SoC02 Watoto wa Mitaani ni Janga la Kitaifa

Stories of Change - 2022 Competition

Tukuza hospitality

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
321
Reaction score
691
Watoto wa mitaani, ni watoto ambao wanaishi mitaani, nje ya makazi ya kawaida. Kempe Ronald Hope, (2005) anatoa maana ya Mtoto wa Mitaani kama ifuatavyo: “Mtoto wa Mtaani, ni msichana au mvulana ambaye hajafikia umri wa utu uzima, ambapo mtaa (ikijumuisha makazi yasiyokaliwa, maeneo yenye mazingira magumu, na kadhalika) umekuwa makazi, na mahali pa kujikimu kimaisha, ambaye hana ulinzi wa kutosha na ambaye haongozwi na watu wazima wenye kuwajibika”.

Kuna makundi mawili ya watoto wa mitaani: Kundi la kwanza ni lile la watoto wanaoshinda mtaani, lakini jioni au usiku wanarudi nyumbani kulala; na kundi la pili ni lile la watoto ambao wanashinda na kulala mitaani.

Tafsiri nyingine imetolewa na Marcus Lyon (2003): Kwamba, “Ni watoto wanaoishi na kulala mtaani; ambao wanafanya kazi mtaani lakini wanarudi nyumbani kwao; na wale ambao wanaishi mtaani bila kurudi nyumbani.

Watoto hawa hujishughulisha na shughuli mbalimbali ili waweze kujikimu; hizi ni pamoja na vibarua vya ujira mdogo (mfano: kubeba mizigo, kuchota maji, biashara ndogondogo, kazi za ujenzi, nk); kuombaomba na wizi/udokozi.

Ukubwa wa Tatizo la Watoto wa Mitaani
Kwa mujibu wa shirika la “Consortium for Street Children” (Feb. 2021), idadi inayonukuliwa kwa kawaida ni watoto milioni 100 wa mitaani duniani kote; hata hivyo, kutokana na ukweli kwamba makadirio haya ni ya mwaka 1989, imepitwa na wakati kwa kiasi kikubwa – takwimu za ukweli hazijulikani.

Kwa mujibu wa jarida la “Arusha Press Club, (Septemba 2021)” Tanzania inakadiriwa kuwa na watoto 35,919 wanaoishi na kufanya kazi mitaani katika majiji na miji mbalimbali, licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali pamoja na wadau wengine kutokomeza tatizo hilo.

Picha 1.1: Watoto wakiomba msaada kutoka kwa wasafiri jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Watoto wa Mitaani DW Aug 2022.jpg

Picha kwa hisani ya Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (DW), April 2018

Madhara ya Tatizo la Watoto wa Mitaani

- Mara nyingi watoto hupigwa na maafisa wa serikali (wakiwemo polisi)

- Wanakosa fursa ya kupata elimu na huduma za afya

- Baadhi yao hushikiliwa polisi na/au magereza bila kuzingatia haki zao

- Baadhi ya watoto hutumikishwa na watu wazima bila ujira au kwa ujira mdogo

- Baadhi ya watoto hupigwa, kuibiwa na kutumikishwa kingono na watu wazima

- Wanakabiliana na unyanyapaa na kutengwa na jamii, jambo ambalo linaathiri afya ya akili

- Baadhi ya watoto hutumbukia katika magenge ya uhalifu, kama ya madawa ya kulevya, wizi/uporaji, nk.

Picha 2.1: Watoto wakiwa wamelala barazani katika jengo la Benjamini Mkapa , jijini Dar es Salaam​

Street Children Dar 2011.jpg

Chanzo: Deodatus Balile/Sabahi (Septemba, 2012)

Picha 2.2: Watoto wa Mtaani wakitafuta chochote Jalalani – Kasulu mjini.​

Street Children Kasl 2012 II.jpg

Chanzo: C. J. Samali (Novemba, 2012).

