Watoto wapiga dufu kuomba ovyo kipindi cha mwezi Ramadan ni utamaduni wa ovyo

Watoto wapiga dufu kuomba ovyo kipindi cha mwezi Ramadan ni utamaduni wa ovyo

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Kuna utamaduni umekuwepo wa kuwatumia watoto kuomba omba na vigoma vyao hasa katika mwezi Ramadhani

Huu ni udhalilishaji wa watoto wadogo na kuwajengea fikra duni za kuomba omba

Dr Gwajima Toka ofsini wasaidie hawa Watoto wanaomba omba waende shule wapate maarifa yake kuwafata baadaye kwenye maisha Yao

Kumjengea mtoto kuomba omba ni kumrithisha umasikini hakuna mtu atakuwa tajiri Kwa kuomba

Inafaa viongozi wa dini na madrasa wawafundishe watoto stadium za maisha na kujitegemea sio kuomba misaada

Nimeshangaa wamepiga vigoma vyao na filimbi nikatoka nje kuuliza kulikoni wakasema wanaomba, nikawambia me sio wa dini yenu, wakaomba sana nikawapa sh 2000

Hawa Watoto aliyewapa jukumu la kuomba omba, na wakiomba pesa wanapeleka wapi?
Wanaomba Kwa ajili ya Nini?
Au ni kama fashion tu
 
Back
Top Bottom