Watoto wangu wote hufariki baada ya kuzaliwa au mimba kuharibika

Hilo ni likango, linamaliza watoto wote, yaan na ikikomaa haitibiki mkeo anakufa na mimba. Au wakati wa kujifungua.

Aseeeeh poleeee sanaaa.
asante mkuu,lakini nimefuatilia hii kitu ipo kwenye ukoo wetu kuanzia babu,baba,kaka,dada na mimi pia ila wenzangu wote walifanikiwa kua na familia kwangu mm imekua changamoto
 
kwahiyo mkuu wazazi wangu hawataki niwe na familia?
 
Kwa upande wangu m naona uende kwa nabii anitwa Suguye au kwa Mwamposa haya mambo kwao n madogo sana mwnyezi Mungu anawatumia ipasavyo
nimeshakwenda mkuu na nina imani yote ila bado bilabila
 
Kapime damu zenu wewe na mke wako, kuna rafiki yangu alikuwa na case kama yako........ila alioa mke mwingine na watoto wanakua vizuri.....na mkewe anazaa vizuri alikoolewa..... Ilikuwa rahisi kuachana cos ni Muslims
 
Kaka pole kwa unayoyapitiaa, huko nyuma hukuwahi kuuumiza moyo wa bidada yeyote aliyekupenda sana ukaja kumuacha bila sababu??

#Tumaini la mwisho ni kwa Mungu tu.
Hapana mkuu hua sifikii hatua hiyo nikiona hatuwezani najitoa mapema
 
asante mkuu,lakini nimefuatilia hii kitu ipo kwenye ukoo wetu kuanzia babu,baba,kaka,dada na mimi pia ila wenzangu wote walifanikiwa kua na familia kwangu mm imekua changamoto
Kheeeeh poleeeh sanaaa, ndo uwahi kwa mtaalamu ukapate tiba, nawe uitwe baba km matakwa yako.
 
Kwa uzoefu wangu hiyo ni shida ya kiimani zaidi,kuna watu nishakutana nao wana shida kama hii ni mpaka pale walipofanya taratibu/matambiko ndipo mambo yalipokua sawa.
 
Ushauri wangu ni huu oa ndio uzae fullstop
 
Kapime damu zenu wewe na mke wako, kuna rafiki yangu alikuwa na case kama yako........ila alioa mke mwingine na watoto wanakua vizuri.....na mkewe anazaa vizuri alikoolewa..... Ilikuwa rahisi kuachana cos ni Muslims
ikiwa tofauti kuachana nae ni changamoto mkuu maana nimedate na wasichana 50+ sijaona faida yoyote zaidi ya kujilaumu tu baada ya kumaliza tendo..saiz nataka nitulie nae huyu kwanza nione mwisho wake
 
Sawa Dr. Mandingo... PDX Bawasiri....

Prognosis ikoje Boss

Sent from my Nokia 1 using JamiiForums mobile app
 
Nilikuwa na ubongo mgumu Sana ila ilinibidi nielewe.
Vifo vya watoto na Mimba kuharibika ni mikono ya watu.
Wanga wanaopoa na kuwala. Vichanga.😔😔
 
Hao wanawake wote uliwaoa?? Au ulikuwa unaZini tu?

Tubu kwa ajili ya uzinzi huu, muombe Mungu aanze na wewe kwa upya. Halafu oa mke wako, mwambie Mungu akupe watoto kupitia huyo mkeo. Kataa roho ya mauti juu ya uzao wako, jitenge mbali na maagano yote waliyofanya wazee au uliyofanya wewe. ANZA UPYA NA MUNGU, ATAKUTENDEA MAKUU
 
mkuu kama hautojali waweza elezea zaidi juu ya hilo na tiba yake....
 
Nimesoma ushauri nimegundua wengi bado wana imani za kichawi na ushirikina na hapo hapo wana imani za Dini za ma beberu

Nenda hospital pima Rhesus factor ujue kama inaendana kati yako wewe na Mwanamke utakaembebesha mimba,


Hakuna uchawi wala ushirikina, pima RH kuna sindano mama mjamzito ataandikiwa kuchomwa kila akiwa na ujauzito kusudi Zygote asifie tumboni au mtoto asifariki baada ya kuzaliwa
 
Pole mkuu... Jitahid kusali
 
Hiyo likango ni hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…