WATOTO WANAOFANYIWA UKATILI, JE WANAPATA MSAADA ILI WAPONE?

WATOTO WANAOFANYIWA UKATILI, JE WANAPATA MSAADA ILI WAPONE?

Strong ladg

Senior Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
170
Reaction score
445
Jiulize mtoto
1. Aliyebakwa
2. Aliyelawitiwa
3.Aliyetelekezwa na wazazi
4. Aliyekataliwa
5. Aliyeshuhudia baba akimpiga mama.
6. Aliyeshuhudia mama akimpiga baba
7. Aliyeshuhudia baba na mamá wakipigana
8. Aliyeshuhudia baba na mamá wakitukanana,kutoleana maneno machafu n.k
9. Aliyeshuhudia baba akimsaliti mama live
10 . Aliyeshuhudia mama akibadilisha wanaume kama nguo
11. Aliyepigwa kupitiliza,kunyimwa chakula,aliyetukanwa matusi yote,aliyeambiwa yéyé ni bure,sifuri tu, mbona sio kama dada yake, mbona hafaulu kama kaka yake
12. Aliyemsikia mchepuko wa baba akimtukana mama n.k
Je nani anampa msaada,nani anamfariji,nani anampa matibabu ili akili Ikae sawa?
Cha kushangaza na kusikitisha asilimia kubwa ya watoto hawa hawapati msaada, hawaponi,wanalazimika kukaa na majeraha na vidonda mioyoni mwao. Lakini watakapokuwa watu wazima na kufanya matukio ya ajabu kutokana na hasira na uchungu walioubeba, tuko mbiombio kuwahukumu,kuwasimanga,kuwanyooshea vidole n.k Lakini walipohitaji faraja ,walipohitaji msaada hatukuwepo. Je watapataje kupona?
 
Back
Top Bottom