Jackpiano
JF-Expert Member
- Apr 19, 2025
- 560
- 756
Watoto wanatumikishwa kama watumwa mijini – Je, wazazi wao wako wapi?
Familia moja imeleta binti mdogo sana kutoka kijijini – ukimuona tu, ni wa darasa la tano au sita hivi. Huyu dogo ndio “mfanyakazi wa ndani” wao, ambaye wameleta ili aje kumsimamia mtoto wao wa miaka kama 4. Mpaka sasa hata huyo mtoto bado hajaletwa baada ya mtu alie kua anakaa nae uyo mtoto kuondoka na kumpeleka kwa ndugu zao– lakini kazi zote za ndani anapewa huyu binti.
Hana uelewa, hawezi kusoma wala kuandika, hawezi hata kuwasha TV. Mara nyingi hukaa mwenyewe nyumbani siku nzima. Jana jioni wenye nyumba walirudi wakagonga sana mlango – kumbe dogo amelala kwa uchovu, hadi akasahau kufungua. Kelele nyingi ndo zikamwamsha.
Hii inaumiza sana. Mtoto ananyimwa haki yake ya msingi: kusoma, kucheza, kupumzika. Badala yake, ananyanyasika kwa kazi ngumu ambazo si za umri wake. Na bado jamii inaita hii “ajira ya ndani”?
Sasa swali langu ni moja:
Wazazi wa hawa watoto wako wapi?
Wanajua wanawatuma watoto wao kwenda kutumikishwa? Au wananunuliwa kwa ahadi ya “ataenda shule” na “atapewa maisha mazuri”?
Je, ni sahihi kwa familia za mjini kutumia watoto wadogo kama watumwa wa kisasa?
Wana JF tusaidiane kuelimisha jamii – huu ni ukatili au tumekuwa vipofu?
Nimeumia sana moyoni baada ya kuona hali ya mtoto mmoja jirani hapa.Wadau poleni na mihangaiko.