Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
AhahahahahahahMi nilikuwa nikija na mpira wenyewe tukiita "sembo" lazima nicheze mwanzo mwisho, nikitolewa tu natambaa na mpira wangu mechi inaisha!
[emoji23][emoji23][emoji23]mchoyoo alikuwahahahahaaa we ulikua wakishua mwanangu na hapo lazma mpira unaozungumzia ni gozi,,,,, mana hii ya makaratasi ilikua haiitaji idadi ya wachezaji ndani....hata mkiwa 30 mnakipiga tu[emoji16]
AhahahahahahWa kishua akija na gozi hata kama hajui mpira lazima apangwe.
Jamani njaa vipii ?mkirudi home jeNilikua nikifika uwanjani kama wameanza kucheza mechi inasimama wananigombania,yani nikiamua kucheza timu moja ile nyingine inapewa wachezaji wawili kama compensation kufidia..
Kutoa kucha,ngozi za kwenye vidole,magotini,kawaida,shida wakati wa kuoga *****. Yani kuna siku tulicheza sijui kuanzia saa 4 adi saa 12 njaa haziumi .
Kwanini ulikuwa huvui shatiMie tatizo lilikua moja tu. Timu moja lazima mvue mashati ili kutofautisha na wapinzani. Sasa nilikua chikondee hatari. Wakifikia hapo lazima nifanye figisu nisivue shati.....
Baadae nikawa jiniaz, nnachelewa kidogo mpira uanze, nikifika naingia timu ya wenye mashati. Vidole gumba hadi leo vimeenda upande.
Sasa unashabikia nini?Nilipoanza form one nikawa busy na masomo ila nilibaki kuwa mshabiki tu mpira, isitoshe nilikutana na wababe wa mpira jambo ambalo lilinifanya niachie nafasi watu waoneshe viwango vyao.
Jinsi muda ulivyozidi kwenda hadi kufika Advance nikaacha kushabikia kabisa mpira hadi sasa hivi, mpira sina time nao kabisa
Kwanini ulikuwa huvui shati
ukitaka ndoa ife mwambie mkeo mwanao asome moja ya hizo shule!Yani mzee mzima nakumbuka niling'oa mtoto mmoja wa uswaz mwenzangu kwa ajili ya hii kitu.
Sasa kuna siku nilifunga goli 20 peke yangu yani.....huku vipaji vingi sana vimepotea huku...yote ni kwa ajili ya malez ya bara letu kwa watoto.
Namiss sana enzi hiziView attachment 748243
Njaa ilikua haiumagi kabisa, yani iyo ilikuwa jumamosi, ukishakunywa chai/uji ni safari. Kurud home unajua kabisa una fimbo zako kadhaa,na chakula kimeisha so unasubiria cha usiku.Jamani njaa vipii ?mkirudi home je
AhahhahaahhaNjaa ilikua haiumagi kabisa, yani iyo ilikuwa jumamosi, ukishakunywa chai/uji ni safari. Kurud home unajua kabisa una fimbo zako kadhaa,na chakula kimeisha so unasubiria cha usiku.
Ahahahahukitaka ndoa ife mwambie mkeo mwanao asome moja ya hizo shule!
utasikia watu watatuelewaje utafikiri hao watu ndo kaolewa nao!
HaahahahahahahNani anataka kuhesabiwa mbavu kizembekizembe? Nilikua mwembamba hatari.
Hamna ninachoshabikia kwa sasaSasa unashabikia nini?
Unakaa darasani unawaza breki tu jamaniPole sana Jemedari. Hii kitu ilikua tunaisubiria kengele ya mapumziko kwa vinubi na vinanda. Ikigonga tu, mwendo wa kukamua ndimu.
Ahahahahahahah mnaniuaa mbavuUnatumwa dukani ila ukikuta wanaume wanasukuma kabumbu unajumuika nao. Mpira ukiisha ndio unazinduka kwamba uliagizwa vitu vya muhimu na wakati huo ni saa moja usiku alafu mchafu haufai.
Utashushiwa kipigo cha mbwa mwizi lakini kesho mambo yako vilevile. Ndio siku hizi nahiuliza au hii tabia ya kuchepuka huku tukijua madhara iliimarishwa kipindi hicho?