Fascinating
Senior Member
- May 14, 2025
- 146
- 351
Nimekutana hii list huko mitanaoni ikijadili ongezeko la Mabinti wa marais wa Afrika kushika nafasi za juu za kiserikali au kidiplomasia. Huu mjadala pia umewekwa na TRT Afrika ukinaonyesha orodha za mabinti wa maraisi ambao wnashika nafasi nyeti kwenye utawala wa wazazi wao.
Orodha imekuwa na maoni tofauti, baadhi wanaungamkono kwa kutumia hoja ya uaminifu huku kuna kundi linalo pinga kwa muktadha wa muendelezo wa mifumo ya kifamilia kwenye siasa. Hii ndio oradha ya mabinti wa Marais mbali mbali Afrika ambao wanashika nafasi nyeti katika tawala za wazazi wao:
1. Wanu Hafidh Ameir (Tanzania 🇹🇿)
Mtoto wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan. Yeye anahudumu kama Naibu Waziri wa Elimu . Ni mwanasiasa ambaye amekuwa amejizolea umaarufu siku za hivi karibuni kitu watu wanadhani ni uhusiano wake mama yake ambaye ndio raisi wa nchi.
2. Charlene Ruto (Kenya 🇰🇪)
Anajulikana kama "Youth Champion" na anaendesha kile kinachoitwa (ofisi isivyo rasmi) kama "Office of the First Daughter." Amekuwa akizunguka nchi nzima na hata nje ya nchi akikutana na viongozi, jambo ambalo limezua mjadala mkubwa nchini Kenya kuhusu nafasi yake kisheria.
3. Ange Kagame (Rwanda 🇷🇼)
Binti wa Rais Paul Kagame. Yeye ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Mikakati na Sera (Strategy and Policy Council) katika Ofisi ya Rais. Ameonekana mara nyingi kwenye mikutano mikuu ya kidiplomasia akimsaidia baba yake.
4. Jihan Hassan Sheikh (Somalia 🇸🇴)
Anahudumu kama Mshauri wa Rais (Presidential Adviser) kwa baba yake, Rais Hassan Sheikh Mohamud. Hii inaonyesha jinsi viongozi wanavyowaamini watoto wao kuwa washauri wa karibu wa siri na mikakati.
5. Wengine Kwenye Orodha ni:

- Adut Salva Kiir (Sudan Kusini 🇸🇸): Mjumbe Mwandamizi wa Rais (Senior Presidential Envoy).
- Keneilwe Ramaphosa (Afrika Kusini 🇿🇦): Msanifu Majengo ambaye huonekana mara nyingi kwenye misafara rasmi ya kiserikali ya Rais Cyril Ramaphosa.
- Princess Sikhanyiso Dlamini (Eswatini 🇸🇿): Mkurugenzi Mtendaji wa Masuala ya Uchumi katika ofisi ya Mfalme, na aliwahi kuwa Waziri wa Habari.
- Uwezo Binafsi: Je, watoto hawa wanapewa nafasi hizi kwa sababu ya elimu na uwezo wao, au ni kwa sababu tu ya majina ya baba na mama zao?
- Maandalizi ya Uongozi: Je, hii ni njia inayotumiwa na viongozi wa kiafrika kuandaa vizazi vyao kuja kuwa viongozi (Succession planning)?
- Maadili na Katiba: Ni sawa kimaadili kwa Rais kumteua mwana we wa damu kwenye nafasi nyeti za kiserikali?