Ni kweli K.Lyn ana wakati mgumu kuthibitisha uhalali WA wosia huo Mahakamani.
Lakini MTU anaweza akamwachia urithi wake wote wa Mali KWA MTU yeyote yule anayempenda, hata kama siyo ndugu yake, mwenye mali ana haki ya kufanya hivyo. K.Lyn kilichomgharimu hapo ni kutokana na "shule ndogo kichwani", NA ushauri mbovu alioupata kutoka KWA washauri wake.
Kabla Mzee Mengi hajafariki dunia, yeye K.Lyn angemshawishi mzee ili aandike wosia ambao ni lazima " ungeshuhudiwa NA Mahakama ", NA wala siyo Wakili au kamishina WA viapo WA kawaida kama ilivyofanyika. Angemshawishi KWA nguvu zote ili akubali kuacha wosia ambao ni lazima " Ushuhudiwe NA Mahakama", tena angechagua Mahakama ya juu, kama vile Mahakama ya Wlaya, mkoa, au Mahakama KUU, NA sana sana ingekuwa Mahakama KUU ndio ingependeza zaidi.
Endapo kama Mzee Mengi angeacha wosia ambao umeshuhudiwa NA Mahakama, vurugu zote hizi zisingetokea hata kidogo.
Kuna watu ambao Mimi binafsi nawafahamu vizuri kabisa waliwahi kukumbana NA mkasa na kesi kama hii.Baba yao mzazi aliacha wosia NA kuwanyima Mali zake zote kabisa watoto wake wa kuwazaa wapatao watano, badala yake alimkabidhi urithi wake wote KWA mjukuu wake mmoja tu ambaye alikuwa anamjali. Mzee huyo alipofariki dunia, ulizuka ugomvi mkubwa sana sana WA kugombea urithi kati ya watoto wa marehemu NA mjukuu wake aliyeachiwa urithi.Kesi ilikuwa nzito ilienda mpaka Mahakama KUU, kwa kukatiwa rufaa. Mwisho WA siku mwaka 2007 mjukuu alishinda Kesi hiyo, NA hatimaye Mali zote za urithi zilirejeshwa na kukabidhiwa KWA mjukuu aliyeachiwa urithi.
Nakumbuka watoto wa mmarehemu walinyang'anywa kila kitu, mashamba, nyumba tatu, magari, etc.Tena waliondolewa kwenye nyumba za urithi za marehemu baba yao mzazi kWA nguvu NA Jeshi LA Polisi baada ya mjukuu kushinda rufaa yake ya Kesi Mahakama KUU.
Kitu kilichomuokoa mjukuu kushinda Kesi ni kwamba wosia WA mgawo WA mali za urithi/mirathi uliidhinishwa NA Mahakama, Mzee mwenyewe binafsi kabla hajafa alienda kuandika wosia Mahakamani, na kisha Mahakama iliidhinisha Wosia huo, Baba yao aliamua kuwafunza adabu watoto KWA sababu watoto wake walikuwa NA viburi , walikuwa wanamdharau Mzee wao. Ktk kuwakomesha watoto wake wenye viburi, baba yao mzazi aliamua kuwanyima mirathi, wote waliambulia patupu. Mjukuu alikabidhiwa Mali zote za marehemu.