Watoto wa UVCCM watuachie chama chetu cha kutovumilia unafiki

Watoto wa UVCCM watuachie chama chetu cha kutovumilia unafiki

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Alichosema na kugusia Mwenyekiti wa CCM Mwanza ndg Diallo majuzi juu ya baadhi ya mapungufu ya utawala wa Awamu ya Tano yanaungwa mkono na sisi wapenda chama.

Chama ni mawazo ya wanachama na si mtu.

Hivyo mtu akikosea, kuchambuliwa ni lazima na ndio kukijenga chama.

Moja ya imani ya chama ni kusema kweli Daima na Fitina kuwa mwiko.

Ndg Diallo alisema kweli na bila kumung'unya maneno.

Inasikitisha kwa UVCCM kutumika kama vibaka wa kisiasa.

Ati wanamuonya Ndg Diallo ambaye kiprotokali yuko juu ya uwezo wao wa kufikiri na hata kichama.
Wanatetea mtu kuliko hoja.

Kulikuwa na mapungufu makubwa ndani ya CCM na katika Awamu ya Tano, hivi vitoto vya UVCCM vilitegemewa kama vijana kuja juu kuainisha mapungufu hayo.

Sasa vimeanza kujigeuza kuwa vimamluki vya baadhi ya watu.

Vinatakiwa vijikite katika hoja na si vinginevyo.
 
Kwa nini wewe hukumkosoa pale alipokwepa kodi ya zaid ya 2bilions? Kwa nini hukutoka na kumtaka aache ushenzi huo? Wewe nae ni hewa tu..na hatuwataki ndani ya chama..
Soma posti zangu za miaka ya nyuma.
Nimekosoa hadi wasiojulikana.
 
Kwa nini wewe hukumkosoa pale alipokwepa kodi ya zaid ya 2bilions? Kwa nini hukutoka na kumtaka aache ushenzi huo? Wewe nae ni hewa tu..na hatuwataki ndani ya chama..
Hata sasa najua ulishatoa mapendekezo ambambikiwe ya 20b,kwani hata ile ya 2b ni mbinu chafu za kuwanyamazisha wenye maono na mawazo mbadala.
 
Ninyi ndio vitoto vya juzi msio na nidhamu.
Mnabwekea hata wakubwa wenu hata bila kujua mnabwekea nini, alimradi mmetumwa.
Kujiunga CCM kwa kadi ya namba moja, haina maana una uchungu zaidi na tz.

unawezakuwa bado mbuzi tu.
 
Hata sasa najua ulishatoa mapendekezo ambambikiwe ya 20b, kwani hata ile ya 2b ni mbinu chafu za kuwanyamazisha wenye maono na mawazo mbadala.
Kijana kwa nini unakuwa na fikra finyu kiasi hicho? Kwanini unaamni kaonewa wakat ile ni taasisi ya kukusanya mapato? Hujui kuwa kuna watu walikuwa wakwepa kodi wakubwaa..umemsahau nimrodi mkono?

Jinsi alivyofungiwa ofisi yake kisa halipi kodi? Ifike sehem waafrica waache ushabiki kwa mtu binafsi, tazama south africa walivyo wajinga, yaan mtu anaharibu mali za wengine kushabikia zuma alieiba pesa za uma na hata hawakuzipata.

Watu weusi wana laana ya ajabu sana..sijui shida iko wapi.
 
Alichosema na kugusia Mwenyekiti wa CCM Mwanza ndg Diallo majuzi juu ya baadhi ya mapungufu ya utawala wa Awamu ya Tano yanaungwa mkono na sisi wapenda chama...
Hivyo vitoto vinataka vijipambanue kuwa vidume, kumbe ni vindama tu vinavyonya na kuelekezwa na wanaowapa maziwa na kuwaelekeza cha kufanya.
 
Kijana kwa nini unakuwa na fikra finyu kiasi hicho? Kwa nini unaamni kaonewa wakat ile ni taasisi ya kukusanya mapato? Hujui kuwa kuna watu walikuwa wakwepa kodi wakubwaa..umemsahau nimrodi mkono?

Jinsi alivyofungiwa ofisi yake kisa halipi kodi? Ifike sehem waafrica waache ushabiki kwa mtu binafsi..tazama south africa walivyo wajinga..yaan mtu anaharibu mali za wengine kushabikia zuma alieiba pesa za uma na hata hawakuzipata.

watu weusi wana laana ya ajabu sana..sijui shida iko wapi.
Yeyote hupoteza uhalali hata wa yaliyo mema kutokana na matendo yake,kama uneweza kuwabambikia wawili,je watano wanaoshahili,wasio onewa unawezaje kuwatambulisha kwetu tukakuelewa.
 
Kijana kwa nini unakuwa na fikra finyu kiasi hicho? Kwanini unaamni kaonewa wakat ile ni taasisi ya kukusanya mapato? Hujui kuwa kuna watu walikuwa wakwepa kodi wakubwaa..umemsahau nimrodi mkono?

Jinsi alivyofungiwa ofisi yake kisa halipi kodi? Ifike sehem waafrica waache ushabiki kwa mtu binafsi, tazama south africa walivyo wajinga, yaan mtu anaharibu mali za wengine kushabikia zuma alieiba pesa za uma na hata hawakuzipata.

Watu weusi wana laana ya ajabu sana..sijui shida iko wapi.
Uliye na laana ni wewe mwenyewe usiye jua maovu na mema ya dunia.

Mtu anateka, anabambika kesi, ananyang'anya, watu wanapotea na kukutwa wamekufa vifo vya utatanishi, kwa nini wasisemwe?

Ustaarabu wa kisiasa ni kukubali kukosolewa, na mtu mwenye akili timamu ni kujisahihisha kama alivyosema Mwalimu.

Diallo is right.
 
Alichosema na kugusia Mwenyekiti wa CCM Mwanza ndg Diallo majuzi juu ya baadhi ya mapungufu ya utawala wa Awamu ya Tano yanaungwa mkono na sisi wapenda chama.

Chama ni mawazo ya wanachama na si mtu.

Hivyo mtu akikosea, kuchambuliwa ni lazima na ndio kukijenga chama.

Moja ya imani ya chama ni kusema kweli Daima na Fitina kuwa mwiko.

Ndg Diallo alisema kweli na bila kumung'unya maneno.

Inasikitisha kwa UVCCM kutumika kama vibaka wa kisiasa.

Ati wanamuonya Ndg Diallo ambaye kiprotokali yuko juu ya uwezo wao wa kufikiri na hata kichama.
Wanatetea mtu kuliko hoja.

Kulikuwa na mapungufu makubwa ndani ya CCM na katika Awamu ya Tano, hivi vitoto vya UVCCM vilitegemewa kama vijana kuja juu kuainisha mapungufu hayo.

Sasa vimeanza kujigeuza kuwa vimamluki vya baadhi ya watu.

Vinatakiwa vijikite katika hoja na si vinginevyo.
Kimeumana 😃
 
Back
Top Bottom