Ni madhila mengi yanawakumba watoto wa mitaani, hayo niliyotaja hapo ni machache kati ya mengi. Lakini kwa upande mwingine, watoto wa mitaani huchafua mazingira ya miji husika; husababisha hofu ya kuibiwa na hata kujeruhiwa kwa wakazi wa maeneo husika, kwani baadhi ya watoto hutumia silaha ndogondogo (kama visu, na nyembe) kupora fedha au vitu mbalimbali kutoka kwa wakazi au wapiti njia. Hapa Tanzania tatizo hili linaongezeka na hata kubadilika sura, kwani kwa sasa watoto wengi wa mtaani huambatana na wazazi wao. Pengine tutaanza kubadili jina la Watoto wa Mitaani, na kuwa “Familia za Mitaani” familia hizi zinaonekana zaidi katikati majiji ya Dar es Salaam na Mwanza.

Tatizo hili sii la Tanzania peke yake, lipo nchi nyingi duniani; kwa mfano, nchini India, kunakadiriwa kuwa na watoto wa mitaani takriban milioni 20.

Picha 2.3: Watoto wa Mitaani katika moja ya miji ya India wakiwa na wazazi wao
Street Family of India II.jpg

Chanzo: street families of india - Пошук Google

Sababu zinazowasukuma watoto kwenda mitaani

Zipo sababu nyingi zinazowafanya watoto kukimbilia mitaani, na kila mtoto ana hadithi yake tofauti na ya kipekee. Sababu zinatofautiana kati ya nchi na nchi, jiji na jiji, jamii na jamii na hata mtu na mtu. Sababu mahsusi zinazowapeleka watoto mitaani ni vifo vya wazazi (kutokana na VVU/UKIMWI, na sababu nyingine), umaskini wa kaya uliokithiri, magomvi ya nyumbani, ulevi, kusambaratika kwa familia, kutelekezwa kwa watoto, malezi ya mzazi mmoja, familia zisizowajibika, kunyimwa fursa ya elimu, ukali wa wazazi, unyanyasaji wa kingono, kipigo kupita kiasi, nk.

Kwa nini Tatizo la Watoto wa Mitaani linaendelea kuwepo?

Kwa mujibu wa shirika la “ Consotium for Street Children” (Feb. 2021), Watoto wa mitaani ni mojawapo ya watu waliojificha na wasioonekana zaidi duniani.

Kuna sababu kadhaa kwa nini ni vigumu kukusanya takwimu za kuaminika kuhusu watoto wa mitaani. Hizi ni pamoja na:

- Mbinu za kitaifa za kukusanya takwimu, kama vile tafiti za kaya na sensa, hazijabadilishwa ili kunasa mtindo huu wa maisha na kujumuisha watoto wa mitaani.

- Watoto wa mitaani wanaishi maisha ya kuhamahama na ya muda mfupi, na hivyo kufanya iwe vigumu kusoma maisha yao kirahisi.

- Mara nyingi watoto wa mitaani huwa na mashaka na watu wazima, kwani wanaogopa kubaguliwa na kulipizwa kisasi.

- Uelewa mdogo wa watumishi wa ngazi mbalimbali wa serikali kuhusu sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009; na hivyo kushindwa kuwajibisha vyombo au mamlaka mbalimbali na jamii kwa ujumla kuhusu ulinzi wa mtoto.

Nini kifanyike kuondoa Tatizo la Watoto wa Mitaani?

Kuhamasisha jamii na taasisi mbalimbali kuhusu haki za watoto na wajibu wao kuzilinda.

Kuwezesha kuundwa na kufunza vikundi vya kusaidiana. Kupitia makundi haya, wataongeza kipato cha kaya na watawezeshwa kutengeneza miongozo mbalimbali ya kulinda haki za watoto.

Kuhamasisha watoto kuhusu haki na wajibu wao.

