Chiwa
JF-Expert Member
- Apr 17, 2008
- 4,116
- 4,979
Ni mchezo wa kitoto unanikumbusha mbali sana. kwa wale tuliosoma pwani vijijini tukisomea mtini madarasa hayapo mlango na dirisha vyote sawa lakini bado tulikuwa na adabu ya kuomba ruhusa kwa mwalimu.
Najaribu kuangalia kizazi kilicholelewa kwauadilifu mkubwa leo hii kikiongoza kwa kutenda uarifu mkubwa tena kwa vizazi bila huruma kwa kivuli za uwekezaji.
Tuliendesha bandari wakati ule tukiwa hatuna wasomi lakini ilikuwa yetu na tukiongoza vizuri kwa kusafirisha mkonge.
Hatukuwa na watumiaji wengi wa umeme lakini TANESCO ya marehemu Mosha ilitulia huyu jamaa sikuwahi kuona hata sura yake lakini pamoja na udogo wangu aliweza kunijengea ushawishi kuwa shirika linafanya vizuri.
Najaribu kuwaza hivi kweli nchi bado haina vijana wasomi wanaoweza kujiunga tukawapa mafunzo na kuwajenga katika uadirifu wakasimamia bandari? kweli ? mpaka hawa waarabu ndo watutawale tena?
Hapa nashindwa kukubaliana na ninyi hapa nipigeni mnavyoweza lakini nafsi yangu itabaki kuamini chini ya kapeti hakuna maslahi mapana ya Taifa bali maslahi binafsi kwa kuwaangamiza wengine.
Bora lingekuwa tunda la lawe mwenyetunda aliamua kulitoa sadaka kwa atakayepata na kukosa asimlaumu kwa kuwa hana ya kuwatosheleza bora alirushe kisha wagombanie na yeye hana lawama na kila mshiriki anaingia akitarajia kupata na si kukosa lakini akikosa hana kinyongo. ila kwa hili toka mwanzo tumecheza huku tukiwa na uhakika tumepoteza.!
Ni sawa na mimba ya panya anajifungua paka kisha mama mtu analiwa (kama chakula tafadhari) na mwanawe na kumwacha mtoto yatima! mtoto kila akiwakimbilia ndugu zake panya ili wamsaidie wao wanamkimbia ndivyo ilivyo.
Tuko tayari nchi ipate ipate 17%(mfano tafadhari) wewe upate 3% na hao wawekezaji wapate 80% kweli? halafu hizi fedha za rushwa zitakusaidia nini ikiwa watanganyika wengi wamekufa kwa njaa, maradhi na ujinga kwakuwa hapakuwepo fedha za kutosha kufadhiri huduma zao.
Naamini ipo siku kitakuja kizazi hakitakubali na tanganyika itawaka na hili litatokea kabla hatujafa wakidai vya kwao.
Maisha ni magumu sana na wanaoumia ni vijana tena wamo wengi walioenda shule wamebaki kufanya umalaya ili waishi kweli?
Wacha tusubiri itafika sehemu mama ataamua liwalo na liwe vukeni kumkabili simba siwezi tena.