Watoto wa kishua hamuwezi kuielewa hii picha

Watoto wa kishua hamuwezi kuielewa hii picha

Hatarr ila kipindi hicho hata ukilowa hakuna wowowo La kuangalia maana du umekazia kuloa chakachaka
Hakuna mchezo ambao sijacheza utotoni aisee...
Mdaku, rede, vitoto etc
Kulikua na tim ya mabint na yetu..
Eti kombolela tunajificha kitandan na shuka tunajifunika😀😀
 
Me kuna siku nilifunga magoli 75!
Halafu kuna ile kitu inaitwa tobo, ukipigwa tobo aisee ilikuwa unakimbizwa, ukikamatwa unakula kisago...ponea yako ilikuwa unapaswa ukimbie hadi ushike kisiki au mti uliopangwa!
Hahahaahaaaa.
Hii tobo nilimuotea jamaa, kipindi hicho tupo darasa la pili muda wa mapumziko saa nne.

Tulikuwa tunasimika kijiti chini ili mtu anakipige halafu akimbie akashike ama shina la mti ulio umbali fulani huku tukiwa tunamfukuza kumshushie kichapo cha ngumi.

Mimi nilikuwa karibu na tobo ilipo na wenzangu pia, walikuwepo, sasa jamaa akapiga tobo bahati nzuri wakati anaanza kukimbia akapita karibu na mimi, nikaachia ngumi tumboni kwake jamaa aliumia akasimama hapo hapo hakuweza kukimbia tena kwa maumivu.

Mimi baada ya kuona hivyo nilitetemeka sana na kuhofia kuja kunipiga baadae maana alikuwa ananizidi, ila washkaji wakaja kunitetea sikupigwa na huyo jamaa.

Kuanzia hiyo siku nikawa muoga kushiriki mchezo wa tobo.
 
Kweli mkuu yaan nikiwaona wanangu wanacheza nataman nicheze namm 😀😀😀
Unaingia kwani tatizo nn mi mwenyewe nikikuta lede siku hizi naingia na umama wote nauweka pembeni ule mpira wa wasichana mnafumia soksi za shule usipotoa soksi hauchezi
 
Hahahaahaaaa.
Hii tobo nilimuotea jamaa, kipindi hicho tupo darasa la pili muda wa mapumziko saa nne.

Tulikuwa tunasimika kijiti chini ili mtu anakipige halafu akimbie akashike ama shina la mti ulio umbali fulani huku tukiwa tunamfukuza kumshushie kichambo cha ngumi.

Mimi nilikuwa karibu na tobo ilipo na wenzangu pia, walikuwepo, sasa jamaa akapoga tobo bahati nzuri wakati anaanza kukimbia akapita karibu na mimi, nikaachia ngumi tumbo kwake jamaa aliumia akasimama hapo hapo hakuweza kukimbia tena kwa maumivu.

Mimi hmbaada ya kuona hivyo nilitetemeka sana na kuhofia kuja kunipiga baadae maana alikuwa ananizidi, ila washkaji wakaja kunitetea sikupigwa na huyo jamaa.

Kuanzia hiyo siku nikawa muoga kushiriki mchezo wa tobo.
Sisi kushika ilikua ukata wa nyumba ya mwalimu kama umbali wa viwanja viwili, kama huna mbio wafwa
 
Unaingia kwani tatizo nn mi mwenyewe nikikuta lede siku hizi naingia na umama wote nauweka pembeni ule mpira wa wasichana mnafumia soksi za shule usipotoa soksi hauchezi
Mamdogo na shost zake ndio ilikua zao kucheza lede basi mm sikai mbali ili nione vichupi 😀🙁🙂🙂
 
sasa huo mpira kuna watu hawajui mpka leo unafumwa kwa kamba za aina gn
 
Haaaaaa wacha we migombani mhhh


Hebu tusiharibu uzi wa wenyewe.

Aisee kwenye safari za kuchota maji na kutafuta kuni au kukata majani ya mbuzi na ng'ombe...acha kabisa.

Kama una binti umevutiwa naye (na hapa ni primary..hata nikifirikia sasa siamini aisee!) basi unamvizia akienda kuchota maji. Unamwambia akusubirie mgombani, unaenda kumchotea unafanya haraka ukirudi anakutunuku.

Tulivyozidi kukua, tukaboresha unakuwa na maji yako tayari au kuni ulishakata, au asubuhi ile kabla hata hujaenda shule unawahi unakata mifuko miwili ya majani...jioni mkitoka shule unamwambia utampa nusu..mnakutana migombani mnafanya barter trade!

Kwa kweli nikiri hilo suala la kutumia kondomu kufuma mipira ilikuwa jambo geni (na anasa) kwetu. Tena nakumbuka tuliwahi kwenda kwa wajomba (upande wa mama) tukakuta wanatumia lile gamba la mgomba. Kamba yake ni ngumu balaa, mpira haukatiki haraka ila nao unaumizaje.

Ah utoto raha sana jamani....
 
Hii concept ya "watoto wa kishua" ni udogoni tuu wakiwa wakubwa wanakutana na taabu za dunia kama wengine na kuifuta historia yao ya nyuma
Tena kwa usawa huu watajiita watoto wa Kichuya! 😀😀
 
Back
Top Bottom