Kuboresha huduma za uzazi wa mpango.

Serikali kukaa na asasi za kiraia pamoja na wadau wengine kutathmini tatizo hili, na kutenga bajeti kila mwaka ili kupunguza, kama sii kutokomeza kabisa watoto wa mitaani.

Kuwe na sera na sheria mahsusi kutokomeza watoto wa mitaani.

Rejea
ARUSHA PRESS CLUB BLOG (Sept, 2021), Tanzania yaweka Mikakati Kukabiliana na Tatizo la Watoto wa Mitaani.

“Consortium for Street Children” (Feb. 2021), Ukweli kuhusu Watoto wa Mitaani.

Kempe Ronald Hope, Sir. (2005: “Child Survival, Poverty, and Labor in Africa”.

Unicef 2012 “Report on Cities and Children (The Challenge in Urbanization in Tanzania)”.

Upvote 14
Sidhani kama watahesabiwa!, ila serikali itafanya makadirio ambayo kimsingi sifahamu wanatumia vigezo vipi kufahamu idadi ya watoto wa mitaani.
Ndio maana kwenye makala hii, nimependekeza serikali kuandaa sera na sheria maalum kuhusu watoto wa mitaani. Hii itaibua mbinu za kuwabaini hawa watoto na kuwa na mikakati sahihi na endelevu ya kuwatoa mitaani!
 
Kwa kweli inasikitisha sana, ukatili wa walezi wa watoto na umasikini wa majumbani, unatuletea watoto wa mtaani kwa wingi. Kwanza napenda kuishauri serikali . Itengeneze taasisi yenye kupeleleza kwa kina malezi ya watoto kuzaliwa hadi mpaka kujitegemea. mlezi au mzazi, kaya iwe za kitajiri au za kimasikini. Na iwe sheria kali.
 
Kweli kabisa, ndio maana nimependekeza kuwe na sera na sheria mahsus ya watoto wa mitaani!
 
Kama hupendi dhana ya Mtoto wa Mtaani, sema neno hapa, sauti yako itasikika.
 
Sidhani kama watahesabiwa!, ila serikali itafanya makadirio ambayo kimsingi sifahamu wanatumia vigezo vipi kufahamu idadi ya watoto wa mitaani.
Sensa ya mwaka huu ilikuwa inakusanya taarifa nyingi kuhusu mtu mmojo mmoja kila familia. Hivyo sina uhakika kama watato wanaoishi mitaani wakukuwa kwenye, hesabu.
 
Naweza kusema, kwa sasa tatizo la watoto wa mitaani ni kama kipele ambacho kisipodhitiwa mapema, kitageuka kuwa jipu!
 
Serikali peke yake haitamaliza tatizo la , watoto wa mitaani, bali linaweza kudhibitiwa kuanzia ngazi ya kaya.
 
Watoto wa mitaani, ni watoto ambao wanaishi mitaani, nje ya makazi ya kawaida. Kempe Ronald Hope, (2005) anatoa maana ya Mtoto wa Mitaani kama ifuatavyo: “Mtoto wa Mtaani, ni msichana au mvulana ambaye hajafikia umri wa utu uzima, ambapo mtaa (ikijumuisha makazi yasiyokaliwa, maeneo yenye mazingira magumu, na kadhalika) umekuwa makazi, na mahali pa kujikimu kimaisha, ambaye hana ulinzi wa kutosha na ambaye haongozwi na watu wazima wenye kuwajibika”.

Kuna makundi mawili ya watoto wa mitaani: Kundi la kwanza ni lile la watoto wanaoshinda mtaani, lakini jioni au usiku wanarudi nyumbani kulala; na kundi la pili ni lile la watoto ambao wanashinda na kulala mitaani.

Tafsiri nyingine imetolewa na Marcus Lyon (2003): Kwamba, “Ni watoto wanaoishi na kulala mtaani; ambao wanafanya kazi mtaani lakini wanarudi nyumbani kwao; na wale ambao wanaishi mtaani bila kurudi nyumbani.

