NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,402
- 4,532
Watoto watelekezwa na wazazi wao Morogoro, DC atoa maagizo
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, Ngollo Malenya, ameagiza kukamatwa kwa wazazi wawili, Thomas Ulanda na Adelyda Nakashawa kwa kuwatelekeza watoto watatu huku mmoja anayesoma kidato cha nne akiwa ndiye anayewahudumia wenzake.
Watoto hao wakazi wa Kijiji cha Gombe, mkoani Morogoro, walitelekezwa na wazazi wao wanaodaiwa kuachana na mwanamke akaolewa na mwanaume mwingine.
Mkuu huyo wa wilaya leo Alhamisi, Julai 21, 2022 ametembelea nyumbani kwa watoto hao na kuvielekeza vyombo vya dola kuwasaka wazazi hao.
Chanzo: Mwananchi
“Wazazi hao waliachana, mwanamke akaolewa na mwanaume mwingine na baba akaoa mwanamke mwingine na kuwatelekeza watoto wao kwenye kijumba ambacho muda wowote kitaanguka na kimewekewa miti kusimamisha ukuta,” amesema Malenya.
Kwa kuwa ukuta wa nyumba waliyokuwa wakiishi unakaribia kuanguka, Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Faru Graphite, John De Vries ameahidi kuwajengea nyingine na kuwasomesha.
Hata hivyo, Malenya amewapongeza majirani wa eneo hilo kwa kuwahifadhi watoto hao hasa nyakati za masika na njaa, akitaka wengine waige mfano huo.
=====
Morogoro. Mkuu wa Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, Ngollo Malenya, ameagiza kukamatwa kwa wazazi wawili, Thomas Ulanda na Adelyda Nakashawa kwa kuwatelekeza watoto watatu huku mmoja anayesoma kidato cha nne akiwa ndiye anayewahudumia wenzake.

Kwa kuwa ukuta wa nyumba waliyokuwa wakiishi inakaribua kuanguka, Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Faru Graphite, John De Vries ameahidi kuwajengea nyingine na kuwasomesha.