Nimeumia sana moyoni baada ya kuona hali ya mtoto mmoja jirani hapa.Wadau poleni na mihangaiko.
Hii sio ishu ya siasa wala jinsia. Hili ni suala la ubinadamu na haki za mtoto.WAZAZI NA MACHAWA MJINI WAZAZI WA MAMA.
Inasikitisha sana!
Hujui tofauti ya ukatili na uangalizi, alafu bado unatumia data zako kuandika pumba kwenye mada ya haki za watoto? Acha kutumia keyboard kama roho yako ilivyojaa giza.Acha mdomo, umejuaje ananyanyasika ??
UnAjua makubaliano ya bint na wazazi ? Kama walimuahidi baada ya kipindi fulani watamuendeleza ??
Majirani wapuuz wapuuz kama nyie mnatakiwa mpigwe chuma
Huku Ustawi wa jamii wako busy kufarakanisha ndoa ili waje kupata 30%ya malipo ya wanaume kwa wake wanao ishi na watoto zaoWatoto wanatumikishwa kama watumwa mijini – Je, wazazi wao wako wapi?
Nimeumia sana moyoni baada ya kuona hali ya mtoto mmoja jirani hapa.
Familia moja imeleta binti mdogo sana kutoka kijijini – ukimuona tu, ni wa darasa la tano au sita hivi. Huyu dogo ndio “mfanyakazi wa ndani” wao, ambaye wameleta ili aje kumsimamia mtoto wao wa miaka kama 4. Mpaka sasa hata huyo mtoto bado hajaletwa baada ya mtu alie kua anakaa nae uyo mtoto kuondoka na kumpeleka kwa ndugu zao– lakini kazi zote za ndani anapewa huyu binti.
Hana uelewa, hawezi kusoma wala kuandika, hawezi hata kuwasha TV. Mara nyingi hukaa mwenyewe nyumbani siku nzima. Jana jioni wenye nyumba walirudi wakagonga sana mlango – kumbe dogo amelala kwa uchovu, hadi akasahau kufungua. Kelele nyingi ndo zikamwamsha.
Hii inaumiza sana. Mtoto ananyimwa haki yake ya msingi: kusoma, kucheza, kupumzika. Badala yake, ananyanyasika kwa kazi ngumu ambazo si za umri wake. Na bado jamii inaita hii “ajira ya ndani”?
Sasa swali langu ni moja:
Wazazi wa hawa watoto wako wapi?
Wanajua wanawatuma watoto wao kwenda kutumikishwa? Au wananunuliwa kwa ahadi ya “ataenda shule” na “atapewa maisha mazuri”?
Je, ni sahihi kwa familia za mjini kutumia watoto wadogo kama watumwa wa kisasa?
Wana JF tusaidiane kuelimisha jamii – huu ni ukatili au tumekuwa vipofu?
Leo tukifumbia macho ukatili dhidi ya mtoto kwa visingizio vya "30% ya ndoa" — kesho tutatengeneza kizazi kilichojaa hasira na chuki.Huku Ustawi wa jamii wako busy kufarakanisha ndoa ili waje kupata 30%ya malipo ya wanaume kwa wake wanao ishi na watoto zao
Haki gani mpumbavu wewe, mambo ya familia ya mtu ndani unayajuaje ? Kama yanajulikana si kuna uongozi wa mtaa? Yani niheshimike na mjinga mjinga kama wewe una mavi kichwani ??Hujui tofauti ya ukatili na uangalizi, alafu bado unatumia data zako kuandika pumba kwenye mada ya haki za watoto? Acha kutumia keyboard kama roho yako ilivyojaa giza.
Unalinda ukatili kwa makengeza ya kihisia, halafu unataka kuheshimika kwa kejeli zako za mtaani.
Pole sana, utu haupatikani kwa matusi — unapatikana kwa akili.
Ujinga siyo kutokujua — ni kujua kidogo halafu ukadhani unajua yote.Haki gani mpumbavu wewe, mambo ya familia ya mtu ndani unayajuaje ? Kama yanajulikana si kuna uongozi wa mtaa? Yani niheshimike na mjinga mjinga kama wewe una mavi kichwani ??
Hali ngumu ya maisha haipaswi kugeuzwa leseni ya kuuza utu wa mtoto.Tunazaa watoto, kisha wanalelewa na mzazi mmoja kwenye hali ngumu ya maisha.
Matokeo yake mzazi/mlezi anaamua kumuuza mwanae mjini angalau awe anapewa 50K kila mwezi.
Chanzo cha yote ni hali ngumu za maisha.
Mtoto kuacha shule si tiketi ya utumwa wa kazi za ndani.Almost ni wale watoto wasio soma, aidha waliacha shule kwa sababu kadha wa kadha, hivyo kuepuka kukaa home au kuzurura mtaani 4 nothing, heri watafute kipato kupitia u housemaid.
Mtoto kuacha shule si tiketi ya utumwa wa kazi za ndani.
Heri afanye kazi kuliko kuzurura si suluhisho ni kisingizio cha jamii iliyokataa kuwajibika.
Tunapowazoesha mateso mapema tusishangae wakikua na mioyo migumu.
Hali ngumu ya maisha haipaswi kugeuzwa leseni ya kuuza utu wa mtoto.
Kama mzazi anahitaji pesa, kuna njia nyingi — lakini kumtoa mtoto kama suluhisho ni kuua kizazi kwa mikono yako mwenyewe.
Mtoto si mradi wa kipato. Kama 50K inampitia kila mwezi lakini ananyimwa haki ya kucheza, kusoma, kupendwa — basi hiyo ni biashara ya kiharamia, si malezi.
Umaskini si dhambi — ila kulazimisha mtoto kuubeba ni dhuluma isiyosameheka.