Watoto hawa hujishughulisha na shughuli mbalimbali ili waweze kujikimu; hizi ni pamoja na vibarua vya ujira mdogo (mfano: kubeba mizigo, kuchota maji, biashara ndogondogo, kazi za ujenzi, nk); kuombaomba na wizi/udokozi.

Ukubwa wa Tatizo la Watoto wa Mitaani
Kwa mujibu wa shirika la “Consortium for Street Children” (Feb. 2021), idadi inayonukuliwa kwa kawaida ni watoto milioni 100 wa mitaani duniani kote; hata hivyo, kutokana na ukweli kwamba makadirio haya ni ya mwaka 1989, imepitwa na wakati kwa kiasi kikubwa – takwimu za ukweli hazijulikani.

Kwa mujibu wa jarida la “Arusha Press Club, (Septemba 2021)” Tanzania inakadiriwa kuwa na watoto 35,919 wanaoishi na kufanya kazi mitaani katika majiji na miji mbalimbali, licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali pamoja na wadau wengine kutokomeza tatizo hilo.

Picha 1.1: Watoto wakiomba msaada kutoka kwa wasafiri jijini Dar es Salaam, Tanzania.
View attachment 2320998
Picha kwa hisani ya Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (DW), April 2018

Madhara ya Tatizo la Watoto wa Mitaani

- Mara nyingi watoto hupigwa na maafisa wa serikali (wakiwemo polisi)

- Wanakosa fursa ya kupata elimu na huduma za afya

- Baadhi yao hushikiliwa polisi na/au magereza bila kuzingatia haki zao

- Baadhi ya watoto hutumikishwa na watu wazima bila ujira au kwa ujira mdogo

- Baadhi ya watoto hupigwa, kuibiwa na kutumikishwa kingono na watu wazima

- Wanakabiliana na unyanyapaa na kutengwa na jamii, jambo ambalo linaathiri afya ya akili

- Baadhi ya watoto hutumbukia katika magenge ya uhalifu, kama ya madawa ya kulevya, wizi/uporaji, nk.

Picha 2.1: Watoto wakiwa wamelala barazani katika jengo la Benjamini Mkapa , jijini Dar es Salaam​

View attachment 2321004
Chanzo: Deodatus Balile/Sabahi (Septemba, 2012)

Picha 2.2: Watoto wa Mtaani wakitafuta chochote Jalalani – Kasulu mjini.​

View attachment 2321014
Chanzo: C. J. Samali (Novemba, 2012).

Ni madhila mengi yanawakumba watoto wa mitaani, hayo niliyotaja hapo ni machache kati ya mengi. Lakini kwa upande mwingine, watoto wa mitaani huchafua mazingira ya miji husika; husababisha hofu ya kuibiwa na hata kujeruhiwa kwa wakazi wa maeneo husika, kwani baadhi ya watoto hutumia silaha ndogondogo (kama visu, na nyembe) kupora fedha au vitu mbalimbali kutoka kwa wakazi au wapiti njia. Hapa Tanzania tatizo hili linaongezeka na hata kubadilika sura, kwani kwa sasa watoto wengi wa mtaani huambatana na wazazi wao. Pengine tutaanza kubadili jina la Watoto wa Mitaani, na kuwa “Familia za Mitaani” familia hizi zinaonekana zaidi katikati majiji ya Dar es Salaam na Mwanza.

Tatizo hili sii la Tanzania peke yake, lipo nchi nyingi duniani; kwa mfano, nchini India, kunakadiriwa kuwa na watoto wa mitaani takriban milioni 20.

