Watoto wa kishua hamuwezi kuielewa hii picha

Watoto wa kishua hamuwezi kuielewa hii picha

mwenye mpira akiona vipi anakamata mpira wake anasema 'kwa leo' halafu nduki na mpira wake
 
mwenye mpira akiona vipi anakamata mpira wake anasema 'kwa leo' halafu nduki na mpira wake
 
hahahahaaa we ulikua wakishua mwanangu na hapo lazma mpira unaozungumzia ni gozi,,,,, mana hii ya makaratasi ilikua haiitaji idadi ya wachezaji ndani....hata mkiwa 30 mnakipiga tu[emoji16]
[emoji23][emoji23][emoji23]mchoyoo alikuwa
 
Nilikua nikifika uwanjani kama wameanza kucheza mechi inasimama wananigombania,yani nikiamua kucheza timu moja ile nyingine inapewa wachezaji wawili kama compensation kufidia..
Kutoa kucha,ngozi za kwenye vidole,magotini,kawaida,shida wakati wa kuoga *****. Yani kuna siku tulicheza sijui kuanzia saa 4 adi saa 12 njaa haziumi .
Jamani njaa vipii ?mkirudi home je
 
Mie tatizo lilikua moja tu. Timu moja lazima mvue mashati ili kutofautisha na wapinzani. Sasa nilikua chikondee hatari. Wakifikia hapo lazima nifanye figisu nisivue shati.....

Baadae nikawa jiniaz, nnachelewa kidogo mpira uanze, nikifika naingia timu ya wenye mashati. Vidole gumba hadi leo vimeenda upande.
Kwanini ulikuwa huvui shati
 
Nilipoanza form one nikawa busy na masomo ila nilibaki kuwa mshabiki tu mpira, isitoshe nilikutana na wababe wa mpira jambo ambalo lilinifanya niachie nafasi watu waoneshe viwango vyao.

Jinsi muda ulivyozidi kwenda hadi kufika Advance nikaacha kushabikia kabisa mpira hadi sasa hivi, mpira sina time nao kabisa
Sasa unashabikia nini?
 
Yani mzee mzima nakumbuka niling'oa mtoto mmoja wa uswaz mwenzangu kwa ajili ya hii kitu.

Sasa kuna siku nilifunga goli 20 peke yangu yani.....huku vipaji vingi sana vimepotea huku...yote ni kwa ajili ya malez ya bara letu kwa watoto.

Namiss sana enzi hiziView attachment 748243
ukitaka ndoa ife mwambie mkeo mwanao asome moja ya hizo shule!
utasikia watu watatuelewaje utafikiri hao watu ndo kaolewa nao!
 
sasa watacheza lini wanaishia games za simu kwanza viwanja vya shule vimevamiwa. Hakuna nyakati nzuri kama hizi. sheria 17 za mpira hapa hazina nafasi yake
 
Unatumwa dukani ila ukikuta wanaume wanasukuma kabumbu unajumuika nao. Mpira ukiisha ndio unazinduka kwamba uliagizwa vitu vya muhimu na wakati huo ni saa moja usiku alafu mchafu haufai.

Utashushiwa kipigo cha mbwa mwizi lakini kesho mambo yako vilevile. Ndio siku hizi nahiuliza au hii tabia ya kuchepuka huku tukijua madhara iliimarishwa kipindi hicho?
Ahahahahahahah mnaniuaa mbavu
 
Back
Top Bottom