala usiku. Baadhi ya watoto husaidia kazi za nyumbani, kufanya shughuli za kiuchumi za familia au kumalizia kazi za shule kabla ya kwenda kulala.

Endapo mtoto anapaswa kuamka alfajiri ili kuwahi shule, muda wa kulala unaweza kupungua zaidi. Hivyo, wataalamu wanashauri suala la usingizi wa mtoto liangaliwe kwa kushirikisha familia, shule na mazingira anamoishi mtoto.

Kwa wazazi, hatua muhimu ni kuweka utaratibu unaomsaidia mtoto kupata usingizi wa kutosha. Hii inaweza kujumuisha kupanga muda wa kufanya kazi za shule, kupunguza matumizi ya simu na vifaa vya kielektroniki kabla ya kulala, kuhakikisha mtoto ana mazingira tulivu ya kulala na kumsaidia kuwa na muda maalumu wa kwenda kitandani.

Kwa upande wa shule, mjadala huu unahitaji kuangalia zaidi ya mahudhurio na kuchelewa, Ratiba za masomo zinapaswa kuzingatia pia afya na uwezo wa mwanafunzi kujifunza. Hii haimaanishi kwamba kuwahi shule hakuhitajiki, bali inahitaji kuwepo kwa uwiano kati ya nidhamu ya muda, muda wa safari, ratiba ya nyumbani na mahitaji ya usingizi ya mtoto.

Ushirikiano kati ya walimu, wazazi, wataalamu wa afya na watungasera unaweza kusaidia kutambua changamoto zinazowakabili wanafunzi katika mazingira tofauti.

Hata hivyo, swali muhimu si tu “Mtoto anawahi shule?”, bali pia “Mtoto anayewahi shule amepata usingizi wa kutosha wa kumwezesha kujifunza?” Jibu la swali hili linahitaji wazazi, walimu, wataalamu wa afya na watunga sera kuangalia kwa pamoja ratiba zinazolinda afya huku zikiboresha mazingira ya kujifunza.
Wazazi wengine ni WEHU ,utampelekaje mtoto aende kusoma shule ya mbali wakati za karibu zipo? Mizazi mingine ni ile ambayo imekariri ebwana shule flani ni nzuri kwahiyo hata ikiwa 30km kutoka kwake anaona UFAHARI kumpeleka...Mimi sifanyi huo Upumbavu,wangu wanasoma 3km kutoka home ,wanaamka saa moja na robo wanajiandaa nusu saa ,saa mbili kasoro wanatoka ,saa mbili kasoro 5 wapo shule.

Mambo ya kuwaamsha watoto saa 10 alfajiri huo UJINGA siwezi kufanya.
 
Tishio kwa afya na wasimamizi wamelala usingizi wa kufa.
 
Kuna siku nimetoka huko nilipotoka kwenye mida ya saa 11 alfajiri. Nakutana na mtoto wa jirani yangu yupo na dada wa kazi, anampeleka dogo akapande gari la shule.

Dogo ana usingizi kabisa unamuona na ndani kaacha baba na mama wamelala ambao ni waajiriwa na wanapokea mshahara lakini Bado wamelala. Dogo hajui kusoma ni Ile unampeleka shule ili akakue, ilibidi nicheke tu.

Kuna muda watoto hawa wadogo wa day care ingetakiwa hata mida ya saa 2 hivi iwe mida yao ya shule na si alfajiri kiasi kile, Ni uonevu kabisa.
 
Ni upuuzi wa wazazi tu. Huwa nashangaa nikitoka kwenye miahe zangu za kukaba saa 11 unakutana na katoto ka miaka mitatu kako kanasubiria usafiri road
 
Back
Top Bottom