March 29, 2026
Even With a Title Deed You Can still Lose Your Land — Lawyer Omari Explains Why
View: https://m.youtube.com/watch?v=fnQLSSSzFJo
16 May 2026
Mahakama Kuu ya Tanzania
Dar es Salaam, Tanzania
MJANE ALIYETIMULIWA NA RC ALBERT CHALAMILA AKIMBILIA MAHAKAMANI KUU, UAMUZI MEI 29, 2026
View: https://m.youtube.com/watch?v=JokIMPZ34E4Bi. EverlinChiomba wa 317 Regent Estate Mikocheni, Dar es Salaam Tanzania ameweza kuweka kuzui mahakama kuu ya Tanzania dhidi ya amri ya mkuu wa mkoa wa DSM RC Albert Chalamila
TOKA MAKTABA :
May 6, 2026
317 Regent Estate
Mikocheni, Dar es Salaam
Tanzania
RC CHALAMILA AMALIZA MGOGORO wa NYUMBA DAR - AMTAKA BIBI HUYU AONDOKE AMPISHE MMILIKI...
View: https://m.youtube.com/watch?v=LjGYbxUqLaEMKuu wa mkoa wa Dar es Salaam, RC Albert Chalamila, amehitimisha mgogoro wa nyumba iliyopo eneo la Mikocheni, kiwanja namba 317 Regent Estate, jijini Dar es Salaam.
Ambapo RC Albert Chalamila amesema kuwa kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, nyumba hiyo ni mali ya Godifrey Shuma na Carista Shuma.
Aidha, amemtaka Bi Everlin Chiomba, aliyekuwa akiishi hapo akidai nyumba hiyo ni mali yake aliyorithi kutoka kwa marehemu mumewe Chiomba, kuondoka kwenye nyumba hiyo ndani ya muda wa saa moja na nusu.
Akizungumza katika mtaa wa Regent, eneo la Mikocheni, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, mkuu wa mkoa RC Albert Chalamila amesema Godifrey Shuma na Carista Shuma ndio wamiliki halali wa nyumba hiyo kwa mujibu wa maelekezo ya mahakama na nyaraka zilizopo.
Hivyo, amemtaka mkuu wa wilaya ya Kinondoni pamoja na RPC wa Kinondoni kusimamia zoezi hilo ili mwenye haki akabidhiwe nyumba hiyo, huku akimtaka Bi Everlin Chiomba kurejea mahakamani endapo hataridhika na maamuzi hayo.
RC Albert Chalamila ameongeza kuwa yupo tayari kumsaidia Bi Everlin Chiomba kurejea mahakamani ili kupata ufafanuzi zaidi na ushauri wa kitaalamu.
Hata hivyo RC Albert Chalamila, amesema kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, mmiliki halali ni Godifrey Shuma na Carista Shuma. Pia ameitaka Ofisi ya Ardhi na Mahakama kumsaidia kumaliza kitendawili cha binti aliyejitokeza akidai kuwa ni mtoto wa marehemu Chiomba, aliyekuwa mmiliki wa awali wa nyumba hiyo.
Inadaiwa mtoto huyo anatumia majina mawili tofauti, Flora Chiomba na Flora Mwashaa.
Aidha, kabla ya uamuzi huo, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam aliunda kamati ya kufuatilia suala hilo. Mwenyekiti wa kamati hiyo ya mgogoro, Mbaraka Forogo, alipowasilisha taarifa yake alisema kamati imejiridhisha kuwa nyumba hiyo iliuzwa na kwamba Godifrey Shuma ndiye mwenye hati miliki ya sasa.
Vilevile, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, DC Saad Mtambule, amekemea kitendo kilichofanywa na mtoto anayedai ni wa marehemu Chiomba, Bi Flora, kwa kuleta mabaunsa kufanya fujo, wakati tayari matumizi ya mabaunsa yalishapigwa marufuku.
Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam, Shukrani Kyando, ameeleza kuwa Godifrey Shuma na Carista Shuma ndio wamiliki halali wa nyumba hiyo kwa mujibu wa nyaraka