Watoto wa Wasira waliojiunga CHADEMA watoa ufafanuzi juu ya uhusiano wao na Waziri Wasira

Nilidhani wanasura kama Tyson ningeenda mahakamani kupinga! Kumbe siyo hivyo sasa hakuna kurudi nyuma mbele DAIMA HAKUNA CHA NEC WALA NINI wasubiri 2015 nitakuwa kijijini kwetu kuhamasisha nakuelimisha CCM wasichagulike maana ni WIZI MTUPU!!!!
 
Hapana tuwe wazi na wa kweli... Nadhani tatizo sio habari tu, tatizo lipo kwa waandishi, wana CCM na wana CDM wenyewe.

Habari ya mabinti wawili kupata card mpya ya CDM alafu tena wamekabidhiwa hizo card na Slaa, unadhani itaacha kutengeneza headlines na hali ni wazi hivyo vyama pinzani kubwa?
Siku si nyingi tutajua rangi yako halisi...hiyo ndiyo CDM usipoikubali mdomoni utaikubali moyoni
 
Hakika hawa watoto ni vichwa kweli kweli. Umeona walivuopangua hoja wamefanya "defend without offending" excellent! Wasira uko wapi umewaona watoto hao? Hawajatukana wala kukashfu kama wewe!! Very shame!
 
Nimeipenda hiyo "defend without offending"
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UFAFANUZI KUHUSU SISI KUJIUNGA NA CHADEMA NA MALUMBANO KUHUSU MAJINA YETU

Tarehe 30/09/2012 mimi Esther Wasira na dada yangu Lilian Wasira tulijiunga na CHADEMA na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Dr Willibrod Slaa.

Tulielezea kwa kirefu sababu za sisi kujiunga
CHADEMA na tukasisitiza kuwa tumeridhika kuwa CHADEMA ni chama chenye dhamira safi ya kuiongoza Tanzania na kwamba ni chama kinacholeta matumaini mapya ya kuijenga Tanzania mpya yenye neema.

Waandishi wa habari walijaribu sana kutudodosa kujua tuna uhusiano gani na Waziri Steven Wasira. Tulielezea wazi kuwa mahusiano yetu ya kifamilia hayahusiki na sababu na dhamira yetu ya kujiunga CHADEMA. Hata hivyo tulielezea kuwa Waziri Steven Wasira ni baba yetu mdogo ambaye alinyang'anyana ziwa na baba yetu mzazi, wakili George Wasira. Tulidhani hiyo ilitosha na lisingekuwa swala tena la kujadili na badala yake hoja ya kujadiliwa ingeweza kuwa sababu tulizozieleza za kujiunga CHADEMA.

Tunasikitishwa sana na malumbano yaliyofuata baada ya hapo kuhusu kama sisi ni watoto wa Wasira au la. Kama tulivyoeleza, tumejiunga CHADEMA kwa sababu tulizozieleza hapo awali na wala si kwa sababu nyingine yeyote. Hatujajiunga CHADEMA kumdhalilisha mtu, kumfedhehesha mtu au kukipatia umaarufu CHADEMA kwa vile tu tunatumia jina la Wasira.

CHADEMA ni chama cha siasa tena chenye wanachama na wafuasi wengi Tanzania hivyo si kashfa bali ni fahari kubwa mtu kujiunga CHADEMA na tena ni ushahidi wa mtu kujitambua. Pia CHADEMA ni Chama maarufu sana Tanzania kwa sasa hata pengine ni maarufu kuliko CCM hivyo hakihitaji kujipatia umaarufu kwa mgongo wetu.

Sisi tunawaheshimu sana wazee wetu na tutaendelea kuwaheshimu ila linapokuja swala la chama cha kujiunga linabaki kuwa hiari yetu kwa kuzingatia sera za chama na uwezo wa chama husika katika kujenga Tanzania tunayoitaka na hilo ndilo lililotupeleka CHADEMA. Na hii ni haki yetu ya msingi kabisa inayolindwa na Katiba ya nchi hii chini ya ibara ya 20(1).

Ikumbukwe kuwa mmoja wa Waanzilishi wa CHADEMA ni Mzee Wasira. Dhamira ya kuanzisha CHADEMA ilikuwa ni kushika dola na hili ndilo CHADEMA imekuwa siku zote inajaribu kuwashawishi Watanzania kuwa sasa wamekomaa na wanastahili kuchukua dola. Kwa vile kuchukua dola ilikuwa ndio ndoto ya baba yetu mzazi Mwanzilishi wa CHADEMA, sisi kama watoto tumejiunga na M4C ya CHADEMA ili tuweze kutimiza ndoto ya baba yetu kuwa CHADEMA siku moja ichukue jukumu la kuiongoza Tanzania.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Lilian Wasira 0719 604156
Esther Wasira 0655 048797

huu ujumbe uliosemwa hapo umenipa raha sana!
 
Kumbe sio watoto wa Wasira bana.

wasira ni jina la ukoo na si miliki ya stephen. nimesikitishwa sana na kauli ya kiongozi msomi wa kiwango cha juu na umri wake kukana watoto wa kaka yake kuwa si wa kwake hali akijua ni kinyume na tamaduni zetu za kiafrica Hili linakaribisha UBAGUZI usio na maana katika ukoo wao. S. wasira ajaribu kuvuta kumbukumbu ya mambo yaliyomtokea benjamini mkapa aliposimama majukwaani Arumeru mashariki kumdhihaki vincent nyarere kuwa si mtoto wa mwl Nyerere. mkapa anakumbuka kilichotokea. wasira hakutumia busara kuendeleza mjadala kwenye vyombo vya habari kwani umewaongezea credit wapinzani wake katka siasa ( chadema ) na kukipunguzia hadhi ccm kwa upande mwingine. namshauri wasira ambaye ni mwanachma wa zamani wa NCCR Mageuzi kuwa mpole wakati huu M4C inapoendeleza vuguvugu la kuwavuna watoto wa viongozi wa ccm waliojitambua. 2015 wasira atabaki peke yake na kadi yake ya ccm.
 
