Watoto wa kishua hamuwezi kuielewa hii picha

sahivi ishalainika kiasi fulani
Ahahahah nakumbuka na sisi tulikuwa tunacheza mpira wa miguu siku moja niliguswa na binti mmoja hivi mguu weee nilikomaa na hivi walikuwa wanatembea kila siku peku mweee sikucheza tena mi zangu ikawa rede tu
 
Ahahahah nakumbuka na sisi tulikuwa tunacheza mpira wa miguu siku moja niliguswa na binti mmoja hivi mguu weee nilikomaa na hivi walikuwa wanatembea kila siku peku mweee sikucheza tena mi zangu ikawa rede tu
Hahahaaa sasa usiombe ukakanyagwa na mtu aliyewahi kuumwa funza. hatariiii
 
Siku mshua kapita ghafla mitaa ya shule na kukuta nipo napiga kinyenga na dundo aliloniletea jana yake,hizo fimbo alizonipa niliporudi dah!
 
Enzi hizo watoto wa hohehahe hakuna cha chai wala bibi yake uji, saa nne mapumziko tunapiga sembo hadi kengele ya kurudi class. Nguo zimeloa mijasho ya kutosha, saa sita break fupi tunarudi dimbani, saa nane na 30 dimbani, tukisharudi nyumbani tunapumzika, jioni tena tunarudi uwajani shuleni. Ilikuwa kama dozi ya malaria kutwa ×4!!

Na hakuna kuoga hadi siku tutakapokula wali ndo tunabananishwa, soka kama kawaida iwe kabla au baada ya kuoga.

Huu mchezo huwa ni wa kipekee sana aisee, vipaji vingi vinafia vijijini huko kutokana na mazingira ya bara letu, wazazi hawajui faida za michezo, ukiwa unacheza sana ni viboko tu hadi unaacha! Pia watoto tulikuwa tunacheza tu tukiwa hatujui kwamba hiyo ni ajira yenye mshahara mrefu sana huko majuu!

Akina Diego Costa, Roberto Carlos, Carlos Tevez, Salomon Kalou, Ronaldinho Gaucho, Didier Drogba..etc..etc walianzia kwenye mazingira magumu na wengi wao walikuwa vijijini ndani sana, lakini kwakuwa ni mambele, waliweza kujua faida na kutumia vyema vipaji vyao. Sisi tunabanana na jiwe letu huku maisha yanatupiga, umri umeshasonga na hata kutuliza kabumbu tu ni seleka!
 
Hakika kabisa mi nilikuwaga hata sijisomeiii yaan ni michezo tu ,mara rede,dama, Ukimwi, yaan ilikuwa balaa

Sasa hivi ndio fainali ila nyie wenzetu mna masponsa. Sie tuliona kubeba kaunta book ni nzito huku kuamka mapema ikiwa kama adhabu, sasa hivi tunaamka kwa lazima na maisha yanatuchezesha kwata.
 
Ha hahaha kitambo sana 1989 nilikua sipewi nafasi kwa sababu ya njumu zangu nakaa bench hadi siku mtakapo siacha ndo napiga game
 
hahahaha enzi zangu, nlisumbua sana walikuwa wananiita REDONDO mana nlikuwa mtu wa kufinya finya hata ktk 18,,
 
Katika vitu ambavyo ninajivunia kwa sasa ni kupitia kwenye maisha hayo,,,,hawa watoto wa sahiz hata wakikua sijui watasimuliana nini yani
 
Sasa hivi ndio fainali ila nyie wenzetu mna masponsa. Sie tuliona kubeba kaunta book ni nzito huku kuamka mapema ikiwa kama adhabu, sasa hivi tunaamka kwa lazima na maisha yanatuchezesha kwata.
Haahahah jamanii wanawake tuna raha eee
 
Umaskini huu. Yatupasa kuwatoa watoto wetu wasipitie hiyo hali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…