Watu 11,896 walioondolewa kazini kwa kughushi Vyeti walipwa Tsh. Bilioni 35.2

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameliambia Bunge leo kuwa Fedha hizo zimelipwa kutoka katika Mifuko ya hifadhi ya Jamii ya NSSF na PSSSF ikiwa ni agizo la #RaisSamia kutaka wahusika walipwe stahiki zao.

Fedha hizo ni sehemu ya michango ya Wafanyakazi 14,516 walioondolewa kwa kukosa sifa baada ya zoezi la Uhakiki wa Vyeti uliofanyika kati ya Oktoba 2016 hadi Aprili 2017 kutokana na maalekezo ya #HayatiMagufuli aliyotoa Machi 6 2027 wakati akipokea ripoti ya Uhakiki wa Vyeti.

Aidha, kuhusu malipo ya Wastaafu hadi kufikia Februari 2023, Waziri Mkuu amesema Tsh. Trilioni 1.74 zimelipwa kwa wastaafu 41,949 wa mfuko wa #PSSSF, na upande wa #NSSF wastaafu 43,832 wamelipwa Tsh. Bilioni 72 hadi kufikia Februari 2023.
 
Ni jambo jema
 
Yaani hiyo kitu sitoielewa kabisa, watu wameghushi vyeti kupata kazi(dhulma) wamekuja kujulikana eti wanalipwa badala ya washtakiwe
Hujui kitu kuhusu utumishi wa umma! Kimantiki hawajalipwa bali wamerejeshewa jasho lao walipokuwa kazini.
Huenda baadhi yao walikusaidia hata kukusomesha,kukufundisha,kuku-mentor nk,nk. Ni michango yao. Imereneshwa kwao.
Namsifu sana Samia kuiepuka hii dhuluma ya bwana yule.

Mtu akifukuzwa kazi au akiondoshwa kazini, anazo haki anazostahili. Nyingi tu.
 
Hii ni sawa nakutoa hela mfuko wa kushoto halafu unahamishia wa kulia.
 
Takwimu za wanaostaafu ni kubwa halafu ajira hakuna! Hiiiiiii, Bhagosha.
 
Tsh. Trilioni 1.74 zimelipwa kwa wastaafu 41,949 wa mfuko wa #PSSSF, na upande wa #NSSF wastaafu 43,832 wamelipwa Tsh. Bilioni 72
serikalini kutamu sana huku kwa private ni ovyoovyo pesa kiduchu sana..
 
Hujui kitu kuhusu utumishi wa umma! Kimantiki hawajalipwa bali wamerejeshewa jasho lao walipokuwa kazini.
Huenda baadhi yao walikusaidia hata kukusomesha,kukufundisha,kuku-mentor nk,nk. Ni michango yao. Imereneshwa kwao.
Namsifu sana Samia kuiepuka hii dhuluma ya bwana yule.

Mtu akifukuzwa kazi au akiondoshwa kazini, anazo haki anazostahili. Nyingi tu.
Mkuu usijitoe fahamu kuwa hawa watu wamefanya kosa la udanganyifu, imagine kuna wangapi wanateseka bila Akira ingawa Wana vyeti hali..it's not fair walitakiwa kushtakiwa kabisa!
 
Yaani hiyo kitu sitoielewa kabisa, watu wameghushi vyeti kupata kazi(dhulma) wamekuja kujulikana eti wanalipwa badala ya washtakiwe
Lakini si wametumika.
Kosa lao au serikali iliyowaajiri
 
Mkuu usijitoe fahamu kuwa hawa watu wamefanya kosa la udanganyifu, imagine kuna wangapi wanateseka bila Akira ingawa Wana vyeti hali..it's not fair walitakiwa kushtakiwa kabisa!
Walionewa jiwe anakuwa anapunguza idadi ya kulipa wafanyakazi,pia kuwakomoa watumishi KWA sababu walimpigia kura Lowasa
 
Hujui kitu kuhusu utumishi wa umma! Kimantiki hawajalipwa bali wamerejeshewa jasho lao walipokuwa kazini.
Huenda baadhi yao walikusaidia hata kukusomesha,kukufundisha,kuku-mentor nk,nk. Ni michango yao. Imereneshwa kwao.
Namsifu sana Samia kuiepuka hii dhuluma ya bwana yule.

Mtu akifukuzwa kazi au akiondoshwa kazini, anazo haki anazostahili. Nyingi tu.
Washitakiwe kwa kughushi, au hilo sio kosa?
 
Back
Top Bottom