Halafu hizi ndoa za uzeeni ni matatizo tupu.Wazee wengine sijui wakoje tu,mwisho wa siku huziacha familia katika migogoro isiyo ya lazima.
Scenario hii inafanana na ile iliyoikumba familia yetu. Baba yetu baada ya kustaafu kazi (alikuwa mtumishi wa Idara ya Afya) akaamua 'kuoa' mdada fulani ambaye kiumri anazidiwa na dada na kaka zangu wakubwa.Mdada yule alianza mahusiano na mshua mwaka mmoja kabla Mzee hajastaafu,mwaka uliofuata Mzee akastaafu na akaitumia pension kuvuta 'kigori' ndani.
Kiukweli tulikereka, ndugu zake baba nao hawakufurahishwa.Mama alipata pressure, na baada ya muda alipata stroke,na huo ndo ukawa mwisho wake.
Kilichotukera zaidi,yule mdada alikuwa mfujaji wa mali ni balaaa.Alimfundisha baba starehe ambazo hakuzijua wala kukulia.Baba akawa kituko kama 'Kiokote'.Ma'mdogo alijua kula pension, na aliitafuna hasa. Kuona vile tulimwanzishia timbwili la ukweli. Kuna siku brother alimvizia mahala akampa kipondo cha maana hadi akachakaa.
Mungu atusamehe, maana tulimtengenezea ajali akagongwa na pikipiki iliyomwachia majeraha makubwa.In short aendelee kupumzika huko kwa amani.Japo nami nitamfuata, lakini aendelee tu na pumziko lake la milele.
Ila sometimes sisi wanaume tukizeeka tunakuwaga 'vilaza' sana.