Watoto wakutwa wakisafiri chini ya basi kutoka Bukoba - Mwanza

Mbona kawaida tu hao ni mabaharia storaway hadi Dar wanakuja wengi sana KWA njia hii.
Muhimu ni ukaguzi kabla bus halijaondoka. Ni hatari sana bus likipiga kwenye bumps lazima asagwe na tairi akikaa vibaya
 
Hawa ni makomandoo! Serikali inasubiri nini isiwapokee kwenye Jeshi la Wananchi na kuwapa mafunzo zaidi? Mtu unasafiri kilometer 200 chini ya basi linakwenda 120km/h umejishika na springi utashindwa nini vitani?
200 chache hizo yaani dar moro.
Wapo ukaa uvunguni masaa 14 yaani Mwanza dar km 1200.
 
Nchi yetu ina baadhi ya madereva na makondakta wasio jua wajibu wao 😃unakuta basi lina makondakta wanne au wa tatu lakina wote wameshindwa kujua kama kuna abiria wameingia kimagendo✅✅
kama watu wanaweza kujibanza hata kwenye ndege, basi ni kitu gani mkuu? kuna kitu natafakari lakini sipati majibu, kule chini kuna mahali wanalala, wanakaa au wanakuwa wananing'inia...?
 
Waheshimu sana watoto wa mtaani sana si kidogo .

Wana ushirikiano sana na wakiamua jambo hawawazi kifo wala nini

Ukitaka kujua how serious they are jaribu siku moja kuingilia harakati zao utakuja kusimulia ikiwa utaachwa hai
 
kama watu wanaweza kujibanza hata kwenye ndege,basi ni kitu gani mkuu?kuna kitu natafakari lakini sipati majibu,kule chini kuna mahali wanalala,wanakaa au wanakuwa wananing'inia...?

duuu viongoz hawpo makinii kbisa yaan unakuta wanpigq kelele kujaza abiria lakin akikutwna na gari abiri wapo nyomi [emoji14]analamba chake ana pita hivii
 
Hawa ni makomandoo! Serikali inasubiri nini isiwapokee kwenye Jeshi la Wananchi na kuwapa mafunzo zaidi? Mtu unasafiri kilometer 200 chini ya basi linakwenda 120km/h umejishika na springi utashindwa nini vitani?
Wapi umeona jeshi laajiri watoto au fundisha watoto?
 
Hawa ndo wanatakiwa wapelekwe JKT na polisi, na JWTZ Wana roho ngumu
 
Abiria huingia nani ya bus hawa walikuwa nje chini ya chassis. Hata kama ungekuwa ungedhania Vipi mtu kujibanza huko?

unajua hili swala bhna hawa majangi wanashida yakufika sehem flan kumwelekeza konda itakuwa kipengele wakaona njia rahisi nikujichimbia mahali kosa lipo kwa makondakta wanakuwaga sio waelewaaa kabisaa na ni wakorofiii
 
Hawa ni makomandoo! Serikali inasubiri nini isiwapokee kwenye Jeshi la Wananchi na kuwapa mafunzo zaidi? Mtu unasafiri kilometer 200 chini ya basi linakwenda 120km/h umejishika na springi utashindwa nini vitani?
Naunga mkono! kama aliyeokoa watu aliingizwa jeshini hawa pia waingizwe wanaweza kufanya yasiyofikirika wakipata training jeshini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…