Picha 2.3: Watoto wa Mitaani katika moja ya miji ya India wakiwa na wazazi wao
View attachment 2321015
Chanzo: street families of india - Пошук Google

Sababu zinazowasukuma watoto kwenda mitaani

Zipo sababu nyingi zinazowafanya watoto kukimbilia mitaani, na kila mtoto ana hadithi yake tofauti na ya kipekee. Sababu zinatofautiana kati ya nchi na nchi, jiji na jiji, jamii na jamii na hata mtu na mtu. Sababu mahsusi zinazowapeleka watoto mitaani ni vifo vya wazazi (kutokana na VVU/UKIMWI, na sababu nyingine), umaskini wa kaya uliokithiri, magomvi ya nyumbani, ulevi, kusambaratika kwa familia, kutelekezwa kwa watoto, malezi ya mzazi mmoja, familia zisizowajibika, kunyimwa fursa ya elimu, ukali wa wazazi, unyanyasaji wa kingono, kipigo kupita kiasi, nk.

Kwa nini Tatizo la Watoto wa Mitaani linaendelea kuwepo?

Kwa mujibu wa shirika la “ Consotium for Street Children” (Feb. 2021), Watoto wa mitaani ni mojawapo ya watu waliojificha na wasioonekana zaidi duniani.

Kuna sababu kadhaa kwa nini ni vigumu kukusanya takwimu za kuaminika kuhusu watoto wa mitaani. Hizi ni pamoja na:

- Mbinu za kitaifa za kukusanya takwimu, kama vile tafiti za kaya na sensa, hazijabadilishwa ili kunasa mtindo huu wa maisha na kujumuisha watoto wa mitaani.

- Watoto wa mitaani wanaishi maisha ya kuhamahama na ya muda mfupi, na hivyo kufanya iwe vigumu kusoma maisha yao kirahisi.

- Mara nyingi watoto wa mitaani huwa na mashaka na watu wazima, kwani wanaogopa kubaguliwa na kulipizwa kisasi.

- Uelewa mdogo wa watumishi wa ngazi mbalimbali wa serikali kuhusu sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009; na hivyo kushindwa kuwajibisha vyombo au mamlaka mbalimbali na jamii kwa ujumla kuhusu ulinzi wa mtoto.

Nini kifanyike kuondoa Tatizo la Watoto wa Mitaani?

Kuhamasisha jamii na taasisi mbalimbali kuhusu haki za watoto na wajibu wao kuzilinda.

Kuwezesha kuundwa na kufunza vikundi vya kusaidiana. Kupitia makundi haya, wataongeza kipato cha kaya na watawezeshwa kutengeneza miongozo mbalimbali ya kulinda haki za watoto.

Kuhamasisha watoto kuhusu haki na wajibu wao.

Kuboresha huduma za uzazi wa mpango.

Serikali kukaa na asasi za kiraia pamoja na wadau wengine kutathmini tatizo hili, na kutenga bajeti kila mwaka ili kupunguza, kama sii kutokomeza kabisa watoto wa mitaani.

Kuwe na sera na sheria mahsusi kutokomeza watoto wa mitaani.

Rejea
ARUSHA PRESS CLUB BLOG (Sept, 2021), Tanzania yaweka Mikakati Kukabiliana na Tatizo la Watoto wa Mitaani.

“Consortium for Street Children” (Feb. 2021), Ukweli kuhusu Watoto wa Mitaani.

Kempe Ronald Hope, Sir. (2005: “Child Survival, Poverty, and Labor in Africa”.

Unicef 2012 “Report on Cities and Children (The Challenge in Urbanization in Tanzania)”.

Hongera kwanza kwa kazi nzuri. Natumaini andiko lako litachochea mabadiliko. karibu pia kusoma andiko langu nipate maono na kura yako SoC 2022 - Kwanini Wanaume wanaongoza kwa kujiua?
Nina swali pia kuna wakati serikali ya Tanzania imejaribu kuwakusanya watoto hawa katika vituo lakini wengi wanatoroka unafikiri kuna tatizo gani hapa?
 
Back
Top Bottom