KERO Watu 178 tuliitwa kuripoti kazini VETA Dodoma, Februari 14, 2026, mpaka sasa hatujapangiwa vituo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni miongoni mwa Watu 178 walioitwa kuripoti kazini na VETA tangu tarehe 14 Februari 2026.

Tulifika Ofisi za VETA Dodoma tukajaza taarifa binafsi, kisha tukaambiwa tusubiri maelekezo mengine… lakini hadi leo tunaingia mwezi wa tatu tunasubiri taarifa za kupangiwa vituo vya kazi na hakuna update ya kueleweka tunayopewa zaidi ya kuwa "utaratibu haujakamilika".

Hii hali itaendelea hadi lini, mbona wanatufanya kama misukule?
 
Mtuvumilie. Hela za kuwapangia vituo zimetumika kwenye "matumizi mengineyo". Mwezi Julai tujitahidi tuwapangie vituo vyenu.
 
Mambo ya serikalini ndio yalivyo. Kuwa na subra
 
Ma gen z sijui kwanini huwa hamna subra. Mnapenda kila kitu kifanyike papo kwa papo.
 
Duh , vuta subira kijana . kazi zikianza utadodge vya kutosha .
 
ambo ya Serikali ni kama mwendo wa kinyonga yanaenda taratibu pengine taratibu mno kuliko kobe, unaweza kumaliza miezi 6 au mwaka hujaitwa kazi kama kuna sehemu umejishikilia usiache kazi kama hujaitwa rasmi kazini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…