Safi sana hawa watoto wanaonekana ni vipanga sana na ni wafuasi halisi wa Chadema

Kuna test imefanywa kuleta haya matokeo ya UKIPANGA???? Au kwa kutoa TAMKO LAO KWA WAANDISHI WA HABARI =Ukipanga??? Nilikuwa natafakari kwa sauti tuuu......
 
Hahahaaaaa, mkuu umenivunja mbavu ulipoendelea kuwaita WATOTO WA WASIRA, licha ya 'PET' kukataa, hakyamungu safari hii Wasira atatapika usingizini!

UFAFANUZI KUHUSU SISI KUJIUNGA NA CHADEMA NA MALUMBANO KUHUSU MAJINA YETU[/FONT][/SIZE]
[/COLOR][/CENTER]

Tarehe 30/09/2012 mimi Esther Wasira na dada yangu Lilian Wasira tulijiunga na CHADEMA na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Dr Willibrod Slaa.

Tulielezea kwa kirefu sababu za sisi kujiunga
CHADEMA na tukasisitiza kuwa tumeridhika kuwa CHADEMA ni chama chenye dhamira safi ya kuiongoza Tanzania na kwamba ni chama kinacholeta matumaini mapya ya kuijenga Tanzania mpya yenye neema.

Waandishi wa habari walijaribu sana kutudodosa kujua tuna uhusiano gani na Waziri Steven Wasira. Tulielezea wazi kuwa mahusiano yetu ya kifamilia hayahusiki na sababu na dhamira yetu ya kujiunga CHADEMA. Hata hivyo tulielezea kuwa Waziri Steven Wasira ni baba yetu mdogo ambaye alinyang'anyana ziwa na baba yetu mzazi, wakili George Wasira. Tulidhani hiyo ilitosha na lisingekuwa swala tena la kujadili na badala yake hoja ya kujadiliwa ingeweza kuwa sababu tulizozieleza za kujiunga CHADEMA.

Tunasikitishwa sana na malumbano yaliyofuata baada ya hapo kuhusu kama sisi ni watoto wa Wasira au la. Kama tulivyoeleza, tumejiunga CHADEMA kwa sababu tulizozieleza hapo awali na wala si kwa sababu nyingine yeyote. Hatujajiunga CHADEMA kumdhalilisha mtu, kumfedhehesha mtu au kukipatia umaarufu CHADEMA kwa vile tu tunatumia jina la Wasira.

CHADEMA ni chama cha siasa tena chenye wanachama na wafuasi wengi Tanzania hivyo si kashfa bali ni fahari kubwa mtu kujiunga CHADEMA na tena ni ushahidi wa mtu kujitambua. Pia CHADEMA ni Chama maarufu sana Tanzania kwa sasa hata pengine ni maarufu kuliko CCM hivyo hakihitaji kujipatia umaarufu kwa mgongo wetu.

Sisi tunawaheshimu sana wazee wetu na tutaendelea kuwaheshimu ila linapokuja swala la chama cha kujiunga linabaki kuwa hiari yetu kwa kuzingatia sera za chama na uwezo wa chama husika katika kujenga Tanzania tunayoitaka na hilo ndilo lililotupeleka CHADEMA. Na hii ni haki yetu ya msingi kabisa inayolindwa na Katiba ya nchi hii chini ya ibara ya 20(1).

Ikumbukwe kuwa mmoja wa Waanzilishi wa CHADEMA ni Mzee Wasira. Dhamira ya kuanzisha CHADEMA ilikuwa ni kushika dola na hili ndilo CHADEMA imekuwa siku zote inajaribu kuwashawishi Watanzania kuwa sasa wamekomaa na wanastahili kuchukua dola. Kwa vile kuchukua dola ilikuwa ndio ndoto ya baba yetu mzazi Mwanzilishi wa CHADEMA, sisi kama watoto tumejiunga na M4C ya CHADEMA ili tuweze kutimiza ndoto ya baba yetu kuwa CHADEMA siku moja ichukue jukumu la kuiongoza Tanzania.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Lilian Wasira 0719 604156
Esther Wasira 0655 048797

[/QUOTE]
 
Kuna test imefanywa kuleta haya matokeo ya UKIPANGA???? Au kwa kutoa TAMKO LAO KWA WAANDISHI WA HABARI =Ukipanga??? Nilikuwa natafakari kwa sauti tuuu......
Taarifa yao tu inaonyesha wazi kuwa ni vipanga ile mbayaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
3.jpg

ahsante kwa kwenda beyond the margin.
Ngoja wadau wamchangamkie kumpa compan.
Mtoto mzuri na atakuwa turufu ya chadema.

hongera dada! sura yako kama ya waziri, naona CDM ikichuka dola na wewe utakua waziri! tehe tehe teheeeee!
 
kwani baba yako mdogo wewe anakuita nani kama sio mtoto wake?wangejiunga chichiem angewapongeza na kuwatangaza kuingia chadema sio watoto wake!hii ndio dhana ukiwa chichiem msafi ukiwa CDM hufai kuwa kiongozi ha ha ha wanalo hilo 2015
 
Yaleyale ya mkapa na mtoto wa nyerere ARUMERU or Eti oh sio ukoo wa nyerere mara sio mtoto wa nyerere JK,siasa ndivyo ilivyo
 
Back
Top Bottom