Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,438
COVID-19 imetikisa dunia, vyombo vya usafiri wa abiria dunia nzima vilisimamisha shughuli. Kwakua dunia ni kijiji kidogo kila mtu ameguswa na madhara ya ugonjwa huu.
Sehemu nyingi shughuli za kijamii zilisimama . Maduka ya chakula na ya dawa tu ndiyo yalifunguliwa kwa muda maalum huku yakizingatia umbali kati ya mtu na mtu.
Zoezi la kwenda kuhemea chakula sokoni lilichukua masaa matatu mpaka manne. Unakaa kwenye foleni kwa umbali wa mita mbili mkisubiri waliomo ndani watoke nje. Hii ilipelekea kuwa muangalifu na bidhaa ulizonunua. Watoto walipangiwa matunda yao ya kula kwa siku na mengine yaliyobaki kwaliwekwa juu ya kabati au jokofu watoto wasiyafikie na kujichulia kiholela. Ule utaratibu wa bakuli la matunda mezani ulibadilika.
Wapo waliopoteza ajira, wapo waliopoteza maisha, waliopunguziwa masaa ya kazi, wapo waliopoteza mahali pa kuishi. Watoto na wajukuu watasimulia vizazi vyao maisha waliyopitia wakati wa mfumuko wa Covid-19.