Watoto sio lazima eti

Watoto sio lazima eti

Nyanda Banka

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
304
Reaction score
1,054
"Mimi na mke wangu tumekubaliana kwamba hatutakuwa na watoto. Tunataka kufurahiya maisha yetu, Kuwa na watoto kutatuzuia." — John Cena

"Ni sawa kabisa watu kutaka watoto, lakini mke wangu na mimi hatuko tayari kuchukua jukumu hilo. Ninataka kufurahiya maisha yangu na kuwa na furaha bila mzigo wa kulea watoto. Tulifanya uamuzi huu kabla ya ndoa yetu, na tunashukuru sana kwamba tuliufanya, kwa sababu maisha yetu yamejaa furaha kwa zaidi ya miaka minne. Hatujali kuhusu kuacha watoto shuleni, kutengeneza kifungua kinywa kwaajili ya watoto, au kukaa nyumbani kutunza watoto, Sisi ni kufurahiya maisha tu. Kila mtu ana haki ya kuchagua anachotaka maishani, na kwa upande wangu, ni ndoa yenye furaha bila watoto."- John cena
1732823939012.jpg
 
Sio lazima kuwa na watoto ikiwa unajua watakukwaza ama wewe utashindwa kuwatimizia mahitaji yao

Kibongobongo ukifa bila mtoto utazikwa futi 20 na gunzi la mhindi mk*ND*n* Moshi huko wanasema hauna faida
 
Ila jamaa ana hoja. Wakati fulani watoto nao wanatusumbua sana. Tena kama hawa wa 2000, ndiyo balaa kabisa. Ni basi tu tunawavumilia.
 
Ila jamaa ana hoja. Wakati fulani watoto nao wanatusumbua sana. Tena kama hawa wa 2000, ndiyo balaa kabisa. Ni basi tu tunawavumilia.
Sema wakati fulani watu mnasumbua sana, hakuna haja ya kuwa na watu maana dunia yote hii watu unaowaona walikuwa watoto.
Sawa?
 
Bongo hii utaseeemwa wewe upate pressure ya masikio na mkeo,utapewa shutuma za gumba na utasa mawaifi na ma mkwe watadai katoto.
Utasemwa, kama mmeamua kuto zaa, timizeni hilo kimya unamtangazia nani, ukiamua kutangaza kukubali maoni yao.
.Wanaozaa, mbona kabla hawatangazi matarajio yao.
 
Sisi mbwa tunaamini kwamba:kusudi la kuishi ni kufurahi.Huyu bwana yupo sahihi kwa mtazamo wake.Linganisha na mtazamo wangu kwamba:binadamu asipokuwa chimbuko la furaha yangu basi viumbe wengine watachukua nafasi.Kati yangu na huyo bwana nani kichaa zaidi?
 
Back
Top Bottom