Almagedoni
Member
- Aug 1, 2022
- 11
- 10
Ikisiri
Nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia afya njema na kunipa nafasi ya kuandika makala hii kuhusu elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum kwa makundi yao. Katika makala hii nimeeleza changamoto zinazowakumba watoto wenye mahitaji maalum katika sekta ya elimu pamoja na namna ya kuondokana na changamoto hizo.
1.0 Utangulizi
Watoto wenye mahitaji maalumu wamegawanyika katika makundi mbalimbali kulingana na mahitaji yao kama vile watoto wenye ulemavu wa akili, ulemavu wa kusikia, ulemavu wa kuona, usonji, ulemavu wa ngozi na ulemavu wa viungo.
2.0 Jitihada za Serikali katika sekta ya elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum
Mosi, niipongeze serikali na wadau wengine wengi na mashirika binafsi kama vile Desk And Chair Foundation, Litifao na Sos, Sibusiso kwa mchango wao mkubwa wa kutilia mkazo suala la elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum.
Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la shule za serikali nchi nzima zenye vitengo kwa ajili ya watoto wenye hali ya ulemavu kupata elimu. Kimsingi jambo hili limesaidia kwa kiasi kikubwa kutoa fursa na haki ya kupata elimu kwa watoto hao. Kwa mfano, jiji la Mwanza lina vitengo 16 kwenye shule za serikali na chuo kimoja cha ufundi ambazo pia huwa na walimu mahiri waliofuzu mafunzo kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini Tanzania. Hili ni ongezeko kubwa lililoleta mapinduzi kwenye elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum.
Kwenye shule hizi watoto hujifunza ujuzi wa kijamii kama vile namna ya kuwasiliana, kushirikiana, kuheshimiana, kusoma, kuhesabu na kuandika kama watoto wasiokuwa na kasoro yoyote. Hali hii imesababisha kupungua kwa vitendo vya unyanyapaaji na ukatili vilivyokuwa vikitokea kwenye jamii zetu kwa kipindi kirefu. Pia, kumekuwa na shuhuda nyingi zinazoonesha namna watoto wenye hali ya ulemavu waliopata fursa ya kwenda shule walivyoleta mabadiliko kwenye familia na jamii zao.
Vilevile, serikali imekuwa ikifadhili utoaji wa chakula katika shule hizo jambo hilo limeongeza mahudhurio ya watoto hao shuleni. Licha ya mafanikio hayo kuna changamoto kadhaa wa kadha ambazo huwakumba watoto wenye mahitaji maalum.
3.0 Changamoto zinazowakabili watu wenye Mahitaji Maalum katika Elimu
Moja, upungufu wa miundombinu bora kama vile madarasa na madawati kumekuwepo na upungufu mkubwa wa madarasa kwa ajili ya watoto wenye hali ya ulemavu. Jambo hili limepelekea watoto kutopata maarifa stahiki. Hivyo jamii inapaswa kutatua jambo hili.
Mbili, ukosefu wa mtaala endelevu, watoto wenye hali ya ulemavu hufundishwa katika hatua, hivyo Kuna hatua ya kwanza hadi ya nne. Lakini mara mtoto ahitimishapo hatua hizo nne hakuna mwendelezo wa kipi asome, hivyo wengi hupandishwa kwenda kujiunga na mfumo wa elimu wa kawaida yaani wa watoto wasiokuwa na mahitaji maalumu. Hali hii hupelekea watoto hawa kutofanya vizuri kwenye masomo. Kutokufanya vizuri huko hupelekea kupata vitendo vya unyanyapaa na ukatili kutoka kwa walimu na watoto wenzao. Hii hupelekea wengi kuacha shule na kurudi mtaani na kuonekana mzigo.
Tatu, umbali wa kituo kinachotoa elimu maalum. Vituo vingi vipo sehemu za mjini hivyo watoto wanatokea familia za vijijini au nje ya miji hushindwa kuhudhuria mara kwa mara kutokana na umbali.
Nne, upungufu wa walimu wenye ujuzi wa kuwafundisha watoto wenye hali ya ulemavu, watoto huwa wengi ukilinganisha na idadi ya walimu waliopo. Mfano mtoto mwenye usonji anapaswa kufundishwa na mwalimu mmoja kwa mtoto mmoja. Watoto wakiwa wengi mwalimu mmoja hushindwa kuwamudu na kuwahudumia kwa kiwango sahihi.
Mwisho, afya duni, watoto hawa huwa na kinga dhaifu dhidi ya maambukizi ya magonjwa hivyo wengi hupatwa na magonjwa mara kwa mara,hali hii huathiri suala zima la ujifunzaji.
4.0 Namna ya kukabiliana na changamoto hizo
Kwanza, miundombinu ikiwemo madarasa kwa ajili ya watoto hawa yajengwe kwa usahihi ikiwemo yawe na choo, bafu na sehemu za kufulia nguo ili watoto hawa waweze kujifunza kwa vitendo mambo ya usafi binafsi. Pia, yawe na njia au barabara ambazo zitawezesha watoto wenye hali ya ulemavu kupita pasipo vikwazo.
Pili, uwepo mtaala endelevu, hii itawezesha pindi mtoto ahitimishapo hatua nne basi anakutana na hatua zingine zenye waalimu wajuzi wa elimu maalumu. Hii itasaidia kuwafanya waendelee kupata maarifa sahihi kwa wakati sahihi. Pia, namna ya kuwafanyia tathimini itakuwa rahisi kwani itaondoa ile ya kufanya mitihani tu bali pia tathimini zingine kama vile ujuzi wa kijamii.
Tatu, Shule nyingi zaidi hasa za msingi ziwezeshwe kuweza kuanzisha vitengo kwa ajili ya watoto wenye hali ya ulemavu. Hii itawezesha kuwapata watoto wengi zaidi walioko vijijini au nje ya miji. Shule za bweni kubwa na nzuri ziongezwe ili kutakua tatizo la umbali.
Nne, walimu wenye ujuzi wa elimu maalumu waongezwe mashuleni , sambamba na utolewaji wa semina kwa walimu na wanafunzi wasio kuwa walemavu ili waweze kuwathamini watoto wenzao wenye hali ya ulemavu.
Tano, asasi zitokeze kufundisha watoto hao stadi za maisha ikiwemo ufundi na upishi, hii itawezesha watoto hawa kuendelea kupata mbinu za kujitegemea kimaisha na kuondoa dhana iliyozoeleka kuwa watoto wenye ulemavu hawawezi.
Mwisho, watoto hawa wapewe bima ya afya ambazo zitawezesha kuhudumiwa kwenye hospitali kubwa. Pia, wadau wa afya wapite mara kwa mashuleni kutoa huduma za afya kwa watoto hao. Ni bayana watoto wengi walio walemavu wametelekezwa na wazazi wao na walio waliobahatika kuishi na wazazi bado familia zao zinahali duni kiuchumi.
5.0 Hitimisho
Nitoe wito kwa jamii kuendelea kuwathamini na kuwajali watoto wenye hali ya ulemavu. Kuendelea kuwafichua wale waliofichwa majumbani kwao itawezesha kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii zetu. Tuendelee kujitoa kwa hali na mali kusaidia familia na watoto wenye ulemavu.

Upvote
3