Watoto wa kiume kutelekezwa

Watoto wa kiume kutelekezwa

mabutu1835

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2018
Posts
909
Reaction score
1,425
Ikiwa muda si mrefu tumetoka kuadhimisha miaka takribani 30 tangu masuala ya jinsia kuanza kutafutiwa suluhu huku wakiegemea kwa jinsia ya kike zaidi. Wanaume wanaonekana kama maadui na wasiofaa huku wanawake wakiaminishwa kuwa wanaweza pasipo wanaume, hii ni ajenda nyingine.

Watoto na vijana wa kiume wamenyanyapaliwa kuanzia ngazi ya familia hadi kimataifa. Kundi la watoto na vijana wa kiume hawapati miongozo hata ya kujitambua wenyewe.

Wanaume kaeni vizuri na watoto na vijana wenu wa kiume tuzingatie haya:

1: Mwambie mtoto au kijana wako wa kiume kuwa yeye ni wa kiume na unafurahia yeye kuwa mwanaume.
2: Kaa nae kwenye movie au ikibidi toka nae matembezi, usifuatane na mama yake.
3: Mwambie namna mwanaume anatakiwa kuwa na kamwe asiwe tayari kudharauliwa.
4: Mweleze anatakiwa kuwa na bidii na hodari katika maisha kuanzia darasani hadi kwenye ajira.
5: Mpe mbinu za kutokuwa mnyonge kamwe
6: Mweleze mtoto wako wa kiume asiwe mropokaji kwa mwanamke hata akimpenda vipi.
7: Mwambie kijana wako wa kiume kuwa una Imani kubwa nae na unategemea siku moja atakuwa na familia na watoto wake.
8: Mwambie asikubali ashikwe makalio, kifua chake au sehemu yoyote ya mwili wake na mwanaume mwenzake na ikibidi apigane hadi pachimbike.
9: Mvute karibu yako na awe rafiki yako kabisa na atamani na kufurahia kukuona .
Ongeza mengine kwa mustakabali wa watoto wa kiume.
 
Nafikiri wafuate vitabu vya dini yao,hivyo tu vinatosha,tukiongezea taasisi nyingine kuhusu vijana,itafikiriwa kwamba dini zao hazitoshi.
 
Back
Top Bottom