Watoto wa kishua hamuwezi kuielewa hii picha

Watoto wa kishua hamuwezi kuielewa hii picha

Unatumwa dukani ila ukikuta wanaume wanasukuma kabumbu unajumuika nao. Mpira ukiisha ndio unazinduka kwamba uliagizwa vitu vya muhimu na wakati huo ni saa moja usiku alafu mchafu haufai.

Utashushiwa kipigo cha mbwa mwizi lakini kesho mambo yako vilevile. Ndio siku hizi nahiuliza au hii tabia ya kuchepuka huku tukijua madhara iliimarishwa kipindi hicho?

Mimi ilinikuta moja . Nilitumwa kumnunulia baba sigara,nilikua na mdogo wangu. Tumeshanunua wakati tunarudi njiani tukakuta kipute ,nikampa vitu dogo avishike ,nikaingia dimbani.
Kumbe baba alikua hana hata za kuvutia muda,anatusubiri sisi. Mara namuona mama huyu hapa. Dah! Ile dhoruba niliyopata si mchezo. Mimi ndiye mkubws, dogo wala hakupigwa.
 
Mimi ilinikuta moja . Nilitumwa kumnunulia baba sigara,nilikua na mdogo wangu. Tumeshanunua wakati tunarudi njiani tukakuta kipute ,nikampa vitu dogo avishike ,nikaingia dimbani.
Kumbe baba alikua hata za kuvutia muda,anatusubiri sisi. Mara namuona mama huyu hapa. Dah! Ile dhoruba niliyopata si mchezo. Mimi ndiye mkubws, dogo wala hakupigwa.

Na bado haukukoma, kiu ya kabumbu haielezeki. ile hata kama unaumwa umetundikiwa drip, ukiwaona wenzako wanapiga ndimu lazima upone.
 
hii kitu ilisababisha darasa letu kuwa na kambi mbili pinzani. "wafupi" na warefu" kila tunapopata muda (pumziko ama muda wa kutoka) lazima tukacheze ili mbabe apatikane

ushindani ukahamia kwenye masomo kila kambi ikitaka top 10 iingize watu wengi. mwalimu akikuja kugundua baadae baada ya kambi mojawapo kuingiza watu 6 kati ya 10. ikapigwa sherehe ya nguvu.

hii kitu imetuacha na makovu ya kutosha.
 
Yani mzee mzima nakumbuka niling'oa mtoto mmoja wa uswaz mwenzangu kwa ajili ya hii kitu.

Sasa kuna siku nilifunga goli 20 peke yangu yani.....huku vipaji vingi sana vimepotea huku...yote ni kwa ajili ya malez ya bara letu kwa watoto.

Namiss sana enzi hiziView attachment 748243
Imenikumbusha mbali sana hii saa nne mda wa mapumnziko inapigwa mechi ya kamari kuwekeana biki watakaofugwa goli moja harafu mda wa kuingia darasani umefika mmeshaliwa,kazi inaanza kuazima azima[emoji1]
 
Na bado haukukoma, kiu ya kabumbu haielezeki. ile hata kama unaumwa umetundikiwa drip, ukiwaona wenzako wanapiga ndimu lazima upone.

Ukome wapi ndugu , wakati ile ndiyo starehe yenyewe, baada ya mpira hao mtoni kuoga.

Kuna kipindi nilikwenda kuwatembelea Shangazi zangu Kijiji fulani huko Malinyi ,halafu jioni baada ya mpira mnakwenda kuoga mto Ruhuji , halafu huo mto una Mamba ,Viboko. Nikikumbuka utoto aisee acha tu.
 
Viwanja vyetu nimaeneo ya shule,nanyumbani baada ya mavuno ya mpunga mashamba yaliyokuwa jirani na nyumba mmoja wenu anaomba wazazi au walezi wake , mkipewa hilo eneo mnasafisha ubua wa mpunga , kipute kinaanza huo unakua uwanja wenu wa nyumbani kwa miezi mitano Julai mpaka Novemba.
 
Aisee nimecheka nimekumbuka mbali, sisi kwetu tulikuwa kila jumamosi tunacheza mechi kubwa jumamosi hii wanakuja inayofatia tunakwenda ugenini. Tatizo ilikuwa tukifungwa goli nyingi lazima tulianzishe. Basi tulikuwa tunaandaa mbwa, mtaani kwetu karibu kila nyumba ilikuwa ina mbwa. Basi siku ya mechi tunawachukua mbwa tunawaficha kwa kina Crispin nyumba yao ipo karibu na uwanja,basi tukipigwa goli nyingi tunakonyezana mambo yashaharibika tunakwenda kufungulia mbwa tulikuwa tunawafukuza wale wajinga na mbwa wanakimbia wanasahau mpaka ndala. Basi na Sisi tukienda kwao magereza tukifungwa wanatukimbiza balaa lakini cha ajabu tukikutana shuleni jumatatu tunakuwa washikaji story kama kawa na kama kuna mtu alisahau ndala zake tunamwambia njoo jioni uchukue, utoto raha sana.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sipati picha mlivyokuwa mnanuka jasho
 
kweli kabisa....yani wa viatu tulikua tunaogopa kuwakaba sasa sheria ni kuvua woote........!!! sasa hapo mi nilikua navua nabaki na zile soksi zangu za pundamilia

Peku halafu kiwanja kimejaa MBIGIRI balaa !!!!
 
Back
Top Bottom